Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!

Ipo hivi, hawakazati maji kama maji, bali wanakataza maji kwa sababu watu waneza kuchukua advantage ya maji badala yake wakaweka milipuko.
Kama umewahi kutumia usafiri wa anga procedure ni kuwa hairuhisiwi kuingia kwenye cabin ukiwa na baadhi ya vimiminika kama lotions nk, kinacholengwa pale ni mafuta ya glycerin ambayo yanaweza kutumika kama bomu.
Sasa mkuu, treni imekuwa ndege? Alafu si wanafanya ukaguzi? Kama wameona ni maji ya kawaida tu shida iko wapi?
 
Ukitaka ujue Watanzania bado kiza ukipita Mtera dam utasikia msipige picha hapa na wanaopiga picha wanawasumbua wakati Dunia imezungukwa na satellite ambayo inaweza kuchukua picha hata ya sisimizi popote pale juu ya uso wa Dunia..
Google map inafanya kila kitu
 
Walikuona mlugaluga. Walitakiwa wakuambie uyaache tu hayo maji usipande nayo treni. Hao walinzi hawana common sense. Wao wako kama Bobby akiambiwa shika anashika.
Sasa mtu anatoka porini JKT halafu anapewa kazi ya ulinzi unatarajia afanye nini kama siyo matumizi ya mabavu kuliko akili?
 
M
Sasa mkuu, treni imekuwa ndege? Alafu si wanafanya ukaguzi? Kama wameona ni maji ya kawaida tu shida iko wapi?
Mkuu vimiminika vimekuwa issue kwenye ndege maana ni ngumu sana kutofautisha kati ya glycerin na vimiminika salama, ndio sababu ili isiwe shida vikawa banned
Unaweza ona chupa ya maji safi kumbe ndani mtu keshamix na smart gin anaenda kuleta fujo kwenye behewa.
Ndo mana kama unataka maji basi nunua maji yao ndani
 
Tanzania ina Askari wajinga sana.
Ijumaa tarehe 20 saa 1:15 asubuhi haikuwa siku njema kwangu, nilifika stesheni ya SGR nikiwa na furaha ya kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam, baada ya kukaguliwa tikiti yangu nikaambiwa niweke begi kwenye mtambo wa ukaguzi kisha nikaenda upande wa pili wa mtambo kulipokea begi.

Nilipofika upande wa pili nikasikia askari akitaka kumjua mwenye begi ambalo ni langu, nikajitokeza, kwa mshituko nikajikuta nipo kati ya askari watatu kijasho kilanitoka, nikaambiwa ndani ya begi kuna chupa ya maji, nikatakiwa niitoe, nikaitoa. Nikawaambia hayo ni maji yangu ya kunywa endapo nitahitaji kama ikitokea, wakati huo watu wameacha mazungumzo yao wakishuhudia kukamatwa kwa msafirishaji wa maji ya kunywa mil.500!

Kitendo cha kunihoji kijinai kilitaka kunifanya nivunje safari yangu ya SGR, baada ya mahojiano niliamriwa hiyo chupa ya maji mil.500 niiache kwenye kaunta yao alipo askari! Ndugu zangu hapo ndipo nilipojua si lazima uwe mwizi ili uende jela, mmoja wa askari aliniambia kosa hilo endapo ningeingia nayo ndani ya treni ni faini ya shilingi 500,000/=! Ninajuta kupanda SGR.
 
M

Mkuu vimiminika vimekuwa issue kwenye ndege maana ni ngumu sana kutofautisha kati ya glycerin na vimiminika salama, ndio sababu ili isiwe shida vikawa banned
Unaweza ona chupa ya maji safi kumbe ndani mtu keshamix na smart gin anaenda kuleta fujo kwenye behewa.
Ndo mana kama unataka maji basi nunua maji yao ndani
Inaonesha haujawahi kusafiri kwa treni, ndani ya treni imo baa inauza pombe.
 
Mkuu kwenye flight, tunaruhusiwa kuingia na chakula vinywaji na kuvitumia humohumo kwenye flight?.

Na sgr ndio iko hivyo kama flight, zimetumika pesa zenu za Kodi na tozo, kuweni na huruma jamani na pesa za serikali.

Hatuwezi kuruhusu watu waje na vitumbua, bagiya, mayai ya kuchemsha, wali wa maharage, humo ndani ya sgr itakuwaje, ?
Tatizo haujawahi kupanda treni, kuna hoteli na baa.
 
Treni ya asibuhi saa 1:30 ikitokea Dodoma haikujaza abiria, dalili za mwanzo wa kifo. Stesheni ya sgr Moro iko mbali sana na hakuna daladala huku bodaboda sh 5,000/=! Barabara ni njia iliyotengenezwa na magurudumu ya malori wakati wa ujenzi ni vumbi na kokoto. Ukifika stesheni utaona wasafiri ni kundi la wenye uwezo.
 
Ijumaa tarehe 20 saa 1:15 asubuhi haikuwa siku njema kwangu, nilifika stesheni ya SGR nikiwa na furaha ya kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam, baada ya kukaguliwa tikiti yangu nikaambiwa niweke begi kwenye mtambo wa ukaguzi kisha nikaenda upande wa pili wa mtambo kulipokea begi.

Nilipofika upande wa pili nikasikia askari akitaka kumjua mwenye begi ambalo ni langu, nikajitokeza, kwa mshituko nikajikuta nipo kati ya askari watatu kijasho kilanitoka, nikaambiwa ndani ya begi kuna chupa ya maji, nikatakiwa niitoe, nikaitoa. Nikawaambia hayo ni maji yangu ya kunywa endapo nitahitaji kama ikitokea, wakati huo watu wameacha mazungumzo yao wakishuhudia kukamatwa kwa msafirishaji wa maji ya kunywa mil.500!

Kitendo cha kunihoji kijinai kilitaka kunifanya nivunje safari yangu ya SGR, baada ya mahojiano niliamriwa hiyo chupa ya maji mil.500 niiache kwenye kaunta yao alipo askari! Ndugu zangu hapo ndipo nilipojua si lazima uwe mwizi ili uende jela, mmoja wa askari aliniambia kosa hilo endapo ningeingia nayo ndani ya treni ni faini ya shilingi 500,000/=! Ninajuta kupanda SGR.
Jamani iishie huko huko Dar sisi wasukuma lazima tupande na bata wetu sembuse maji
 
usipaki gari hapo wewe unapaki. Tusikukamate kweli?

usipite hapa kuna mbwa wakali, wewe unapita. Mbwa wakali watakuacha kweli?

Ni muhimu kua makini na kuuliza vitu vinavyokwenda maeneo mbalimbali nchini 🐒
 
Wabongo wanapenda sana kulalamika. It's simple hununui wala kula chakula au maji yao. Trip ya masaa matatu na nusu usipokula au kunywa maji utakufa? Wakikutaza maji yako kunywa yaishe au yamwage uwakomoe 🤣🤣
Safari ya 2hrs mtu anataka ale ndio maana huwa tunashikwa na tumbo la kuhara,😂😂😂
 
Back
Top Bottom