Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Kwa mkopo wa miaka 8 yaani Ile mikopo ya unafunga ndoa unazaa mtoto yupo darasa la tatu ndo mkopo unaisha riba hio ni sawa.
Mkopo ni laana Kama sio lazima ya ugonjwa au kusoma acha na kukopa bora ujenge taratibu taratibu.
Mkopo usizidi miaka 3
 
Ndo maana Serikali iliweka ukomo wa kukopa ni robo ya tatu bila hivyo wengi wangeacha kazi.
Japo haisaidii bado watumishi wanapigwa kwenye salary advance plus wazee wa kuzuia card na password yako ili mwisho wa mwezi wakachukue kwenye ATM mkopo wao
 
Wakuu eleweni kitu kimoja, naona wengi wetu tunachangia kwa kujiamini afu tunachangia uongo.

Benki haitumii hizi hesabu zetu za madukani kwamba ukiambiwa riba ni 17% kwa mwaka maana yake kwa miaka mitano utachukua tu 17% × 5 upate 85%, hizi ni hesabu za form one simple interest[emoji2]

Kumaliza utata mtoa mada aseme alikopa benki gani, kwa riba gani na muda gani.
 
Tusitishane jamani interest rate kwa mwaka ni Kati ya 16% mpaka 18% kwa mwaka kwa mabank haya tunayoyafahamu. Ukizidisha hiyo Raye na let say miaka mitano ya kulipia bado haifiki hata 100%. Ukute mtoa Mada alitaka arudishe pesa ndani ya miaka kumi.
Dah mkopo wa muda mrefu nao kasheshe
 
Hizi microfinance ni janga kwa taifa na sijui kwa nini serikali imekaa kimya. Yaani mkopo una vigarama vilejificha kibao. Yaani kukopa huku ni kujichimbia kaburi mwenyewe. Wana mikataba mirefu halafu ukifika wanakuambia sign harakaharaka. Nilienda Platnum kutaka kukopa 3M kwa miezi 4 hesabu zanataka nitudisje 4.7 sijui. Huu ni wizi kwa watanzania
 
Ila ndo 10M kwa 24M ? riba 100%+ huu ni wizi aisee
Sio wizi ila sisi sio waelewa wa masuala ya mikopo. Mfano wanakuambia riba ni 14 % Kwa mwaka, maana yake ni kwamba kama mkopo utakuwa wa miaka nane riba itakuwa 14% zidisha Kwa miaka 8 = 112%
Kama umechukua mkopo wa million 10 utarudisha zaidi ya million 22 Kwa hiyo miaka nane.
Ushauri wangu ni vyema tukope mikopo ya muda mfupi, napendekeza isizidi miaka 3.

Mfano wa pili kama angechukua hiyo hiyo million 10 Kwa miaka mitatu ingekuwa hivi;
14% zidisha Kwa miaka 3= 42%
Hapa angerudisha million 14 na laki kadhaa.
42÷100x1000000= 4,200,000/= hii ndio riba ukijumlisha na ile million 10 ndio unapata 14,200,000/=
 
Hii ni chai hakuna riba ya bank unaweza chukua 10 ukalipa 24 m kama riba haipo mkuu...riba ni 13% kwa bank nyingi...hiyo milion 12 imezidi saana haiwezi zidi 5m kama riba..ambapo riba plus interest unaweza kulipa milion 17 hapo umedanganya umma

Ila kama ulichukua kwenye sacoss ni kweli saccos riba zao ni kwa mwezi..ila bank riba zao ni annualy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…