SEHEMU YA PILI:
Nilimuuliza kwanini utambike mizimu kwenye nyumba yangu? Je ulishawahi miona mimi mwenye nyumba natambika mizimu? Akanyamaza kimya. Nikamsamehe na maisha yakasonga. Ukapita mwezi tena nashtuka saa 8 usiku nasikia tena ile harufu ya udi/uvumba kumuuliza anasema tena anatambika mizimu ya kwao. Nikamgombeza na kulipokucha nikamwambia aondoke kwangu simtaki. Akazuga na hadi jioni hakuwa ameondoka. Mikampa wiki ya kujiandaa kisha ahame, akajua utani. Nikamkazia aondoke kwangu. Akaamza tuma watu waje niomba msamaha ili aendelee kuishi kwangu. Nikakataa na mwisho akaondoka.
Miezi miwili baada ya kuondoka kwangu, akanitumia sms kuwa nakuchukia sana na utaona na hiyo kazi yako unayoiringia. Mi nikapuuzia na sikuwa namfuatilia.
Kwa kawaida huwa nawahi kulala tokana na mizunguko ya kazi zangu. Siku moja kama kawaida nimelala saa 3 usiku, nakuja shtuka saa 5 usiku nikatoka sebuleni na nikachungulia dirishani. Nikaona pikipiki inakuja mitaa ya nyumbani kwangu. Ilipofika getini kwangu ikasimama kwa muda na kisha ikaondoka. Nilipuuzia na nikarudi kulala.
Kesho yake bosi wangu akanipigia simu nahitajika nimuandalie vifaa ili aende kigoma kwenye kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya magharibi ya nchi. Nikajiandaa then nikafungua geti na kwenda kazini. Pale getini niliona kumechimbwa na mafuta meusi kama ya Nyonyo yamemwagwa kwenye eneo la geti. Mi nikavuka na kuyaruka yale mafuta na kwenda kazini.
Niliporudi nyumbani jioni nikaanza kuona mawenge, nakuwa napoteza kumbukumbu, macho yakakosa nuru na nikawa naona giza. Mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio. Nikawa na hofu kuu ya mauti, wasiwasi na woga muda wote. Shida ilianzia japo na ilikuwa mwezi wa 8 mwaka 201......
Hali hiyo ilipelekea kuwa nakonda, sina amani, mtaani jamaa wakawa wanasema nina kufa muda wowote. Nikaenda Hospitali ya Wilaya wakapima wakukuta nina presha ya kupanda na sukari ya kushuka. Wakanipa transfer Hospitali ya Mpanda Mjini. Ikaonekana nina pressure ya 240/110. Sukari ilikuwa chini ya 5. Nikaanza matibabu ya pressure na kisukari na kwetu hakukuwa na mtu mwenye historia ya ugonjwa huo. Nikatoka hapo na kwenda nyumbani Moro then nikaambiwa niende kule SUA Main Campus kwa Dr. Omary yule specialist wa Moyo. Huko akaniambia nikachukue vipimo kule Mazimbu vya ECG, ECHO, CHOLESTRAL N.K. Majibu yakawa hakuna shida ila mimi mwili hauna nguvu, macho hayana nguvu na ninaona ukungu, moyo unanienda kwa kasi, nina hofu ya mauti, nikilala mawazo tu ya kufa nikiamka nakufa. Nikawa nimekonda ghafla, siwezi muangalia mtu usoni naona aibu na nina muogopa na nina hofu Marafiki wakanikimbia natangazwa mtaani jamaa muda wowote mauti inamkuta.
Itaendelea........