Vita dhidiyaujinga
JF-Expert Member
- May 15, 2026
- 279
- 385
Utamu wa safari za usiku kwa kutumia mabasi
"Nilisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kwa basi. Tuliondoka stendi majira ya saa 10 jioni. Bahati nzuri nilikaa siti moja na kijana aliyekuwa mwenye upole na mwenye sura ya kuvutia.
Baada ya usiku kuingia, nilisinzia. Akiwa anaona nimelala, aliniegemeza kwa upole ili nipate nafasi nzuri ya kupumzika. Tulipofika sehemu ya mapumziko, aliniambia nibaki kwenye siti huku yeye akienda kuninunulia chai. Aliporudi aliniletea chai, na kila tuliposimama njiani alikuwa akijitahidi kuhakikisha niko sawa.
Tulipowasili Bukoba, tulishuka pamoja. Kabla ya kuondoka alinipa shilingi 30,000 pamoja na namba yake ya simu. Kwa kweli, ilikuwa safari ya kipekee ambayo sitaweza kuisahau kirahisi.
Wewe, umewahi kukutana na mtu usiyemfahamu kwenye safari akakuonyesha wema wa namna hii? Tuambie uzoefu wako kwenye maoni hapa Chini.
Umetumia lugha rahisi lakini nahisi una ajenda ya kimalaya.Malaya wengi hupenda vya Bure. Pia shetani amekuwezesha kuandika huu uzi.Kwaufupi huu Uzi kama umeuandika kwa interest binafsi achana na hiyo ajenda mwamini YESU uokoke leo.ZcUtamu wa safari za usiku kwa kutumia mabasi