Nilikuwa nacheki bongo movie kupitia Azam, ni fedheha sana

Nilikuwa nacheki bongo movie kupitia Azam, ni fedheha sana

Wabongo wengi walio kwenye hiyo tasnia ni watu wenye uwezo mdogo wa kiakili pia hawana exposure.

Ndio mana imebaki kuwa kichaka cha watafuta umaarufu hasa wanawake makahaba na vijana mario.

Ila ni tasnia nzuri sana kama ikipata watu sahihi.

#MaendeleoHayanaChama
Mimi hua najiuliza sitapi jibu, wakina cardo, wakin na don million wanatushindia wapi?. Bongo muvi ina nini?.
 
Filamu yangu ya mwisho ilikuwa ile ya kanumba sijui ndo inaitwaje ila jina lake mwisho inaishiwa na kijiji akiinza kama anahutubia ivi mwisho wakaanza kumpinga hapo kijijini na kumkimbiza...Jamaa na enzi za kina mussa banzi waliuza sana hata watu wa vibanda umiza walipiga pesa ila sasa ujinga mtupu.
 
Mkuu maudhui ya tamthilia yaliwataka kuwa vile na pia kule uislam sana upo juu ni uhalisia wao hata yale maigizo ni uhalisia wa tawala zao zamani so usiwatoe ufahamu wabongo sana kwenye hilo hata wao kuna movie nyingine wanavaa sana hivo visuruali, wakosoe kwa ubunifu wa story pia bongo bajeti yao si sawa na hao,


bongo tunafanya bora liende watu wapate pesa ya kula na uhakika kama atakuja muwekezaji akawa serious tutatoboa tu.

Kwahiyo unachoangalia wewe ni hela ya kula, ila humuogopi aliekukataza kufanya dhambi hiyo!! Sawa utapata hela ya kula lakinii mwisho wake sio mzuri, hii dunia isituhadae ndugu zanguni. Ni sitarehe ya muda mfupi, ivyo tusijisahau.
 
Mkuu maudhui ya tamthilia yaliwataka kuwa vile na pia kule uislam sana upo juu ni uhalisia wao hata yale maigizo ni uhalisia wa tawala zao zamani so usiwatoe ufahamu wabongo sana kwenye hilo hata wao kuna movie nyingine wanavaa sana hivo visuruali, wakosoe kwa ubunifu wa story pia bongo bajeti yao si sawa na hao, bongo tunafanya bora liende watu wapate pesa ya kula na uhakika kama atakuja muwekezaji akawa serious tutatoboa tu.

Kama wewe ni muislamu, unakosea kusema hayo.. kuna waislamu wenzio wanaigiza, wengine hawajistiri wala kuongea maneno yanayompendeza Mwenyezi Mungu, hivyo wape nasaha wa-nao tenda mabaya/siojistiri, maigizo mengi tunajionea wanawake wakiwa nusu uchi, nywele wazi, na hata maneno yenyewe hayafundishi wala kuwatoa watu katika ujinga. Uislamu haupo hivyo. Kuna watu wamesilimu kupitia Ertugrul/OSMAN kama ulikua hujui.
 
Bongo muvi ni 🚮 tu kwa upande wangu! Ila hata hilo li tamthiliya lako la Ertugul sijui, nalo limekaa kijinga jinga tu.

Bora hata ile ya kipindi cha nyuma ya Sultan Suleiman Khan, kidogo haikuwa na maudhui mengi ya kujimwambafai kwingi kwa dini fulani hivi.
Siwezi kupoteza muda wangu kufuatlia hayo ma dude hayo mambo ni ya kina dada mkuu
 
Haya mavitu wadada wa kazi wanayapenda sana sijui kwanini, mama watoto akitaka kuwaadhibu ni kuwapa cha kufanya saa ya hizi vitu ni adhabu kubwa sana kwao.
 
Back
Top Bottom