Nilinunua soundbar ya Sony watts 400, 5.1 channels hata sijaielewa!

Nilinunua soundbar ya Sony watts 400, 5.1 channels hata sijaielewa!

Ili afanyaje sasa?
Kuna kitu kinaitwa High Fidelity music system (wenyewe wanaziita Hi-Fi kama sijakosea) hii ndio yenyewe kwenye suala zima la mziki incase of pure music quality na vionjo vyake kusikika katika kila angle.

Soundbar
Home theater

Hizo sio specific kwaajili ya muziki madam nafkiri tunazipa mzigo tu nadhan ni maded for the theater/ movies

Wataalamu watanisahihisha kwenye hili
 
Mimi nina Sony Dav 650 ni home theater 1000Watt sijui hata ninachokisikia kama ni kelele au muziki,kwa ufupi nimeshaichoka.

Kama uwezo upo tafuta JBL wanazo soundbar nzuri iwe hiyo hiyo 5.1 unaweza ukaifurahia kidogo.
Kaka mim nina LG home theater watt 1000 naomna iko powa ina sound moja tam. Unaeza ichek madukan ukaiskia pia
 
Chukua seapiano sp 910 au 912....!
Seapiano siku hizi zimechakachuliwa sana hazina Ile quality kama ya zile za analog

Ninayo hii mpaka Leo inagonga mziki quality sana na base imetulia kinoma
Screenshot_20240208-200007.jpg
 
Nadhani kuhusu high fidelity radio ni the same kama ya jamaa cd tatu ambayo imekufa kiufupi jamaa anataka kuenda na ulimwengu unaenda
Zipo za kisasa mkuu kama hii

Sema bei mkasi sana ila mzee watu wanaojielewa(music enthusiast) wanakaa humu

Kama tu hii ukifanikiwa kuwa nayo aisee ulimwengu wote unauhisi umeukamata hata nje uwezi thubutu kutoka kabisa
images.jpg
 
Mimi nilinunuafa slow cooker sijawahi hata itumia miaka saba sasa.
 
Kabla ya kununua sound system yoyote kwanza unatakiwa kujua hitaji lako ni nini.
Kwa mfano; hitaji lako ni mziki mkubwa( sauti kubwa),mziki mzuri,mziki mtupu,mziki + muvi nk.
Kama hitaji lako ni mziki mzuri basi unatakiwa uangalie kitu kinachoitwa frequence range na frequence response ya spika zako.
Frequence range na frequence response huonyesha uwezo spika zako kucheza/kuplay frequence za sauti ambazo zitakuwa zinatoka kwenye spika zako.
Kwa kawaida wanadamu husikia sauti kuanzia frequence response ya 20 Hz mbaka 20000Hz.
Kwahiyo spika yoyote ambayo inaweza kucheza sauti katika frequence hizo itakufanya uweze kusikia kila kitu kilichopo kwenye saitu hiyo.
Baada kujua frequence range sasa utatakiwa kujua frequence range ya spika yakp ambayo yenyewe itaonyesha uwezo wa spika yako kuwa flat.

Kama hitaji lako ni sauti kubwa unatakiwa isome kitu kinachoitwa SPL( Sound pressure level) hii huonyesha kiwango cha sauti ambao spika zako zinaweza kuzalisha.Watu wengi huwa wanaangalia watt za spika kitu ambacho siyo sahii.
Radio kuwa na watt kubwa haina maana kuwa saiti yake ndo itakiwa kubwa.

Kama matumizi yako yatakuwa kusikiliza nyimbo tu,chukua system ambayo ina spika mbili tu na subwoofer moja.Mana nyimbo zote tunazosikila kuwa stereo kwa maana hutengenezwa kwa mfumo wa masikio yetu ambayo ni mawili.Katika mfumo huu wa stereo( 2.0) au ( 2.1) spika mbili hucheza frequence za kati na za juu huku subwoofer ikicheza frequnce za chini za sauti( Base)

Kama hitaji lako ni kutumia radio system yako kwenye muvi hapa ndo uchue sound bar au home theater ambazo mara nyingi huwa na subwoofer moja na spika kuanzia 5 na kuendelea.
Lengo la spika kuwa nyingi huwa sio sauti kuwa kubwa ila kufanya kila spika kwenye muvi icheze kitu kimoja.
Kwa mfano kuna spika hucheza maongezi,kuna spika hucheza effect nk.

Nje ya hayo yote pia kwenye vifaa vya muziki kuna kitu huitwa breaking time.Breaking time ni muda ambao spika mpya huotaji ili kuweza kuanza kufanya kazi kwa ufasaha mana inapotoka dukani huwa haiwezi kufanya kazi kwa ufasaha.
Mara nyingi huwa ni masaa 24 mbaka 36.
So ukiweza baada ya kununua radio yako soma kwanza breaking time yake alafu ifungulie kwa sauti ya juu kwa muda wote huo alafu baada ya hapo ndo uanze kutumia radio yako utakavyo.
 
Back
Top Bottom