Kabla ya kununua sound system yoyote kwanza unatakiwa kujua hitaji lako ni nini.
Kwa mfano; hitaji lako ni mziki mkubwa( sauti kubwa),mziki mzuri,mziki mtupu,mziki + muvi nk.
Kama hitaji lako ni mziki mzuri basi unatakiwa uangalie kitu kinachoitwa frequence range na frequence response ya spika zako.
Frequence range na frequence response huonyesha uwezo spika zako kucheza/kuplay frequence za sauti ambazo zitakuwa zinatoka kwenye spika zako.
Kwa kawaida wanadamu husikia sauti kuanzia frequence response ya 20 Hz mbaka 20000Hz.
Kwahiyo spika yoyote ambayo inaweza kucheza sauti katika frequence hizo itakufanya uweze kusikia kila kitu kilichopo kwenye saitu hiyo.
Baada kujua frequence range sasa utatakiwa kujua frequence range ya spika yakp ambayo yenyewe itaonyesha uwezo wa spika yako kuwa flat.
Kama hitaji lako ni sauti kubwa unatakiwa isome kitu kinachoitwa SPL( Sound pressure level) hii huonyesha kiwango cha sauti ambao spika zako zinaweza kuzalisha.Watu wengi huwa wanaangalia watt za spika kitu ambacho siyo sahii.
Radio kuwa na watt kubwa haina maana kuwa saiti yake ndo itakiwa kubwa.
Kama matumizi yako yatakuwa kusikiliza nyimbo tu,chukua system ambayo ina spika mbili tu na subwoofer moja.Mana nyimbo zote tunazosikila kuwa stereo kwa maana hutengenezwa kwa mfumo wa masikio yetu ambayo ni mawili.Katika mfumo huu wa stereo( 2.0) au ( 2.1) spika mbili hucheza frequence za kati na za juu huku subwoofer ikicheza frequnce za chini za sauti( Base)
Kama hitaji lako ni kutumia radio system yako kwenye muvi hapa ndo uchue sound bar au home theater ambazo mara nyingi huwa na subwoofer moja na spika kuanzia 5 na kuendelea.
Lengo la spika kuwa nyingi huwa sio sauti kuwa kubwa ila kufanya kila spika kwenye muvi icheze kitu kimoja.
Kwa mfano kuna spika hucheza maongezi,kuna spika hucheza effect nk.
Nje ya hayo yote pia kwenye vifaa vya muziki kuna kitu huitwa breaking time.Breaking time ni muda ambao spika mpya huotaji ili kuweza kuanza kufanya kazi kwa ufasaha mana inapotoka dukani huwa haiwezi kufanya kazi kwa ufasaha.
Mara nyingi huwa ni masaa 24 mbaka 36.
So ukiweza baada ya kununua radio yako soma kwanza breaking time yake alafu ifungulie kwa sauti ya juu kwa muda wote huo alafu baada ya hapo ndo uanze kutumia radio yako utakavyo.