Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Kwa mkopo wa miaka 8 yaani Ile mikopo ya unafunga ndoa unazaa mtoto yupo darasa la tatu ndo mkopo unaisha riba hio ni sawa.
Mkopo ni laana Kama sio lazima ya ugonjwa au kusoma acha na kukopa bora ujenge taratibu taratibu.
Mkopo usizidi miaka 3
 
Ndo maana Serikali iliweka ukomo wa kukopa ni robo ya tatu bila hivyo wengi wangeacha kazi.
Japo haisaidii bado watumishi wanapigwa kwenye salary advance plus wazee wa kuzuia card na password yako ili mwisho wa mwezi wakachukue kwenye ATM mkopo wao
 
Wakuu eleweni kitu kimoja, naona wengi wetu tunachangia kwa kujiamini afu tunachangia uongo.

Benki haitumii hizi hesabu zetu za madukani kwamba ukiambiwa riba ni 17% kwa mwaka maana yake kwa miaka mitano utachukua tu 17% × 5 upate 85%, hizi ni hesabu za form one simple interest[emoji2]

Kumaliza utata mtoa mada aseme alikopa benki gani, kwa riba gani na muda gani.
 
Tusitishane jamani interest rate kwa mwaka ni Kati ya 16% mpaka 18% kwa mwaka kwa mabank haya tunayoyafahamu. Ukizidisha hiyo Raye na let say miaka mitano ya kulipia bado haifiki hata 100%. Ukute mtoa Mada alitaka arudishe pesa ndani ya miaka kumi.
Dah mkopo wa muda mrefu nao kasheshe
 
Kuna baadha ya hizi micro finance mfano Finca wanatoa mikopo kwa riba ya mwezi 5% kwa mwaka inakua 60%. Sasa unakuta mleta mada kachukua mkopo huko kwa muda wa miaka miwili tu riba inakua 120% bado hawajakata bima na Administration fee lazima uchanganyikiwe tu.!
Hizi microfinance ni janga kwa taifa na sijui kwa nini serikali imekaa kimya. Yaani mkopo una vigarama vilejificha kibao. Yaani kukopa huku ni kujichimbia kaburi mwenyewe. Wana mikataba mirefu halafu ukifika wanakuambia sign harakaharaka. Nilienda Platnum kutaka kukopa 3M kwa miezi 4 hesabu zanataka nitudisje 4.7 sijui. Huu ni wizi kwa watanzania
 
Ila ndo 10M kwa 24M ? riba 100%+ huu ni wizi aisee
Sio wizi ila sisi sio waelewa wa masuala ya mikopo. Mfano wanakuambia riba ni 14 % Kwa mwaka, maana yake ni kwamba kama mkopo utakuwa wa miaka nane riba itakuwa 14% zidisha Kwa miaka 8 = 112%
Kama umechukua mkopo wa million 10 utarudisha zaidi ya million 22 Kwa hiyo miaka nane.
Ushauri wangu ni vyema tukope mikopo ya muda mfupi, napendekeza isizidi miaka 3.

Mfano wa pili kama angechukua hiyo hiyo million 10 Kwa miaka mitatu ingekuwa hivi;
14% zidisha Kwa miaka 3= 42%
Hapa angerudisha million 14 na laki kadhaa.
42÷100x1000000= 4,200,000/= hii ndio riba ukijumlisha na ile million 10 ndio unapata 14,200,000/=
 
Acha kabisa aisee!

Nikiwa nimepagawa na changamoto iliyokuwa inanikabili bila kujua la kufanya, nikakimbilia benki moja kuomba mkopo. Kufika pale nikamuambia afisa mikopo kuwa nahitaji m15, akaniambia m10 ni uftapata lakini si hizo ulizotaka. Nikaona kheri tu itaokoa kitu tena kwa kiasi kikubwa sana tu.
Wakati huo, simu inapigwa kila baada ya sekunde 20 kutoka huko kwenye chamgamoto iliyonifanya niende kukopa......nilipagawa sana. Wakati afisa mikopo ananieleza habari za makato n.k mi hata sikuwa nasikia chochote. Akili ilikuwa kwenye kupata pesa tu nikamalize tatizo. Siku kadhaa mbele nikafanikiwa na tatizo likaisha na akili ikarudi katika utulivu wa kawaida.

Siku zinavyoenda haraka, mwisho wa mwezi ukafika bwana! Aisee, ile naiangalia salary slip sikuamini nilichokiona......milioni 24 nahitajika kulipa. 24M!! Kwanza nilihisi baridi, harafu ganzi; baadae nikahisi uono wangu kama hauko sawa. Nikajiuliza imekuaje mbona sioni vizuri? Kwakuwa nilikuwa chumbani, nikasogea kwenye kioo kujiangalia. Dah, si ndo nakuta jicho moja la upande wa kushoto limejifunga, kope haitaki kupanda juu ('kukupila' watu wa pwani ya kusini wanasema). Nikajaribu kulifunua kwa mkono, wapi! Nikiliacha linajifunga tena. Hali iliendelea hivyo kama dakika 40 au saa moja hivi. Baadae sana ndo likarejea katika hali ya kawaida. Nilishapagwa, nilijua limeparalyse!

Mikopo!!!! Ukiweza kuachana nayo iache ndg'angu!
Hii ni chai hakuna riba ya bank unaweza chukua 10 ukalipa 24 m kama riba haipo mkuu...riba ni 13% kwa bank nyingi...hiyo milion 12 imezidi saana haiwezi zidi 5m kama riba..ambapo riba plus interest unaweza kulipa milion 17 hapo umedanganya umma

Ila kama ulichukua kwenye sacoss ni kweli saccos riba zao ni kwa mwezi..ila bank riba zao ni annualy
 
Back
Top Bottom