Nilimpiga Mwalimu akahama shule

Nilimpiga Mwalimu akahama shule

Sijawahi kusoma shule ikawa haina kiranja mkuu wa shule! Chuo Kuna rais wa serikali ya wanafunzi.
Ni shule gani hapa Tanzania haina kiranja mkuu?
Naona kama bangi hivi.
Una miaka mingapi,itakuwa umemaliza shule juzi,nachoandika hapa kilifanyika.kitambo sana
 
Kuna msela kwao kulikuwaga na pesa sana,nakumbuka tulikuwa tukiwa likizo alikuwa anapenda kwenda arusha,na baadae alianzisha kuandaa matamasha na mziki picnic,tulikuwa tunakutana huko wanafunz wa shule mbalimbali wanafunz walikuwa wanakunywa pombe sana siku hiyo na mziki ulikuwa unapigwa mpaka saa mbili usiku hz mambo zilikuwa zinafanyikaga jumamosi,naona haya mambo aliyatoa huko Arusha.

Ila nasikitika huyo jamaa kwasasa amekuwa teja yaani ukikutana nae hadi huruma kawa chizi nasikia alikuwa akienda Arusha anajihusisha na matumizi ya unga na unga mwingine alikuwa anakuja nao kwao
Aliendekeza madawa sana
 
Kuna nyakati shule za msingi Arusha ziligeuka madojo na makanisa ya kilokole! Baada ya muda wa shule vijana wengi tulienda kujifunza Karate!

Asilimia kubwa ya sisi vijana tuliokulia Arusha 90s tumepitia yale madojo!
Kweli mkuu mimi nimezaliwa iliboru,sema kaloleni ilikuwa ndo chimbo langu,nako 2 nako walikuwa mabrother kwetu,sisi tulikuwa juniors nako,taekwondo na kick boxer nimejifunzia kaloleni,kipindi kile lazima uwe fit tu kulingana na mazingira ya ubabe yaliyokuwepo,nimepiga mazoezi gym moja na bou nako pamoja na fido vato,wote tulifundishwa na teacher mmoja
 
Enzi za picnic miaka hiyo nakumbuka,tulikua tunakutania hapo kaloleni then tunaenda usa river kuna club nadhani ni mbele ya ngarasero ama kama sikosei ni mji mwema,kitambo sana,ile club iko pemben ya mji,kule kulikua na vurugu nyingi sometimes wanawake wanabakwa....

Pia safari zingine tulikua tunaenda duluti ziwani,kuna mwaka nilipigwa bapa za kushanta nikazikatia picnic mazima....

Nishapiga sana hizi kick boxer mpaka bhas..
Nilijikuta naangukia uvutaji wa ndumu uliokisiri..
Kuna baadhi ya shule ukipeleka kijana akimaliza vyema bila kuaribika ni jambo la kumshukuru Mungu.
 
Daah mkuu itakuwa tushakutana sana kwenye hiyo club usa River pia duluti tushakutana sana sema kitambo,kuna watu huku jamii wanaona ni chai,hawajui maisha ya chugah yapoje wanachukulia poa poa tu
 
Hii kweli nililifanya, nikiwa o level kipindi hicho wanafunzi wa shule hiyo, iliyopo Arusha chini waliogopeka kwa uhuni, uvutaji bangi, wizi, hiyo shule ina O level na A level.

Kipindi nikiwa form 3, nilikuwa na vuta bangi mfano hakuna, nikisha vuta bangi naingia gheto napiga msuli kinoma, darasani zilikuwa zinachoma matokeo sikosi top ten hata siku moja, lakini mvutaji bangi mzuri.

Nilianza mafunzo ya taekwondo nikiwa na miaka 12, kwa teacher Abuu Kaloleni Arusha, nakumbuka tulipewa mafunzo na nako 2 nako pamoja na junior nako, kipindi hicho Arusha iliogopeka kwa uhuni.

Mtaani waliniita Damme, maana nilikuwa napiga mateke, hakuna mjinga yeyote alinitania wala kunidharau heshima ilikuwa debe sio kwa wahuni mpaka raia wote.

