Nilisafiri kwa pikipiki Dar mpaka Tabora

Dah hongera mkuu ,hii kitu naiogopea magari makubwa njiani namna yanavyokupita ,unaweza jikuta mtaroni na huwa hawathamini pikipiki ,

Vp hii changamoto ulikabiliana nayo vp ,maana ujanja wangu pikipiki mwisho mjini,
Kama nia yako ni kufanya adventure huna haja ya kukimbizana na magari makubwa japo kiukweli ukiwa na boxer na ikiwa imekolea mwendo vizuri unaweza ukatembea umbali mrefu bila kupitwa na magari makubwa.

Binafsi mimi huwa nacheza na side mirror tu muda wote, haiwezi kupita dakika sijaangalia nyuma kuna nini, kama kuna gari kubwa litakuwa nyuma yangu likinikaribia sihangaiki kukimbizana nalo huwa nabana pembeni tu lipite then naendelea na safari yangu.
 
Nenda Upanga mtaa wa Ally Khan maeneo karibu na Goete Institute unapoenda kuikuta Ally Hassan Mwinyi kuna mafundi pikipiki. Ukienda Muulize fundi Elisha.

Kinondoni Biafra kuna mafundi pikipiki kubwa uliza fundi Panya.
 
Mfugaji wa jamii ya kimasai mkazi wa kijiji cha Melela wilayani Mvomero mkoani Morogoro Lomario Matajani (54), amefariki dunia baada ya kuvamiwa na tembo wakiwa kwenye pikipiki na mwenzake . Radio One Stereo on Twitter
 
Uzuri mwingine wa boxer haina mitetemo so haichoshi kivile ukienda nayo umbali mrefu.
Next time usitembee usiku bora uweke malengo ya sehemu ya kulala, lala utapokua umefika at 6 PM.

Hongera sana mtoa mada.
Kwa nini asitembee uck wakati barabara ya itigi tabora haina magari

Stay home, stay safe
Corona kills
 
Umeanza vizuri , ila sasa ulipo malizia ndio nimebaki hoi
 
Dah hongera mkuu ,hii kitu naiogopea magari makubwa njiani namna yanavyokupita ,unaweza jikuta mtaroni na huwa hawathamini pikipiki ,

Vp hii changamoto ulikabiliana nayo vp ,maana ujanja wangu pikipiki mwisho mjini,
Basi huwezi amini , watu wenye magari makubwa ndio wastaarabu sana barabani ukilinganisha na hawa wengine hasa wa private car, na ukiwa barabarani na piki piki usikubali kuwa sambamba na mwenye gari kubwa au lori , hiyo ni kwa utafiti wangu.
 
Kuna jamaa hua anatoka Dar anaenda Malawi na Boxer BM 150 kila siku saa tisa lazima apite hapa kijijini kwetu Soliwaya.
 
Kabla ya kubisha ni bora ungejua Dar to Dom ni kilomita ngapi?(457) mie nimetumia wastani wa karibu masaa 7 haya niambie shida ipo wapi hapo?
Upo sahihi, mi naendeshaga rafu road km150 masaa mawili nanusu mpaka matatu, ukifanya calculation ni mule mule, anayebisha sio dereva wa pikipiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…