Niliporudi kutoka Uswisi baada ya kukaa kule wiki mbili niliona Dar ni chafu sana

Hali ya vyoo vingi haifai kwa matumizi ya kibinadamu.

Sijui tunakwama wapi?!

Ni kukosa exposure kweli? Au ?

Hata kwenye ofisi za Umma vyoo si vya kuridhisha.

Vichafu vingine vimepasukapasuka yaani ilimradi tu!
 
Vyoo havina Maji ya ku flush automatically,

Eti ufanye kumwaga kwa kopo au sado ukishajisaidia,

Watu wote wanashika hiyo sado kwa mkono!

Ukishajisaidia maji safi ya kunawa mikono Na sabuni hakuna!

Na watu wako wana amani tu wala Hawa raise any concern!
 
Bro hakika nami ilinitokea hii hali. Nilihudhuria seminar nchi fulani ulimwengu wa kwanza huko ya siku kumi. Nilivyorudi bongo sijui nilikuwa najisikiaje, it was like nimerudi sehemu ambayo haina mipangilio sahihi ya kimaisha na jinsi watu wanavyofanya mambo yao kwa wakati in a very perfect way. Baada ya muda nikazoea mazingira yetu yaleyale ya ufanyaji kaziπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Wacha bongo iwe bongo tu, huku wanasiasa wanachezea sana maisha ya wananchi na wameridhikaπŸ™Œ
 
Msim
Lema amezidi.

Anashambulia mpaka ugali. Ugali!? [emoji15]

Kwa hili sitamsamehe kwa kweli.

Anataka Wasukuma tule nini? Burger ama? [emoji51][emoji51][emoji706][emoji706][emoji706]

View attachment 2543587
Mkuu ungewahi kuishi nje ya Tanzania especially Ulaya au America ya Kaskazini hata kwa mwezi mmoja tu, naimani ungemuelewa Lema, usijari bado akili yake ipo ki nje nje, baada ya muda atazoea mazingira ya nyumbani na hutasikia hayo maneno tena toka kinywani mwake.
 
Hali ya vyoo vingi haifai kwa matumizi ya kibinadamu.

Sijui tunakwama wapi?!

Ni kukosa exposure kweli? Au ?

Hata kwenye ofisi za Umma vyoo si vya kuridhisha.

Vichafu vingine vimepasukapasuka yaani ilimradi tu!
Mkuu nakuunga mkono hali ya vyoo kwenye ofisi zetu zinatisha. Hivi hawa ma-HRO wanalijua hili, au kuna vyoo vya wakubwa na wenzangu na mimi! Utakuta kwenye parking za magari ya watumishi wa ofisi hiyo kuna magari mazuri sana yenye bei mbaya hadi ma-v8. Jamani vijana hawana ajira waajirini wasafishe hivyo vyoo.
 
Kamanda kuna siku nilishuka hapo airport, nakwenda mjini ndio niliona utitiri huo wa watu...

Mbaya zaidi hawakuonekana kama ni watafuta vibarua!
Itakuwa ulipita ile mida raia wametoka kwenye vibarua kule viwandani.
 
Lema amezidi.

Anashambulia mpaka ugali. Ugali!? [emoji15]

Kwa hili sitamsamehe kwa kweli.

Anataka Wasukuma tule nini? Burger ama? [emoji51][emoji51][emoji706][emoji706][emoji706]

View attachment 2543587
Uswiss ugali mbona ndio chakula chetu unaitwa polenta inabidi useme Uswiss ulienda kwenye kabila gani Yako makabila 4 na tuna maraisi 7 hatutaki shida na ma dictators na hatutaki uchafu kila mtu anaheshimu haki ya mwenzake na kila mtu anabunduki nyumbani hataki mchezo na ujinga na wizi wizi wa mali za uma
 
Masikini akipata matako hulia mbwata

Hapa nimetoka kula ugali dagaa
 
Lema amezidi.

Anashambulia mpaka ugali. Ugali!? [emoji15]

Kwa hili sitamsamehe kwa kweli.

Anataka Wasukuma tule nini? Burger ama? [emoji51][emoji51][emoji706][emoji706][emoji706]

View attachment 2543587
Ugali siyo chakula cha maskini. Ugali ni chakula cha Waafrika wengi. Mimi siwezi kupitisha hata siku mbili bila kula ugali, ingawaje nina uwezo wa kula vyakula vingi vya Kitanzania. Kila watu wana chakula chakula cha asilia, na Waafrika wengi ni ugali unaotokana na nafaka mbalimbali. Mhaya chakula anachokipenda na anakila bila kuchoka ni ndizi laini, Mchagga ndizi mshale, watu wa pwani na Morogoro wanapenda wali na ugali wa Mhogo, zamani watu wa Mara walipenda ugali wa ulezi siku hizi ugali wa Mahindi, Mjaluo humuondoi kwa Ugali wa mtama, kusini mwa Afrika ukianzia Nchumbiji, Malawi, Zambia mpaka Afrika kusini ni ugali. Kwa hiyo kudai chakula cha jadi cha Waafrika wengi ni chakula cha maskini unaqukosea uafrika wako. Mimi hata wakati nilikaa Marekani nilikuwa nakula ugali na bamia au mrenda kuliko chakula kingine chochote.
 
Huo ndio ukweli ugali ni chakula cha mifugo
Wewe utakuwa Mhaya, maana ninyi ndugu zetu kwa majivuno hamuwezekana. Utaitaje chakula kinacholiwa na zaidi ya 50% ya Waafrka chakula cha mifugo. Mimi ninachojuwa mifugo hula chakula chochote inayopewa. Tena, naomba kukumbusha kuwa nguruwe wanapenda ndizi kukliko chakula chochote duniani. Na mhaya anapenda ndizi kuliko chakula chochote duniani...yaliyobaki naomba Wahaya wajazie!
 
Itakuwa ulipita ile mida raia wametoka kwenye vibarua kule viwandani.
Ndege ililand saa mbili hivi asubuhi, pilikapilika za uhamiaji na kadhia zingine inanifanya niwe nje ya uwanja ka saa tatu hivi.

Huu ni muda wa kuwa kazini... na bado nikaona huo utitiri... Hapana shaka ni tatizo kubwa la ajira.
 
Lema angekuwepo humu ningem-tag aje asome hizi nondo. Ametukosea sana Waafrika 😁😁😁
 
Hata sijui ni kwa nini umenikwoti mimi mkuu maana ulichokisema hakihusiani kabisa na malalamiko yangu kwa Lema 😳
 
Siku moja nikibahatika kuishi nje pengine nitamwelewa huyu kamanda 😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…