Nilikuwa nacheki bongo movie kupitia Azam, ni fedheha sana

Nilikuwa nacheki bongo movie kupitia Azam, ni fedheha sana

Abu Ubaidah Commando

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
7,591
Reaction score
6,946
Nilikuwa nacheki bongo movie mchana wa leo kupitia azam 😁 dah ni fedheha sana, ni aibu mno, mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa ERTUGRUL na kwa sasa OSMAN, kwakweli waturuki wapo mbali sana, hii historia ya Ottoman inatufundisha mambo mengi sana ambayo huyakuti katika movie zetu za kibongo wala Nigerian movies. Wanawake wamejisitiri, wanaume wapo kiume haswaa, na pia kabla ya jambo wanamtanguliza sana Mwenyezi Mungu mbele, aise kwa hili niseme tu hawa jamaa walibarikiwa sana (OTTOMAN EMPIRE)✅

Bongo and all African movies bado sana, hata wakina shankari na amita bachan hatuwakaribii.


Hongereni sana waturuki, mpo vizuri.
 
Wabongo wengi walio kwenye hiyo tasnia ni watu wenye uwezo mdogo wa kiakili pia hawana exposure.

Ndio mana imebaki kuwa kichaka cha watafuta umaarufu hasa wanawake makahaba na vijana mario.

Ila ni tasnia nzuri sana kama ikipata watu sahihi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bongo muvi ni 🚮 tu kwa upande wangu! Ila hata hilo li tamthiliya lako la Ertugul sijui, nalo limekaa kijinga jinga tu.

Bora hata ile ya kipindi cha nyuma ya Sultan Suleiman Khan, kidogo haikuwa na maudhui mengi ya kujimwambafai kwingi kwa dini fulani hivi.
 
Shida ya bongo movie IPO Hapa *ukiwa mdada mnzuri unashepu kubwa bhas we tayar unafaa kuigiza na sio kipaji🤣,,hata upande wa men wale walamba lips ndo wanaopewa priority ktk kuigiza na sio kipaji🤣 * movie inaandaliwa ndani ya two weeks tayar IPO mtaan🤣wakat wezetu wanatumia hata 6 yrs kuiandaa na kuipromote. ** Movie inaitaji budget kubwa kuliko music lakin Hilo ni vise versa Kwa bongo movie yaan unakuta video ya diamond imetumia gharama kubwa kuliko movie iliyoigizwa na mkojani🤣 ** wengi bongo wanafanya maigizo kama KAZI Yao ya ziada na sio shughuli Yao kuu🙄
 
Bongo muvi ni 🚮 tu kwa upande wangu! Ila hata hilo li tamthiliya lako la Ertugul sijui, nalo limekaa kijinga jinga tu.

Bora hata ile ya kipindi cha nyuma ya Sultan Suleiman Khan, kidogo haikuwa na maudhui mengi ya kujimwambafai kwingi kwa dini fulani hivi.
Dini imeleta mushkeli!!!
 
Back
Top Bottom