Mohammed wa 5
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,215
- 3,035
Leo March 20 Kuna tukio nimelikumbuka kipindi Niko o level kidato Cha nne.
Nilipewa hela kama laki 4 kwa ajiri ya kulipa Ada na michango mingine ya shule. Kipindi hicho Ada inalipwa shuleni unapewa risiti halafu muhasibu wa shule anapeleka benki..nilikuwa nasoma shule ya jeshi ni ya day na bweni. Nakumbuka ile hela sikupeleka shuleni nikawa naitumia tu kununulia vitu mbalimbali na kura Bata shuleni nikawa boss muda mfupi. Sijui Ile akili niliitoa wapi.
Baada ya miezi kupita shuleni nikawa nadaiwa Ada na nyumbani mzee anahitaji risiti nikawa namdanganya mzee muhasibu hayupo akirudi atanipa risiti zangu.
Na shuleni muhasibu namdanganya baba yupo course hapatikani kwenye simu nikimpata tu hela ya Ada nitaileta mzee sababu anajulikana muhasibu akanielewa, hakumpigia simu kosa ilo alilolifanya.
20/3/ 20...........
Baada kumpiga tarehe nyingi mzee siku moja mida ya asubuhi kama saa 5 nakuja kuitwa nahitajika ofisi ya head master nikajua ishu za kawaida tu. Parking ya shule na ofisi ya head master zinaangaliana ukitoka class parking unaiona kwa upande wa chini. Niliona gari ya mzee nikajua labda zimefanana mzee aje kufanya nini shuleni.
Baada ya kuingia ofisi ya head master nilishtuka nilitaka kuzimia namkuta headmaster, mzee, mhasibu, ticha wa nidhamu na second master wote wananiangalia kwa hasira.
Palepale ticha wa nidhamu akaniamuru nipige magoti. Nikajua nishaisha leo nakufa hapa.
Ikabidi nipige magoti nikingojea hukumu yangu.
Headmaster akaniuliza hela ya Ada iko wapi kama umeleta shuleni ulimkabidhi nani.
Nikajichanganya nikamjibu ile hela ya Ada nilipoteza nakumbuka nilichezea kichapo kutoka kwa mzee mpaka nikawa natoka damu mdomoni ikabidi teacher wa nidhamu ni mwanajeshi aje kunisaidia mzee asiendelee kunipiga ataniua Baada ya maongezi kidogo na kusemwa sana nikapeleka assembly Kama mtuhumiwa
Kengele ya dharula
Wanafunzi wote assembly baada ya matangazo mafupi nikiwa npo mbele pale wanafunzi wote wanashangaa hasa classmates zangu nimefanya Nini mdomo ushaanza kuvimba, mzee ametulia pembeni na gwanda zake. ananichora.
Headmaster baada kusalimia wanafunzi ikabidi aongee kuhusu Ile kengele ya ghafla iliyopigwa kuwa Mimi nikatajwa jina na kidato nimekula hela ya Ada laki 4 na kusema uongo. Wanafunzi wote wakawa wanashangaa huku wananiangalia.
Headmaster anaendelea hivyo sasa atapigwa viboko pamoja na suspension ya miez 3 atoruhusiwa kuingia darasana pamoja na adhabu.
Nilichezea viboko sio poa siku hiyo assembly huku wanafunzi wezangu wakishuhudia mpaka demu wangu wa shule alikuwa analia,niliambiwa na classmate wangu tunakaa kitaa kimoja home.
Nilikaa nyumbani miezi 2 mwezi mmoja nilienda kufanya adhabu shule ya kufukia mashimo yalitokana na kuchimba tofali na kuchimba visima vya maji. Baadhi ya classmates zangu walikuwa wanakuja kunisaidia adhabu
Nakumbuka baada ya msala ule nilikuwa maharufu Sana shuleni habari zilikuwa ni Mimi tu kila mwanafuzi vidato vya chini alikuwa ananishangaa tu.
Nyumbani niliishi kimateso Sana mzee alilipa Ada nyingine. Kwa Sharti moja nifaulu necta nikifeli nimrudishe hela zake na nihame nyumbani
Baada ya matokeo nilifaulu Japo kibishi.
Je, wewe unakumbuka uliwahi kufanya msala gani shuleni?