Nililogwa ili nife kwa kisukari na pressure

SEHEMU YA PILI:

Nilimuuliza kwanini utambike mizimu kwenye nyumba yangu? Je ulishawahi miona mimi mwenye nyumba natambika mizimu? Akanyamaza kimya. Nikamsamehe na maisha yakasonga. Ukapita mwezi tena nashtuka saa 8 usiku nasikia tena ile harufu ya udi/uvumba kumuuliza anasema tena anatambika mizimu ya kwao. Nikamgombeza na kulipokucha nikamwambia aondoke kwangu simtaki. Akazuga na hadi jioni hakuwa ameondoka. Mikampa wiki ya kujiandaa kisha ahame, akajua utani. Nikamkazia aondoke kwangu. Akaamza tuma watu waje niomba msamaha ili aendelee kuishi kwangu. Nikakataa na mwisho akaondoka.

Miezi miwili baada ya kuondoka kwangu, akanitumia sms kuwa nakuchukia sana na utaona na hiyo kazi yako unayoiringia. Mi nikapuuzia na sikuwa namfuatilia.

Kwa kawaida huwa nawahi kulala tokana na mizunguko ya kazi zangu. Siku moja kama kawaida nimelala saa 3 usiku, nakuja shtuka saa 5 usiku nikatoka sebuleni na nikachungulia dirishani. Nikaona pikipiki inakuja mitaa ya nyumbani kwangu. Ilipofika getini kwangu ikasimama kwa muda na kisha ikaondoka. Nilipuuzia na nikarudi kulala.

Kesho yake bosi wangu akanipigia simu nahitajika nimuandalie vifaa ili aende kigoma kwenye kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya magharibi ya nchi. Nikajiandaa then nikafungua geti na kwenda kazini. Pale getini niliona kumechimbwa na mafuta meusi kama ya Nyonyo yamemwagwa kwenye eneo la geti. Mi nikavuka na kuyaruka yale mafuta na kwenda kazini.

Niliporudi nyumbani jioni nikaanza kuona mawenge, nakuwa napoteza kumbukumbu, macho yakakosa nuru na nikawa naona giza. Mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio. Nikawa na hofu kuu ya mauti, wasiwasi na woga muda wote. Shida ilianzia japo na ilikuwa mwezi wa 8 mwaka 201......

Hali hiyo ilipelekea kuwa nakonda, sina amani, mtaani jamaa wakawa wanasema nina kufa muda wowote. Nikaenda Hospitali ya Wilaya wakapima wakukuta nina presha ya kupanda na sukari ya kushuka. Wakanipa transfer Hospitali ya Mpanda Mjini. Ikaonekana nina pressure ya 240/110. Sukari ilikuwa chini ya 5. Nikaanza matibabu ya pressure na kisukari na kwetu hakukuwa na mtu mwenye historia ya ugonjwa huo. Nikatoka hapo na kwenda nyumbani Moro then nikaambiwa niende kule SUA Main Campus kwa Dr. Omary yule specialist wa Moyo. Huko akaniambia nikachukue vipimo kule Mazimbu vya ECG, ECHO, CHOLESTRAL N.K. Majibu yakawa hakuna shida ila mimi mwili hauna nguvu, macho hayana nguvu na ninaona ukungu, moyo unanienda kwa kasi, nina hofu ya mauti, nikilala mawazo tu ya kufa nikiamka nakufa. Nikawa nimekonda ghafla, siwezi muangalia mtu usoni naona aibu na nina muogopa na nina hofu Marafiki wakanikimbia natangazwa mtaani jamaa muda wowote mauti inamkuta.

Itaendelea........
 
Uchawi haupo na hauta kuwepo
Nyinyi ndiyo wale waleeeeeee, kudanganya wenzenu uchawi haupo duniani ila mnafungua makanisa na kuroga kondoo wenu wasiwe na akili huku mkiwatumia kujinufaisha wenyewe. Kwenye Uislam hata Mohammed anatambua uchawi na Yesu pia anatambua uchawi ila wewe Mchungaji uchwara unasema HAKUNA uchawi?
 
Kigoma wameagiza wahanga kumi kutoka Rukwa kwenda kupambana na wachawi!! Nilichoka kusikia hili radioni!!
 
Endelea tunakusubiri.
 
Sehemu ya tatu........
Hali ile iliendelea hadi mwezi wa 10. Nikawa mtu wa hofu, wasiwasi, nahisi kifo muda wote, nikawa naogopa watu, nimekonda sina amani rafiki kazini wakaniambia nina stress na muda wowote nakufa. Hospitali wakanishauri nitafute digital machine ya kupima pressure niwe najipima pia nikanunua kale kakifaa cha kujipima sukari. Nikaenda tena Hospitali moja kule Mbeya na nyingine Arusha wakaniambia nina "Panic attach" kwani kuna kipindi nilikuwa nashtuka na Moyo unapiga kwa nguvu na kwa mshtuko mkubwa. Hii kitu ilikuwa iniletee stroke na kupalaryze.

Kuna ndugu yangu mmoja ni mjanja mjanja wa masuala ya kijadi kule Morogoro akazunguka kwa wataalamu wakamwambie mdogo wenu katupiwa jini la mauti. Akaniambia niende Moro ili walishughulikie. Nikagoma kwani namuamini Mungu.

Mzee wangu akaniita niende naye kule Machame, nikaenda na akamtuma Baba mdogo aende kwa mzee mmoja wa mila wanamuita "muonaji" kule kijijini Kyeeri akawaambia huyo mtoto ametupiwa "majini ya Mauti na magonjwa, lengo la aliyemtumia ni kwamba apalaryze na asiende kazini awe amelala kitandani na kisha afe" kipindi hiko cha miezi 2 sikuwa naenda kazini kwa kuogopa watu kunisema, sikuwa na uwezo wa kuona vizuri, nilikuwa na hofu kuu ya mauti pia miguu ilikuwa inaniwaka moto hatarii.
 
Nyinyi ndiyo wale waleeeeeee, kudanganya wenzenu uchawi haupo duniani ila mnafungua makanisa na kuroga kondoo wenu wasiwe na akili huku mkiwatumia kujinufaisha wenyewe. Kwenye Uislam hata Mohammed anatambua uchawi na Yesu pia anatambua uchawi ila wewe Mchungaji uchwara unasema HAKUNA uchawi?
Acha kupanic buraza, wapi nimesema mimi ni mchungaji na nikiwa mchungaji ndo uchawi utakuepo?
 
Back
Top Bottom