Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanamme hata akutongoze kwa miaka 10, ukimkubali tu na kuishi pamoja lazima migongano itakuwepo. Youn can't eliminate conflicts, but you can manage conflicts.
Kila jumatatu na alhamis huwa nafunga na kufanya maombi ya faragha kwa ajili ya ndoa yangu huu mwaka wa 4 sasa.
af sasa kakutana na NOBODY boy!He he he, mamaz boi na papaz gal mbaya sana
Sasa huyu ni bibiz gal, utajuuta kumfahamu.
Pole, now I understand clearly. Ulitakiwa kuonesha umekulia katika familia gani tangu mwanzo ili wachangiaji tukuelewe wewe ni mtu wa aina gani.
Kwanza nataka ujue hili, "The truth is, everyone is going to hurt you. You just got to find the ones worth suffering for."
Usidhani kuna mwanamme utampata akawa perfect 100%, unachotakiwa kujiuliza ni je, anakupa furaha? Anatimiza majukumu yake? Ankupenda kwa dhati? Ukishajijibu maswali hapo juu, utajua kama anakufaa ama lah.
At 30, ulitakiwa kuwa mwanamke mkomavu, ngangari na mwenye kutafuta suluhisho la matatizo yake kwa njia za kiutu uzima zaidi, Hili ulilofanya hapa, ni kama binti wa miaka 17. Haliendani na umri wako kabisa.
Wakati huo huo, baada ya kujua umelelewa na bibi, uko peka yako, nimekuelewa kwa nini umetumia njia hii. Watoto wanaolelewa na bibi zao wanakuwa na deko zisizo za kiuhalisia. Unaweza kuwa ulizoea kubembelezwa bembelezwa bila sababu za msingi. Ndio maana labda hata huyu mwanamme uliyenaye anaona kero kushinda na wewe sababu unataka kila saa ubembelezwe (love sucker?')
Kwanza unatakiwa kujiuliza, kwa nini mzazi mwenzio anashinda mtandaoni? Unamkera? Na kama ndio, ni mambo yapi yanamkera?
na watu wengine husema, watoto wanaozaliwa na kulelewa peke yao huwa selfish in term ya vitu na hisia, je na wewe ukoje katika hilo?
Emotional stability yako pia unatakiwa kuichunguza, are you emotionally stable? Sio kakitu kadogo tu unaruka kama umeona simba. Kweli alichokifanya mzazi mwenzio kinastahili kuachana.
Mie nakushauri kwanza ujichunguze mapungufu yako, halafu ndio uanza kumlaumu mzazi mwenzio. Nashawishika kuamini kuwa wewe ndio chanzo cha matatizo, bila hata ya wewe kujijua. na inaweza kuwa inachangia na makuzi yako.
You can do better than this. Hii dunia sio laini kihivyo, usipokuwa imara wewe mwenyewe kutetea unalolitaka hakuna atakayekuja kukutetea. Be strong for you kid and hubby, hili linajadilika. Kaa nyumbani, pika, msubiri mmoe jioni akirudi mkalishe chini muongee. Waweza jaribu kumuuliza kama na wewe unamkwaza, usidhani wewe ni malaika.
Na pia jaribu kuangalia mmeo kakulia mazingira yapi, kama ni mtu asiye emotional sana, ujue hapo kuna 'clash' Inabidi mjadialiane mtachukulianaje hizo tabia zenu za kuhisia.
Mengi ya kuandika hapa.
kwa muda uliofunga kwa mungu haufiki ata sekunde INGOJE AHADAI YA MUNGU NA UWE NA MSULI WA IMANI WEWE !....
you are very right conie.Natamani ningejua malezi ya mumewe ili kuweza kuwafanyia analysisi ya emotional stability.
Au mumewe angekuja hapa naye akatoa yake ya moyoni, tatizo huyu dada anadhani yeye yuko perfect na hamkwazi mumewe. Kutoshinda home ni dalili kubwa ya kukosa kitu fulani home.
Kingine hata njia zake za kutatua matatizo ni kuzira na kukimbia badala ya kukabiliana na kuliongelea tatizo. Imagine mtu hawezi hata kumface mmewe kumwambia anaondoka home? Anakuja kumuagia jf? Low self esteem ya hali ya juu sana.
Lakini huyu anahitaji kukalishwa na mtu na kuwa trained, aondolewe hayo mawazo ya kitoto kitoto yaliyomjaa na awekewe kichwani reality. Anatakiwa ajue ndoa sio ku du tu na kupelekana guest, kunakutafuta chakula na kutolelewana pia.
Anaishi maisha ya mtu wa miaka 17 at 30.
