Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!

Unakataza mtu kupanda treni na maji na vinjwaji, vipi kama mtu mgonjwa anatakiwa kunywa dawa na chakula, akishindwa na kufa kosa la nani hapo?

Kampuni ya reli haiwezi kishtakiwa kwa kisababisha kifo hicho?
Maji, viywaji na Chakula vinauzwa ndani ya treni kwa bei ya kizalendo; Mfano, Maji ya lita moja shs 1000
 
Mkuu kumbuka utamaduni wa tz , kumbuka hii treni inapopita , unataka watu wajiharishie ndani ya sgr, waulizeni wamiliki wa mabasi yanayopita huko kwenda mwanza ni shida TUpu.

Ukimwachilia mswali mshamba afanye anavyotaka sgr itanuka mavi na kunguni.

Tuendelee kuintuza sgr yetu
Kusumbuliwa na tumbo si lazima ule maji! Vichaa ni wengi.
 
Ni hatarishi kwa usalama wa abiria na treni.
Kwa namna gani? Kwenye bus huwa napenda kusafiri na maji kuhakikisha nakunywa maji ya kutosha, nisiwe dehidrated. Kama ni hivyo si wangetoa elimu kwa umma ili raia wakisafiri kwa SGR wasichukue maji ya kunywa kwa sababu za kiusalama? Ni kweli kama mtu hujawahi kuhojiwa na polisi, siku ukijikuta unahojiwa unapaniki sana, maana hautakuwa na uhakika kama issue itaishia hapo tu au utajikuta kwenye tatizo lingine (kulingana na maelezo ya baadhi ya watu waliokwishapitia hali hiyo).
 
Ukitaka ujue Watanzania bado kiza ukipita Mtera dam utasikia msipige picha hapa na wanaopiga picha wanawasumbua wakati Dunia imezungukwa na satellite ambayo inaweza kuchukua picha hata ya sisimizi popote pale juu ya uso wa Dunia..
Hizo cautions zipo sehemu nyingi tu ila zipo Kwa ajili ya kina sisi, wageni haziwahusu
Kivukoni pale wanzuia kupiga picha ila wazungu wanapiga mchana kweupe na Wala hawazuiliwi, piga wewe Sasa nyani mwenzako uone watakavokuoshea
 
Mkuu kumbuka utamaduni wa tz , kumbuka hii treni inapopita , unataka watu wajiharishie ndani ya sgr, waulizeni wamiliki wa mabasi yanayopita huko kwenda mwanza ni shida TUpu.

Ukimwachilia mswali mshamba afanye anavyotaka sgr itanuka mavi na kunguni.

Tuendelee kuintuza sgr yetu
Kwahiyo wanavyoviuza humo ndo vina uhakika wa watu kutoharisha?? Hii hoja yako haina mashiko labda tu km wangekuwa wamepiga marufuku kabisa kula chochote tangu mwanzo hadi mwisho wa safari au la uwe ni mnufaika wa hiyo sheria yao,

Kunguni hawaletwi na kula kula ovyo wala hawasababishi kipindupindu, mpaka hapo huna hoja
 
Ijumaa tarehe 20 saa 1:15 asubuhi haikuwa siku njema kwangu, nilifika stesheni ya SGR nikiwa na furaha ya kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam, baada ya kukaguliwa tikiti yangu nikaambiwa niweke begi kwenye mtambo wa ukaguzi kisha nikaenda upande wa pili wa mtambo kulipokea begi.

Nilipofika upande wa pili nikasikia askari akitaka kumjua mwenye begi ambalo ni langu, nikajitokeza, kwa mshituko nikajikuta nipo kati ya askari watatu kijasho kilanitoka, nikaambiwa ndani ya begi kuna chupa ya maji, nikatakiwa niitoe, nikaitoa. Nikawaambia hayo ni maji yangu ya kunywa endapo nitahitaji kama ikitokea, wakati huo watu wameacha mazungumzo yao wakishuhudia kukamatwa kwa msafirishaji wa maji ya kunywa mil.500!

Kitendo cha kunihoji kijinai kilitaka kunifanya nivunje safari yangu ya SGR, baada ya mahojiano niliamriwa hiyo chupa ya maji mil.500 niiache kwenye kaunta yao alipo askari! Ndugu zangu hapo ndipo nilipojua si lazima uwe mwizi ili uende jela, mmoja wa askari aliniambia kosa hilo endapo ningeingia nayo ndani ya treni ni faini ya shilingi 500,000/=! Ninajuta kupanda SGR.
Ungepanda na maji ya Kilimanjaro Wala wasingekusumbua, Juzi nimepanda na maji ya Knjaro Toka Dom Hadi Dar Tena nimepita getin huku nimeyabeba mkononi tu, labda walitishika kutokana na sare nilizovaa
 
Bahati mbaya nilikuwa natoka Morogoro ya Tanzania, hatutumii pasipoti kusafiri.
Ndiyo hivyo utaratibu. Kuna kabila huko kusini nyumani kwetu akanunua basi nadhani unajua buti la zungu basi zile siti za VIP wenyeji wakawa wakikata ticket wanaenda kukaa zile siti then wanafukuzwa baadaya wakazila kupanda zile gari wakisema zinanyanyasa kwa sababu unakata ticket halafu unazuiwa kukaa siti nzuri hahah
 
Ungepanda na maji ya Kilimanjaro Wala wasingekusumbua, Juzi nimepanda na maji ya Knjaro Toka Dom Hadi Dar Tena nimepita getin huku nimeyabeba mkononi tu, labda walitishika kutokana na sare nilizovaa
Treni imejaa ulimbukeni na ushamba ndiyo sababu wanakataza mifuko ya vitambaa inayoruhusiwa kisheria.
 
