Nilimpiga Mwalimu akahama shule

Sijawahi kusoma shule ikawa haina kiranja mkuu wa shule! Chuo Kuna rais wa serikali ya wanafunzi.
Ni shule gani hapa Tanzania haina kiranja mkuu?
Naona kama bangi hivi.
Una miaka mingapi,itakuwa umemaliza shule juzi,nachoandika hapa kilifanyika.kitambo sana
 
Aliendekeza madawa sana
 
Kuna nyakati shule za msingi Arusha ziligeuka madojo na makanisa ya kilokole! Baada ya muda wa shule vijana wengi tulienda kujifunza Karate!

Asilimia kubwa ya sisi vijana tuliokulia Arusha 90s tumepitia yale madojo!
Kweli mkuu mimi nimezaliwa iliboru,sema kaloleni ilikuwa ndo chimbo langu,nako 2 nako walikuwa mabrother kwetu,sisi tulikuwa juniors nako,taekwondo na kick boxer nimejifunzia kaloleni,kipindi kile lazima uwe fit tu kulingana na mazingira ya ubabe yaliyokuwepo,nimepiga mazoezi gym moja na bou nako pamoja na fido vato,wote tulifundishwa na teacher mmoja
 
Enzi za picnic miaka hiyo nakumbuka,tulikua tunakutania hapo kaloleni then tunaenda usa river kuna club nadhani ni mbele ya ngarasero ama kama sikosei ni mji mwema,kitambo sana,ile club iko pemben ya mji,kule kulikua na vurugu nyingi sometimes wanawake wanabakwa....

Pia safari zingine tulikua tunaenda duluti ziwani,kuna mwaka nilipigwa bapa za kushanta nikazikatia picnic mazima....

Nishapiga sana hizi kick boxer mpaka bhas..
Nilijikuta naangukia uvutaji wa ndumu uliokisiri..
Kuna baadhi ya shule ukipeleka kijana akimaliza vyema bila kuaribika ni jambo la kumshukuru Mungu.
 
Daah mkuu itakuwa tushakutana sana kwenye hiyo club usa River pia duluti tushakutana sana sema kitambo,kuna watu huku jamii wanaona ni chai,hawajui maisha ya chugah yapoje wanachukulia poa poa tu
 
Arusha mji wq kipekee
 
Inaendeleeea...
Baada ya mabala kukimbia,nikabaki nimemshika Ebenezer damu zikiwa zinamtoka kwa wingi sana,tukambeba mpaka kwenye coster za moshi ili tumuwaishe hospital,damu.zilimtoka kwa wingi sana,viti vilichafuka kwa damu,ukiniangalia mimi damu imenitapakia kwenye sharti niliokuwa nimevaa yani ilikuwa kama nimetoka kuchinja mbuzi..

Tulimfosi dereva aendeshe gari kwa speed,baadhi ya walevi tuliokuwa tumepanda nao gari wakaanza kuleta vuruga,waligoma kutoa nauli dereva akaona apeleke gari kituo kikuu cha polisi.

Dereva akasimamisha gari kituo cha polisi,tukaamuriwa wote tutoke nnje,baada ya hapo tuliingizwa mahabusu kwa kosa la kukata kutoa nauli na kutukana ndani ya gari..

Ebenezer akawaishwa hospital na defender la police,sisi wengine tukaingizwa mahabusu kwa mbata na mateke,tulikuwa kama 23 daah ndo mara ya kwanza naingia mahabusu kwenye maisha yangu,tena nikiwa mwanafunzi tuu,

Taarifa mzazi akapewa kwa simu,kuwa nipo police aje kuniwekea dhamana,baba akagoma katu katu kuja kunitolea dhamana,nikasota kwa siku 4 hakuna cha mama wala baba,na ukizingatia baba yangu ni mtu maarufu sana chugah alinikataa katu katu.

MUNGU sio athumani bana,uncle alikuja matembezi arusha akiwa na mke wake mzungu kutoka Canada,alipofika Airport kisongo alipokelewa na kaka yangu,ndio akahoji mbona fulani simuoni hapa,maana ndo nilikuwa nampokea sana kuliko wengine wote,kaka akamwambia nipo mahabusu Central,uncle alipanic sana kwanini hamjamuwekea mdhamana???

Uncle akaja akaniwekea mdhamana,ndo nikatolewa
 
Uncle akaokoa jahaz,sjui mdingi atasemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…