Asante ndugu, mengi uliyosema ni kweli tupu, naipenda sana ndoa yangu sikutaka ifike hapa nilipoondoka nyumbani wakati flani mwaka mzima nikiw kwa wifi yangu nilijaribu kujichunguza niligundua makosa yangu na hapo ndo nikajipa miaka 3 nirekebishe na kumuweka mwenzangu kwanza ila yeye sasa bado harudi nachelea kusema nimechoka maana utu wangu wa ndani nimeufungia miaka 3 sasa naishi kwa kujibana kuokoa ndoa yangu nikihesabu miaka 3 naona mingi sana na sidhani kama naweza ibana tena, Nikisema nimejaribu nimethubutu kweli.
Sijui kama nitaweza ongeza mingine 2 ngoja usiku wa leo ndo naweza fikiria maamuzi mengine maana hapa nimepata vitu vipya ambavyo sikuwa nimevifikiria kabla. Nashukuru sana kwa mawazo yenu yanaweza kubadili mawazo yangu ya kuondoka bali niendelee kuishi na baba mtoto na mtoto wangu pamoja.
Kwako baba mtoto,
Samahani nimekuja huku maana najua unashinda humu kuliko kushinda nyumbani, nimeamua kuvuja kwenye pakacha lako iwe nafuu kwako kulibeba, baki salama.
Nilikupenda sana mfano wa keki/chokoleti (napenda sana keki na chokoleti)
Lakini hukupendeka......., nimechoka hakika sijiwezi, kuishi tena mi na wewe
Ingawa nakupenda, lakini sitoweza.....
Ingawa rohoni nimekwisha, namwomba mola anisaidie, niweze kukusahau kabisa, nipate mwingine kushinda wewe.
Najua unausoma ujumbe huu muhusika ila leo ukirudi nyumbani hutanikuta, nitapotea kwenye taswira ya uso wako na maisha yako kabisa, hutaniona tena.
Naenda kuanza upya.
Aliyekuwa mkeo, mama mtoto wako na aliyekupenda daima,
Mkunde.
:disapointed::disapointed:
umenipa tabasamu usoni maana wakati nasoma wanafunzi wenzangu walikuwa wananitania sana that way, thanks much.Ha ha ha, najua mie kiazi.
Ngoja nimkuze huyu mkunde hadi awe mchicha feki.
Ha ha, nikupe siri kwa nini nimeamua kumpa ukweli huu? Kuna kitu amenigusa, ukitaka kujua just hola.
natafuta mke anayenipenda kwa mabaya yangu maana mazuri yangu kila raia hapa duniani anayataka!
jiulize wewe mwenyewe uko radhi kumpenda mtu kwa mapungufu yake??
Asante ndugu, mengi uliyosema ni kweli tupu, naipenda sana ndoa yangu sikutaka ifike hapa nilipoondoka nyumbani wakati flani mwaka mzima nikiw kwa wifi yangu nilijaribu kujichunguza niligundua makosa yangu na hapo ndo nikajipa miaka 3 nirekebishe na kumuweka mwenzangu kwanza ila yeye sasa bado harudi nachelea kusema nimechoka maana utu wangu wa ndani nimeufungia miaka 3 sasa naishi kwa kujibana kuokoa ndoa yangu nikihesabu miaka 3 naona mingi sana na sidhani kama naweza ibana tena, Nikisema nimejaribu nimethubutu kweli.
Sijui kama nitaweza ongeza mingine 2 ngoja usiku wa leo ndo naweza fikiria maamuzi mengine maana hapa nimepata vitu vipya ambavyo sikuwa nimevifikiria kabla. Nashukuru sana kwa mawazo yenu yanaweza kubadili mawazo yangu ya kuondoka bali niendelee kuishi na baba mtoto na mtoto wangu pamoja.
Ukiondoka nitakukata makofi ujue? Mie namaliza wino kukushauri hapa, unadhani unanilipa?
halafu kingine mamii!
SIO KWAMBA NDOA YAKO haina tatizo!
na wala sio kwamba tunavyosema humu zetu ziko poooooa!
HAPANA !NI NAMNA WEWE UNAVYOYACHUKULIA HAYA!
sawa!
hebu hata kama ni kuachana hebua achana nae ukiwa na akili za mwanamke wa miaka 30
We Mkunde Original KWA HIYO UNAMPANGO WA KUWA UNAKUJA KUIBA NAYE..?? Au unataka kuja kuwa nyumba ndogo yake siku za usoni..??? Maana mimi story yangu ilikuwa inakupa athari za kuachana kwa namna unayotaka kufanya wewe
kwangu ni kipimo cha mapenzi ya dhati kwake!