Mfalme Daudi natanguliza pole ikiwa usemayo ni kweli ila ikiwa kuna mengine pia pole binadamu hatujakamilika si wewe wala si huyo ndugu yetu.
Dada rejea comment katika post yako , kuna mtu ameahidi njia ya kuepukana na malipo ya hao wenye solar ili upunguze machungu ya majukumu yanayokuandama , mtafute tafadhali alafu iuze hiyo solar ikusaidie kwenye mambo mengine.
Dada ukibahatika kuuza solar , hakika deni la mkopo wako utaweza kulilipa ila bada ya hapo , jikaze umpate unayemuamini katika mgahawa wako ili uendelee kupambana , mimba miezi sita bado kwa kiasi chake hivyo mtafute msaidizi katika mgahawa wako kabla ya siku za uchovu wa mimba kuzidi.
Dada
Mfalme Daudi natambua umeathirika kisaikolojia juu ya huyo mwanaume , Ndugu yangu jikaze ni wakati mgumu ila nikukumbushe kuwa muda ni mponyaji mzuri , jitahidi kuwqza ya kuwa mlikuwa wote ila sasa hayupo tena ...
Pole sana ndugu , amka simama endelea na mwendo hajakuangusha ila kakuimarisha
Ushauri tu.
TEKERI.[emoji120][emoji120]
Sent from my SM-J410F using
JamiiForums mobile app