Kipindi nikiwa form 3, nilikuwa na maisha ya kihuni sana, nakumbuka siku hiyo niliyomtandika mwalimu ilikuwa hivi.

Kuna teacher wa English alikuwa na tabia ya kuendelea kufundisha hata kama kengele imelia bado ataendelea kufundisha kwa dakika 20 mbele, jambo hilo liliwafanya wanafunzi wamchukie, walimpa jina la mkaba penati.

Teacher mwenyewe ndio alikuwa ametoka chuo kwa hiyo alikuwa na munkari na kazi yake, kwa sisi wanafunzi tuliona uzushi tu

Ilikuwa ijumaa kipindi cha mwisho kilikuwa english, na kilikuwa kipindi cha mkaba penati. Muda wa kipindi uliisha, teacher akaendelea kufundisha, nilikuwa na ahadi na demu wangu tukabanduane na kuvuta bangi, demu alinipa ahadi nikitoka shule nika mpitie kwao maana palikuwa sio mbali na kwetu.

Nilivumilia kwa dakika 10, teacher hana hata dalili za kutoka darasani, kwanza ndio anafuta ubao aanze kuandika notice, akisha maliza aweke na homework, nikicheki muda saa zinaenda sana halafu ninaugwadu kinoma.

Nikasema usinitanie, nikachukua begi langu, darasa kimya teacher yupo ubaoni anaandika notice, hapo kengele ilishalia kitambo kama dakika kumi na tano zilizopita nyuma.

Nikampita teacher,
Teacher: Unaenda wapi,
Mimi: Naenda home,
Teacher: Unioni bado nipo darasani
Mimi: Muda umeshaisha
Teacher: Rudi kakae
Mimi: Muda umeshaisha usinizingue

Teacher alikuja akanikaba shingoni, nikimcheki tunalingana mrefu sema yeye kanipita miaka kadhaa, halafu katoka chuo bado mgeni, akanitandika kofi moja la haja mpaka masikio yakalia nziiiiiii.

Nikalivumilia, ile anajiandaa kunipiga lingine nikamsogelea nikamtandika kichwa kimoja cha maana, teacher akaanguka chini kama mzigo, wanafunzi wenzangu oooooh.

Teacher kaamka kwa wenge, ananifuata kwa hasira kapanic huku midamu inamtoka mdomoni na puani, nikamtandika stop kick ya kifua teacher akanguka kwenye meza ilikuwa mbele ya darasa.

Akaamka akachukua mbao ya kuchorea mstari kwenye ubao ananifuata kwa hasira kama kanifumania na demu wake. Nika mpiga jumping ushiro teacher chini kazirai, wanafunzi wenzangu si wakaanza kupiga kelele ameua! ameua! ameua!

Nikatoka nduki kuelekea nnje ya shule, ile nafika kwenye geti lakutokea nnje ya shule limefungwa nikaduwaa miguu yote nguvu hakuna tena, walinzi wakaja wakanikamata.

Itaendelea...

Muendelezo soma Nilimpiga mwalimu akahama shule
Arusha mji wq kipekee
 
Inaeeendeleeeea!!!
Kweli club kulifana sana,walijaa wahuni wa kila pembe za arusha,baadhi niliyokuwa nawajua chajop,John mabala,Ebenezer,Ringo akiwa na ndugu yake mojaa,Chingori mshikaji mmoja wa ungalimited aliyekuwa fit sana kwenye kick boxer,watu walimuogopa sana pia alikuwa amefuatana na dada ake ambaye pia alikuwa fit sana kwenye ngumi..na wengine wengi wahuni,vibaka,majambazi..

Tulikunywa pombe club huku tukicheza mziki mpaka mida ya saa 11 jioni club ikafungwa,kimbembe ikawa mda wa kurudi town sasa,maana kuna umbali mpaka ufike kwenye hiace za kwenda Town ni kilomita za kushanta zisizopungua 10.kwa kukadiria..

Tulipokuwa tunatembea kuelekea kupanda gari za Town,John mabala(arusha sec) alikuwa na bifu na ebenezer(arusha sec),toka kitambo walikuwaga marafiki sana,walipozinguana wakatengeneza visasi kwa kila mmoja wao..

