Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!

usipaki gari hapo wewe unapaki. Tusikukamate kweli?

usipite hapa kuna mbwa wakali, wewe unapita. Mbwa wakali watakuacha kweli?

Ni muhimu kua makini na kuuliza vitu vinavyokwenda maeneo mbalimbali nchini πŸ’
Maji ya kunywa hayasimamiwi na bodi ya vileo, maji ya kunywa ni haki ya kila kiumbe kilicho hai na ruhusa kunywa wakati wowote na mahali popote.
 
Kesho napanda na maji lita moja nione watanifanyaje
Haha,
Mkuu, si umesikia faini yake ni 500k ?

Andaa tu na pesa ya faini kuepusha usumbufu mambo yasiwe mengi πŸ˜‚ Ukidakwa tu unalipa, usisumbue watu kuja kukutoa ndani kwa dhamana
 
Nikajua chupa ya milioni 500πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„.
 
Hujatuhumiwa kusafirisha chupa mil.500 bali ulifanya kosa la kutaka kusafiri na maji ya kunywa ndani ya treni ya SGR kinyume cha sheria, na uliendelea na safari baada ya kufuata utaratibu uliopo.
 
Inaonesha haujawahi kusafiri kwa treni, ndani ya treni imo baa inauza pombe.
Hii Sgr haina buffet car, ila kila behewa linajitegemea na huduma za vinywaji na cha kula na utahudimiwa na mhudumu husika kwa behewa husika.
Halafu sio kwamba wantakataza unnywaji wa pombe ukiwa ndani ya behewa maana hata wao wanauza pombe , Trc wanataka supply ya food and bevarage iwe juu yao kwa usalama wa kiwango chao.
 
Maji ya kunywa hayasimamiwi na bodi ya vileo, maji ya kunywa ni haki ya kila kiumbe kilicho hai na ruhusa kunywa wakati wowote na mahali popote.
Maji ni uhai na kwakweli ni muhimu mno kwa kila moja.
Lakini kwenye maeneo ya mikusanyiko yana utaratibu wake ambao uko wazi kabisaa.
Na maeneo yale nadhani kuna mabango ya kutosha kuhusu kipi kinaruhusiwa na kipi hakiruhusiwi...

Hata hivyo,
ungalikua umeishikilia mkononi maji yako, wangekuuliza nawe ungejieleza labda una tatizo na kwahivyo maji kwako ni dawa, hilo tatizo halingekua kubwa kiasi hicho..

Hata hivyo,
pole sana bilashaka kuna jambo umejifunza πŸ’
 
Ccm inahusikaje hapa??
 
Muwe mnasoma masharti,

Sgr inakataza kupanda na vyakula na vinywaji, wew unapanda nayo, ukipigwa fine hata Million ni uzembe hutakiwi kulalamika,

Btw, hizo sheria ni za kipuuzi, ila ndio hivyo zipo inabidi tuzifuate

Labda masharti ya waganga wa kienyeji. Masharti mengine huwa hatusomi kabisa
 
Mkuu soma masharti ya kupNda SGR.
Ungekuwa umesoma hayo masharti usingepata usumbufu.
 
Mil. 500 ndo nini?
Mimi baada ya kusoma nilishindwa kuelewa mil.500
Inaingiaje hapo
Ila baada ya kuzisoma comments nikaona wote wanaona sawa tu
Ningekosoa ila nikasema labda ndio lugha yenu hiyo
Mil.500 na 500ml utofauti ni mkubwa sana ila wote wameelewa naona kasoro mimi na wewe πŸ˜„ 🀣 πŸ˜‚
Na wewe uko Brazil kama mimi πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…