Nililogwa ili nife kwa kisukari na pressure

Mkuu leta vitu ili watu wajifunze mambo ya kujenga nyumba na kutafuta sijui kijana sijui mlinzi akakae mwisho wa siku anaona pale ni pake na kuleta tafrani na maumivu kwenye familia. Binadamu wengine wapuuzi sana. Na umshukuru sana mkeo maana jamaa alidhamilia upasahau kabisa na alikufanyia wewe alisahau kumfanyia mkeo. Mkeo ile nguvu ya kusema tuhamie kwetu ilikuwepo.
 
Sorry huo upuuzi wako ishia hapo hapo!
 
lazima ITAENDELEA kukutoa marinda, mtoto wa kiume umevaa shanga za dada yako unatuletea habari nusunusu, ITAENDELA ndio upuuzi gani
 
Mkuu

Pole sana!

Hiyo HALI YAKO ilinipata nikiwa udsm mwaka 2012 mwaka wa pili!

Kuna jamaa nikibishana nae mpira tu!akamchukua sana akasema nitaona aiseh nilianza kuona wenge,giza,ukungu kwenye macho,kuishiwa NGUVU,nywele kupoteza rangi yake,kukonda na kubaki mifupa tu,macho kutoa machozi ninaposoma!aiseh NIKIENDA HADI ccbrt nikaambiwa sina TATIZO!lakini pressure ilikua kubwa sana plus MAWAZO ya kifo!!

Nili sup course mbili ZL na CH aiseh nilipoona baada ya Kurudi NYUMBANI LIKIZO!HADI leo jamaa alikua ananipigia akijichekesha chekesha japo SIJUI kama ni YEYE au NANI!
Nahisi MAOMBI na sadaka vilisaidia kiasi chake AISEH!
M
 
SEHEMU YA TANO:

Wakati maumivu na mateso yanaendelea na hata nilipokuwa naenda Hospitali pamoja na wao kunipa Dawa kwa ajili ya Ugonjwa wa sukari na pressure, sikuwahi kuzitumia hizo dawa kwani nafsi yangu ilikuwa inaniambia huo sio ugonjwa wa kibinadamu. Mama yangu alinieleza kuwa mwanangu huo sio ugonjwa wa kawaida ni Mapepo hayo. Muangalie Mungu.

Kipindi chote hiko na maumivu yote, kukataliwa na kusemwa vibaya, kukonda n.k hakuna Dr aliyenithibitishia kuwa nina either pressure au sukari. Nikaamua maamuzi ya kumtafuta Mungu.

Kulikuwa na kanisa moja la kilokole lililokuwa limejengwa kwa miti na juu limeezekwa kwa nyasi jirani na hapo kwangu. Huyo Mchungaji alikuwa ni yeye na mkewe na watoto tu na kimsingi nilikuwa namdharau na pamoja nilikulia kwenye familia ya wazee wa Kanisa ila nilikuwa napinga uwepo wa Mungu. Nikaona kwanini niteseke wakati nimekulia kwa Baba na Mama ambao ni wazee wa Kanisa. Nimekulia na kulelewa katika maadili ya Kikristo na nakumbuka Mwaka 1998 Bwana aliniambia na nilimuona waziwazi katika Maono ya usiku kuwa nitamtumikia. Nikasema, sifi nitaishi ili nitangaze matendo makuu ya Bwana. Nikachukua hatua na kwenda Kanisani kwa yule Mchungaji.

Hapo ndipo maisha yangu yalibadilika, nikaokoka na kumkabidhi Yesu Maisha yangu na tola mwezi huo wa kumi 201.... imebaki kuwa historia. Vile vifaa nikavitoa msaada hospitali moja huku nilipo sasa japo changamoto hiyo ilinifanya nikimbie kutoka kule na pia nilipoteza nyumba yangu ambayo nilikuja uiza kwa hasara, mashamba ekari 50 ambazo wasukuma waliofukuzwa kwenye maeneo ya hifadhi wakati wa Operation tokomeza ujangili walizivamia na viwanja 6 (sita) nilivyokuwa nimenunua niliviacha na kukimbia japo navyo nilikuja kuuza kwa hasara.

Sasa nina amani na kumtukuza Mungu japo nilipoteza vingi vya kimwili ila ninauzima na nimepata vingi vya Kiroho ikiwemo kumjua Mungu wa kweli yaani Yesu Kristo.

Asanteni wote na tumefikia Mwisho
 
Hongera Kwa kufata njia sahihi'....ila hujatueleza jee kazi uliacha?na jee baada ya kutoka ulimuuliza chochote yule kijana ulie kua una mlea?na jee vipi kuhusu mke Bado mko wote au matatizo yaliwatenganisha!!
 
Kwanini uliamua kukimbia Mkuu WAKATI ushindi uliupata!!?

Kwanini ulipoteza nyumba kisa mapepo!!?

Ungekomaa tu Mkuu ili ushindi uupatie pale pale!
 
Kisukari ni ugonjwa unajulikana acha imani za kijinga
 
KINENGUNENGU!!!! mimi naona wewe ndio ulimloga mtu akapata KISUKARI,manake jina lako lenyewe limekaa kichawichawi!!
 
Ubarikiwe sana kwa ushuhuda huu mzuri.
 
Heri umemaliza uongo wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…