Niliporudi kutoka Uswisi baada ya kukaa kule wiki mbili niliona Dar ni chafu sana

Lema amezidi.

Anashambulia mpaka ugali. Ugali!? [emoji15]

Kwa hili sitamsamehe kwa kweli.

Anataka Wasukuma tule nini? Burger ama? [emoji51][emoji51]

View attachment 2543587
Anachokifanya Lema ni ulimbukeni wa kuishi nje ya nchi. Anaonekana hakuwahi kuvuka boda kwenda ng'ambo before.

Tangu arudi kutoka Canada anaona Bongo Kama tupo motoni/jehanamu. Kila kitu kwake ni uchafu na umasikini.
 
Nenda Moshi,the city is amazingly clean,sijaweza kufananisha na miji mingine ya Tanzania,nimepita kama mara mbili,Moshi ni pasafi sana pale mjini...
 
Ni kweli kabisa!.. Kama hujawahi kutoka nje ya mipaka ya nchi hii huwezi kuona tofauti, huwezi kuona uchafu wala harufu na mazingira machafu. Huwezi kuona harakati za maisha katika miji yetu yenye kelele kama kero. Watu kuitana kwa miruzi kama wachunga ngombe ni jambo la kawaida.... Ukweli unabaki kuwa, sehemu yoyote katika Dunia hii inaweza kupangwa ikawa sehemu bora ya kuishi kama ilivyo Ulaya. Tatizo kubwa ni watu na malezi yao, mitazamo ya kijima, kurithishwa ujinga na ubishi unaoambatana na kiburi cha kuto- kutii sheria hasa kwa watanzania.

Huhitaji kwenda mbali sana kujifunza jinsi wengine wanavyothamini kuishi maisha bora, vuka mpaka ingia Rwanda utashangazwa na jinsi watu walivyojipanga na kufuata sheria katika mazingira yale yale kama ya hapa kwetu. Usafi unazingatiwa kupita maelezo, nyumba zinajengwa kwa viwango na barabara hali kadharika. Watanzania karibu wote ni kina "Hambiliki" tabia zetu ni chafu kuliko uchafu wenyewe na hatuoni taabu kukaa kwenye uchafu. Kukojoa popote na kujikuna panapo ni kawaida kwa kisingizio cha kubanwa.

Ukitengeneza mazingira ya kuvutia kwako, unavutia watu kuja kubarizi na kupiga "Selfie" stori hazikauki hapo. Kila mtu ni mjuzi asiyependa kukosolewa. Ukienda kinyume na utamaduni wa hovyo ambao ndio unaosifika kuwa nyendo za kimjini mjini, basi utaambiwa una roho mbaya kuliko Rucifer, sio mtu wa watu au sio mtanzania!. Nchi hii tulidai uhuru tu wa kujitawala, baada ya kuupata uhuru hatuna mpango na kujenga au kuboresha chochote, hata tukijaribu ni kwa kulipua maana hapa Duniani tunapita tu..... Duu!!.
 
FACT, ukitoka JNIA hadi unafika buguruni...then ubungo kichwa kinaanza kuuma, uchafu, vumbi, kelele...disorganisation ya hali ya juu. Then unakaa unajiuliza, kwani nilizaliwa wapi, nilikulia wapi...mbona niliishi. Home is best regardless.
 
Hiyo hali ndiyo anayopitia Godbless Lema kwa sasa.
 
Men! Siyo siri Bongo ni kuchafu! Harufu mbaya manoise kibao, majungu na kufuatilia mambo yasiyowahusu.

Men! siku moja nimeenda bush kumuona babu, kukawa namsiba kwa jirani. Tumeenda kwenye msiba tukakuta wanachimba kaburi.
Naona watu wananyang'anyana tools za kuchimbia, nikadhani wamelipwa kuchimba kumbe ni kazi ya kijamii.

Kumbe wameninote, jioni baada ya kuzika nikawekewa kikao kwamba nimedharau wazee sikuchimba kaburi, na hata kuzika maana hata kwenye mazishi bado watu walikuwa wananyang'anyana tools kuzika.

Wakanilipisha gallon 10 za pombe na kilo 10 za sukari, nikaleta gallon 20 za pombe na sukari kilo 20, bado wakawaka tena eti nimewadharau.
 
Nawaza ungekaa 1/2 years sijui ingekuwaje.
 
Mtoa mada umeongea Kitu sahihi kabisa, kama mtu hajatoka bongo kwenda hizo nchi inaweza kuwa ngumu kukuelewa, exposure ni kitu cha muhimu sana, acha tu uchafu hata magari unaona yote kama yamechakaa.
 
Hizo wiki mbili tu ungekaa miaka miwili si ungewaona wazazi wako nyani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…