Ndiyo hivyo utaratibu. Kuna kabila huko kusini nyumani kwetu akanunua basi nadhani unajua buti la zungu basi zile siti za VIP wenyeji wakawa wakikata ticket wanaenda kukaa zile siti then wanafukuzwa baadaya wakazila kupanda zile gari wakisema zinanyanyasa kwa sababu unakata ticket halafu unazuiwa kukaa siti nzuri hahah
Kila abiria ndani ya basi anapewa tikiti ikionesha namba ya kiti, hata hilo basi utaratibu uko hivyo.
 
Ungepanda na maji ya Kilimanjaro Wala wasingekusumbua, Juzi nimepanda na maji ya Knjaro Toka Dom Hadi Dar Tena nimepita getin huku nimeyabeba mkononi tu, labda walitishika kutokana na sare nilizovaa
Itakua ulivaa sare za ukada au Kaunda suti, kina sisi wanatusimamisha Kwa makofi
 
Waliotunga hizo Sheria ni wajinga na wapumbavu.je kama mgonjwa anatakiwa anywe dawa inakuwaje?maji hayana tishio lolote Kwa sgr ni upunguani wa walioziweka hizo sheria
 
Kwamba hata maji ya kunywa hawataki? Yani nimenunua chupa yangu ya lita moja, nikainywa robo ikabaki robo tatu, hawataki nipande nayo?

Kwani shida ni nini?
Ipo hivi, hawakazati maji kama maji, bali wanakataza maji kwa sababu watu waneza kuchukua advantage ya maji badala yake wakaweka milipuko.
Kama umewahi kutumia usafiri wa anga procedure ni kuwa hairuhisiwi kuingia kwenye cabin ukiwa na baadhi ya vimiminika kama lotions nk, kinacholengwa pale ni mafuta ya glycerin ambayo yanaweza kutumika kama bomu.
 
Kuna mdada alikuwa na nepi na vinguo vingine kwenye mfuko vya mtoto mchanga wakamlazimisha anunue boksi lao kwa shs. 1,000/=! Huu ni upumbavu uliokithiri.
 
Ijumaa tarehe 20 saa 1:15 asubuhi haikuwa siku njema kwangu, nilifika stesheni ya SGR nikiwa na furaha ya kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam, baada ya kukaguliwa tikiti yangu nikaambiwa niweke begi kwenye mtambo wa ukaguzi kisha nikaenda upande wa pili wa mtambo kulipokea begi.

Nilipofika upande wa pili nikasikia askari akitaka kumjua mwenye begi ambalo ni langu, nikajitokeza, kwa mshituko nikajikuta nipo kati ya askari watatu kijasho kilanitoka, nikaambiwa ndani ya begi kuna chupa ya maji, nikatakiwa niitoe, nikaitoa. Nikawaambia hayo ni maji yangu ya kunywa endapo nitahitaji kama ikitokea, wakati huo watu wameacha mazungumzo yao wakishuhudia kukamatwa kwa msafirishaji wa maji ya kunywa mil.500!

Kitendo cha kunihoji kijinai kilitaka kunifanya nivunje safari yangu ya SGR, baada ya mahojiano niliamriwa hiyo chupa ya maji mil.500 niiache kwenye kaunta yao alipo askari! Ndugu zangu hapo ndipo nilipojua si lazima uwe mwizi ili uende jela, mmoja wa askari aliniambia kosa hilo endapo ningeingia nayo ndani ya treni ni faini ya shilingi 500,000/=! Ninajuta kupanda SGR.

Hata kwenye ndege huruhusiwi... Standard lazima zizingatiwe
 
Walikuona mlugaluga. Walitakiwa wakuambie uyaache tu hayo maji usipande nayo treni. Hao walinzi hawana common sense. Wao wako kama Bobby akiambiwa shika anashika.
Hao walinzi nao chenga. Walitakiwa tu wamuambie aache maji. Kazi kwelikweli. Airport viwembe, viliminika zaidi ya mls 100 hutakiwi kuingia navyo ndani. Kiroho safi tu wanakuambia uviache au uweke kwenye begi ambalo litawekwa kwenye mizigo
 
Kwa namna gani? Kwenye bus huwa napenda kusafiri na maji kuhakikisha nakunywa maji ya kutosha, nisiwe dehidrated. Kama ni hivyo si wangetoa elimu kwa umma ili raia wakisafiri kwa SGR wasichukue maji ya kunywa kwa sababu za kiusalama? Ni kweli kama mtu hujawahi kuhojiwa na polisi, siku ukijikuta unahojiwa unapaniki sana, maana hautakuwa na uhakika kama issue itaishia hapo tu au utajikuta kwenye tatizo lingine (kulingana na maelezo ya baadhi ya watu waliokwishapitia hali hiyo).
Kuna kundi la wafanyakazi wameamua kujinufaisha kwa kufanya biashara za kijinga za kulazimishana.
 
Back
Top Bottom