Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Ijumaa tarehe 20 saa 1:15 asubuhi haikuwa siku njema kwangu, nilifika stesheni ya SGR nikiwa na furaha ya kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam, baada ya kukaguliwa tikiti yangu nikaambiwa niweke begi kwenye mtambo wa ukaguzi kisha nikaenda upande wa pili wa mtambo kulipokea begi.
Nilipofika upande wa pili nikasikia askari akitaka kumjua mwenye begi ambalo ni langu, nikajitokeza, kwa mshituko nikajikuta nipo kati ya askari watatu kijasho kilanitoka, nikaambiwa ndani ya begi kuna chupa ya maji, nikatakiwa niitoe, nikaitoa. Nikawaambia hayo ni maji yangu ya kunywa endapo nitahitaji kama ikitokea, wakati huo watu wameacha mazungumzo yao wakishuhudia kukamatwa kwa msafirishaji wa maji ya kunywa mil.500!
Kitendo cha kunihoji kijinai kilitaka kunifanya nivunje safari yangu ya SGR, baada ya mahojiano niliamriwa hiyo chupa ya maji mil.500 niiache kwenye kaunta yao alipo askari! Ndugu zangu hapo ndipo nilipojua si lazima uwe mwizi ili uende jela, mmoja wa askari aliniambia kosa hilo endapo ningeingia nayo ndani ya treni ni faini ya shilingi 500,000/=! Ninajuta kupanda SGR.
Kiongozi, Pole sana; hata hivyo ni utaratibu wa kawaida kabisa; ukitumia usafiri kama meli na hata ndege , wakiscreen wakaona kitu ambacho hakiruhusiwi unaambiwa utoe; kama ni mwelewa ukatoa ushirikiano haikutumii hata dakika mbili labda kama ni kitu hatarishi kama silaha, chemikali au madawa ya kulevya.
Ni muhimu pia kujua kuwa vitu vyenye presha (gasi) ndani kama perfume nk haviruhusiwi kuingia navyo ndani ya ndege labda iwe ndogo sana 100mil
Huyo aliyekuambia sijui faini ya 500,000 wala hakuwa na haja ya kufika huko kwani maji ni kitu cha kawaida kwa mazingira ya kitanzania mtu kujisahau na kuingia nayo