Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!


Kiongozi, Pole sana; hata hivyo ni utaratibu wa kawaida kabisa; ukitumia usafiri kama meli na hata ndege , wakiscreen wakaona kitu ambacho hakiruhusiwi unaambiwa utoe; kama ni mwelewa ukatoa ushirikiano haikutumii hata dakika mbili labda kama ni kitu hatarishi kama silaha, chemikali au madawa ya kulevya.
Ni muhimu pia kujua kuwa vitu vyenye presha (gasi) ndani kama perfume nk haviruhusiwi kuingia navyo ndani ya ndege labda iwe ndogo sana 100mil
Huyo aliyekuambia sijui faini ya 500,000 wala hakuwa na haja ya kufika huko kwani maji ni kitu cha kawaida kwa mazingira ya kitanzania mtu kujisahau na kuingia nayo
 
Haijalishi bei ya kawaida ni bei gani lakini hilila kukataza watu kupanda na maji ya kunywa ni jambo la kupumbavu mno. CCM kuna siku itapata inachokitafuta.
mkuu sheria ni mbaya ndio ila usilete siasa kila mahali,
Hata nchi tukiwapa Chadema haitakuwa unafanya kila unachotaka, na hio sheria haitafutwa hata kije chama gani
 
Walikuona mlugaluga. Walitakiwa wakuambie uyaache tu hayo maji usipande nayo treni. Hao walinzi hawana common sense. Wao wako kama Bobby akiambiwa shika anashika.
Tanzania hawana mluga mluga wala nini Mkuu mtu yeyote akiwa kwenye nafasi anaitumia atakavyo kwa mtu yeyote na ni kukosa ustaarabu tu..hapo si walitakiwa wampe maelekezo mazuri tu kuwa humu vinywaji havitakiwi maana sio ndege ile yeye alichukulia kama usafiri wa Bus tu.
 
Kwasisi wenye sukari na presha, tunaotakiwa kula vyakula maalum, sheria inakuwaje sasa?
naamini vyakula vitakuwepo
hata hivyo kutoka dar kwenda moro ni lisaa na nusu sijui kama mtu anahitaji kula au pengine kutoka dar kwenda Dodoma ni masaa 3 naona kama sio muda mrefu sana japo kula ni uamuzi wa mtu na bajeti yake
 
Muwe mnasoma masharti,

Sgr inakataza kupanda na vyakula na vinywaji, wew unapanda nayo, ukipigwa fine hata Million ni uzembe hutakiwi kulalamika,

Btw, hizo sheria ni za kipuuzi, ila ndio hivyo zipo inabidi tuzifuate
Unakataza mtu kupanda treni na maji na vinjwaji, vipi kama mtu mgonjwa anatakiwa kunywa dawa na chakula, akishindwa na kufa kosa la nani hapo?

Kampuni ya reli haiwezi kishtakiwa kwa kisababisha kifo hicho?
 
Kesho napanda na maji lita moja nione watanifanyaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…