Basi tukiwa tunatembea huku tumelewa,tupo wengi barabarani John mabala akamfuata Ebenezer, akamwambia kama vipi leo tumalize ugomvi huku huku,mpaka tujue mbabe nani,aisee huyo John mabalaa alikuwa sio powah jamaa alikuwa fiti sana kwenye mateke,na ukicheki mshikaji wangu ni Ebenezer pia yeye alikuwa fiti sema.sio sana..

Huyo mabalaa akampiga Ebenezer round kick ya shingo,Ebenezer akaweweseka mpaka nilipokuwa nimesimama mimi,nikamzuia kwa mkono,nikamwambia kausha kausha mabalaa,mabalaa akanifuata akaniambia wewe ndo nilikuwa nakutafuta siku zote sasa nimelianzisha ili ujae,umewazingua madogo sana shuleni wakivuta kaya unawang'ang'anya,unajifanya kaka mkuu wa shule leo hii nataka kupigana na wewe,tupiganeeee aliongea kwa nguvu tena kapandisha mzuka..

Ile na tahamaki jamaa karusha right hook,nikakwepa ile nakaa sawa akanipiga wash ya usoni, nikajisemea moyoni leo hii nimekutana na jet Lee.

Kusema la kweli sikujua kama ingetokea ugomvi siku hiyo,kumbe watu walikuwa na bifu nami toka kitambo sana,kitendo cha kuwa kaka mkuu kimenitengenezea bifu kwa watu,sio wavuta bangi tu mpaka wauzaji ambao wanaogopeka mtaani.

John mabalaa akachomoa kisu,ile anataka kunichoma kisu msela angu Ebenezer akanikingia kisu akachomwa cha mbavu,akamchoma tena visu vya paja kama mara tatu,John mabalaa alikimbia baada ya kuona damu inamtoka sana Ebenezer..
Itaendeleeea nikipata mda wa kuandika tena
Inaendeleeea...
Baada ya mabala kukimbia,nikabaki nimemshika Ebenezer damu zikiwa zinamtoka kwa wingi sana,tukambeba mpaka kwenye coster za moshi ili tumuwaishe hospital,damu.zilimtoka kwa wingi sana,viti vilichafuka kwa damu,ukiniangalia mimi damu imenitapakia kwenye sharti niliokuwa nimevaa yani ilikuwa kama nimetoka kuchinja mbuzi..

Tulimfosi dereva aendeshe gari kwa speed,baadhi ya walevi tuliokuwa tumepanda nao gari wakaanza kuleta vuruga,waligoma kutoa nauli dereva akaona apeleke gari kituo kikuu cha polisi.

Dereva akasimamisha gari kituo cha polisi,tukaamuriwa wote tutoke nnje,baada ya hapo tuliingizwa mahabusu kwa kosa la kukata kutoa nauli na kutukana ndani ya gari..

Ebenezer akawaishwa hospital na defender la police,sisi wengine tukaingizwa mahabusu kwa mbata na mateke,tulikuwa kama 23 daah ndo mara ya kwanza naingia mahabusu kwenye maisha yangu,tena nikiwa mwanafunzi tuu,

Taarifa mzazi akapewa kwa simu,kuwa nipo police aje kuniwekea dhamana,baba akagoma katu katu kuja kunitolea dhamana,nikasota kwa siku 4 hakuna cha mama wala baba,na ukizingatia baba yangu ni mtu maarufu sana chugah alinikataa katu katu.

MUNGU sio athumani bana,uncle alikuja matembezi arusha akiwa na mke wake mzungu kutoka Canada,alipofika Airport kisongo alipokelewa na kaka yangu,ndio akahoji mbona fulani simuoni hapa,maana ndo nilikuwa nampokea sana kuliko wengine wote,kaka akamwambia nipo mahabusu Central,uncle alipanic sana kwanini hamjamuwekea mdhamana???

Uncle akaja akaniwekea mdhamana,ndo nikatolewa
 
Uncle akaokoa jahaz,sjui mdingi atasemaje
 
Back
Top Bottom