SEHEMU YA TANO:
Wakati maumivu na mateso yanaendelea na hata nilipokuwa naenda Hospitali pamoja na wao kunipa Dawa kwa ajili ya Ugonjwa wa sukari na pressure, sikuwahi kuzitumia hizo dawa kwani nafsi yangu ilikuwa inaniambia huo sio ugonjwa wa kibinadamu. Mama yangu alinieleza kuwa mwanangu huo sio ugonjwa wa kawaida ni Mapepo hayo. Muangalie Mungu.
Kipindi chote hiko na maumivu yote, kukataliwa na kusemwa vibaya, kukonda n.k hakuna Dr aliyenithibitishia kuwa nina either pressure au sukari. Nikaamua maamuzi ya kumtafuta Mungu.
Kulikuwa na kanisa moja la kilokole lililokuwa limejengwa kwa miti na juu limeezekwa kwa nyasi jirani na hapo kwangu. Huyo Mchungaji alikuwa ni yeye na mkewe na watoto tu na kimsingi nilikuwa namdharau na pamoja nilikulia kwenye familia ya wazee wa Kanisa ila nilikuwa napinga uwepo wa Mungu. Nikaona kwanini niteseke wakati nimekulia kwa Baba na Mama ambao ni wazee wa Kanisa. Nimekulia na kulelewa katika maadili ya Kikristo na nakumbuka Mwaka 1998 Bwana aliniambia na nilimuona waziwazi katika Maono ya usiku kuwa nitamtumikia. Nikasema, sifi nitaishi ili nitangaze matendo makuu ya Bwana. Nikachukua hatua na kwenda Kanisani kwa yule Mchungaji.
Hapo ndipo maisha yangu yalibadilika, nikaokoka na kumkabidhi Yesu Maisha yangu na tola mwezi huo wa kumi 201.... imebaki kuwa historia. Vile vifaa nikavitoa msaada hospitali moja huku nilipo sasa japo changamoto hiyo ilinifanya nikimbie kutoka kule na pia nilipoteza nyumba yangu ambayo nilikuja uiza kwa hasara, mashamba ekari 50 ambazo wasukuma waliofukuzwa kwenye maeneo ya hifadhi wakati wa Operation tokomeza ujangili walizivamia na viwanja 6 (sita) nilivyokuwa nimenunua niliviacha na kukimbia japo navyo nilikuja kuuza kwa hasara.
Sasa nina amani na kumtukuza Mungu japo nilipoteza vingi vya kimwili ila ninauzima na nimepata vingi vya Kiroho ikiwemo kumjua Mungu wa kweli yaani Yesu Kristo.
Asanteni wote na tumefikia Mwisho
View attachment 2633258