Siku ya Januari 20, 2025, Rais wa Marekani Donald Trump alisaini agizo la rais (executive order) lililosimamisha kwa muda wa siku 90 utoaji wa misaada nje ya Nchi, ikiwemo programu muhimu za afya kama Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI. "
President's Emergency Plan for AIDS Relief " (PEPFAR).
Kusitisha Huku Progran Hizo kutaathiti Dawa za Virusi vya UKIMWI (ARV), Dawa za kifua kikuu (TB), na Dawa za malaria na Dawa za Uzazi wa Mpango..
Ukiachana na Kuathiri Upatikanaji wa Dawa Taarifa ya USAID kuhusu Kupunguza kusitisha Misaada ya Viti hivyo Kumeanza Kuleta Effect kwa Baadhi ya NGOs Mashirika Mengi..
Yanayohusika na Utoaji wa Dawa za ARV,Kifua kukuu na Ukoma,Uzazi wa Mpango,na malaria yameanza Kuyumba na wote wameanza Kutoa Notice kwa wafanyakazi wao kusubiri na Kuangalia kama Marekani itarudisha Panga kwenye ala bhasi watarudi kazini...
Takribani Wafanyakazi wa Mashirika Tanzania 2900s Wanaenda Kupoteza Kazi kutokana Na upuuzi na Ego ya Trump..
Poleni Afya, Poleni Wafanyakazj wenzangu na Mostly Poleni wagonjwa ambao mnaenda Kuathiriki kwa Order hii Isiyo na Mashiko..
_____________________________________
Waafrika Tujitegemee:
Uhuru kenyata
View: https://youtu.be/wYpSNxTxXE0
Hakuna njia rahisi kwenye maisha, hasa yahusuyo taifa bila KUJITAMBUA.
Tutambue tunahitaji kula kwa urefu wa kamba yetu pia kama Taifa/nchi. Kujibebisha kwa Wamarekani hakutupi haki ya msingi ya wananchi wetu kuhudumiwa na wao/Wamarekani.
Tujiulize:
Tanzania si mtoto wala mjukuu wa Marekani. Tulipata uhuru kama nchi, inabidi tujisimamie na tuwasimamie wananchi kama nchi huru ili tuwe na nafasi ya Uhuru huo, Haki na Wajibu kama nchi.
Hii itatupa nafasi ya kusimama na kusema hili sawa au hili hapana tunapoletewa na hao wadau wa maendeleo. Wakati Mmarekani akituhudumia kwa mtindo husika, je tumeweza kujikwamua kwa kiasi gani? Je ndo uhalisia?
1: Tumewekeza kiasi gani kama Taifa kwenye elimu, afya, sayansi na teknolojia wakati pesa ya Wamarekani imechukua jukumu hilo.
2: Tumewekeza kiasi gani kwenye upatikanaji wa chakula kwa jamii yetu?
3: Tumewekeza kiasi gani kwenye tafiti ili kuweza kukuza uwezo wetu wa kuzalisha mahitaji ya taifa na watu wake dawa?
4: Ni kiasi gani cha pesa tunazopata ndani kinaenda kutatua matatizo ya msingi ya wananchi?
5: Ni kiasi gani cha pesa tunachozalisha kinatumika kufanya uzalishaji zaidi, multiple effect?
6: Ni kiasi gani cha pesa zetu kimepelekwa kutatua upunguzaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ya kuambukiza, matatizo ya lishe miongoni mwa jamii?
7: Au ni pesa kiasi gani inatumika kwa majukumu ya msingi dhidi ya yale ya ANASA, huku wananchi wanalelewa na JIRANI?
Akili ziturudie, tuwe na matumizi kadri tunavyopata. Nguo ya kuazima haiwezi kukuaitili.
8: Turudi kwenye MOTHER BOARD, tuchole NEW ROAD MAP, viongozi warudishwe kwenye DEFAULT SETTING. Tuulizane maswali magumu ili tuweze kutatua matatizo yetu na kutoka hapa na kila mmoja afurahie kuzaliwa au kuishi kwenye nchi yetu iliyojaliwa maliasaili kibao.
Tusionene haya, mficha uchi kifo humuumbua, tunaenda kuumbuka kwa kuwa taifa la kusifu na kuabudu.