Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!

Mkuu, hizo ni sheria kwenye biashara, hata kwenye ndege hupandi na maji, uwe ulaya au bongo,
Na huko ni CCM ?
Wabongo wanapenda sana kulalamika. It's simple hununui wala kula chakula au maji yao. Trip ya masaa matatu na nusu usipokula au kunywa maji utakufa? Wakikutaza maji yako kunywa yaishe au yamwage uwakomoe 🀣🀣
 
Hiyo siyo offense bosi, mbona kwenye ndege pia huwa hatupandi nayo labda yale ambayo umeshanunua baada ya kuchek in. Kuzuia maji ni kuzuia ugaidi basi
 
Mhu! Ni kinyume cha sheria kuwa na maji ya kunywa kwenye treni ya SGR au sijaelewa?
 
naamini vyakula vutakuwepo
hata hivyo kutoka dar kwenda moro ni lisaa na nusu sijui kama mtu anahitaji kula au pengine kutoka dar kwenda Dodoma ni masaa 3 naona kama sio muda mrefu sana japo kula ni uamuzi wa mtu na bajeti yake
Wanachekesha sana hawa. Safari ya masaa matatu unataka kula? Kwamba ukisubiri ufike utakufa na njaa au kiu?
 
Kwamba ukipanda na vyakula inakuwa nini naona sheria imekaa kimchongo kuna kigogo kapewa tenda ya umamantilie auze kwa bei ya kukomoana wanachojali wao ni mifuko yao tu
Mkuu kumbuka utamaduni wa tz , kumbuka hii treni inapopita , unataka watu wajiharishie ndani ya sgr, waulizeni wamiliki wa mabasi yanayopita huko kwenda mwanza ni shida TUpu.

Ukimwachilia mswali mshamba afanye anavyotaka sgr itanuka mavi na kunguni.

Tuendelee kuintuza sgr yetu
 
Kubeba vimiminika na vyakula hata mimi sikubaliani navyo maana wakisharuhusu mle ndani kutakuwa pachafu sana na ni ngumu kucontrol bora kama wangekuwa wanagawa wenyewe kama kwenye ndege.

Ila namna ambayo ukikutwa na hivyo vitu unakuwa treated ndo sijapenda hata Airport ambapo ni high risk zaidi ila wanakuwaga wastaarabu sana. May be mzee umetunisha sana misuli na ukavaa kizibao 🀠🀠
 
Hiyo siyo offense bosi, mbona kwenye ndege pia huwa hatupandi nayo labda yale ambayo umeshanunua baada ya kuchek in. Kuzuia maji ni kuzuia ugaidi basi
Ugaidi wa chupa ya maji ambayo imethibitishwa kuwa ni maji! Kaombe kazi polisi utunyoreshe.
 
Wewe ilibidi ufungwe hata mwezi mmoja jela kwa upumbavu wako. Sheria hapo ni kutopanda na maji halafu kwa makusudi unataka uingie na chupa ya 500ml ulitaka wakuchekee? Wangekulima faini ili iwe fundisho kwa wengine wasiotaka kufuata utaratibu.
 
Kiti nilichokaa sehemu ya kuweka miguu kulikuwa na pakiti ndogo ya kahawa, kikombe cha karatasi na kipakiti kidogo cha sukari vilivyotumika vikatupwa chini, niliwaita wahudumu waondoe lakini mpaka nafika Dar hawakuviondoa.
 
Walikuona mlugaluga. Walitakiwa wakuambie uyaache tu hayo maji usipande nayo treni. Hao walinzi hawana common sense. Wao wako kama Bobby akiambiwa shika anashika.
Kabisa ni swala la common sense tu, hapo wameonyesha hawana tofauti na mashine.
 
Wabongo wanapenda sana kulalamika. It's simple hununui wala kula chakula au maji yao. Trip ya masaa matatu na nusu usipokula au kunywa maji utakufa? Wakikutaza maji yako kunywa yaishe au yamwage uwakomoe 🀣🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Kaka hii imenikumbusha siku jamaa alipiga lita moja chap pale Nyerere. Bahati mbaya nikakaa naye seat moja na mle ndani akagonga bia mbili alipiga route sana za toilet.
 
Ulaya huku kwenye maendeleo na IQ kubwa unaingia hadi na soda na big mac chocolate mazagazaga kibao ya msosi. Ila nyie thed weld dwellers bana yani maji tu. Ndo maana hiyo treni ya SRG iliyogharimu trillion 17 za mkopo inakatiza vichakani huko watu wanapokunya.
 
Naomba maelekezo hapa Kuna tatizo Gani kupanda na maji yangu sgr na kununua maji sgr?

Nini utofauti na maji yangu yanaweza iharibu vipi sgr na ya ndani ya sgr yasiiharibu?
 
Mkuu, hizo ni sheria kwenye biashara, hata kwenye ndege hupandi na maji, uwe ulaya au bongo,
Na huko ni CCM ?
Nani mkweli hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…