Nilishangaa Waziri Mbarawa kutumia muda mwingi kuelezea mradi ambao watanzania hawautaki

Kuna TAZARA, kwa nini isitumike?
Hata hivyo, hakukua na uhitaji wa SGR kwa haraka kiasi hicho kwa kuwa kuna reli ya kati na hata matumizi yake bado yapo chini sana.
Umasikini wa fikra unaweza kuhusika hapa.
 
Nakumbuka ilikuwa inafanya sana na hata Kuna kipindi walitangaza idadi ya metric tonne za mizigo walizosafirisha na ikionekana iliongezeka Kwa karibu 200%
Ilikuwa, sasa haifanyi? Mahitaji ni kiasi gani na kinachofanyika ni asilimia ngapi?
 
Ukweli usemwe hizi akili za kutaka kufanya Jambo kubwa wakati dogo bado Ni kipuuzi.......robo tatu ya barabara za Lindi na Mtwara zinazounganisha wilaya zake hazina lami...

Robo tatu au tuseme asilimia 98 ya wakazi wa Lindi na Mtwara hawana maji salama mpk leo wanamkamua chura mtoni ....hivi nyie vingozi mnajua kweli mahitaji was wananchi....

Halafu wewe unasimama kwa kubana pua eti mikoa nn....halafu kwny kampeni unakuja Tena kuomba kura .....



Halafu wewe utakuwa umekulia IKULU TU...
 
Ilikuwa, sasa haifanyi? Mahitaji ni kiasi gani na kinachofanyika ni asilimia ngapi?
Kama haifanyi kazi Hilo litakuwa tatizo la watawala ila wajue tu SGR ni ishu ambayo CCM wasipokuwa makini watakosa kura 2025 kama wakileta mchezo watajuta
 
Kuna TAZARA, kwa nini isitumike?
Hata hivyo, hakukua na uhitaji wa SGR kwa haraka kiasi hicho kwa kuwa kuna reli ya kati na hata matumizi yake bado yapo chini sana.
Umasikini wa fikra unaweza kuhusika hapa.
SGR inaweza kuwa Masaa 6 hadi 8 Mwanza to Dar kwasasa safari ya Dar Mwanza kwa reli siku tatu watu wanafika wamevimba miguu direct to hospital!

SGR sio yetu ni ya watoto wetu mkuu wataishi kishujaa na Magu watoto wetu watamjengea mnara kama shujaa! Si vizuri sie tuishi kama mashetani na watoto wetu waishi hivyo hivyo. Wazee walitembea umbali mrefu kufuata shule wakiwa peku sie tukasoma karibu tukipelekwa skuli na school bus!!

SGR itawezesha mtu anaeishi Dodoma kufanya kazi Dar au Singida. Wa Mwanza wataweza kufanya kazi Dodoma na kurudi home kulala! Dagaa mbichi za Mwanza zitaliwa Dodoma na barabara zinazotumaliza pesa zitadumu na kila itakapopita SGR pataamka na kutajirika!
 
Kama haifanyi kazi Hilo litakuwa tatizo la watawala ila wajue tu SGR ni ishu ambayo CCM wasipokuwa makini watakosa kura 2025 kama wakileta mchezo watajuta
Ni kweli laweza kuwa tatizo 2025.
Hata hivyo, wapiga kura wengi hawajui maana au umuhimu wa kura yao, hufuata mkumbo kama nyumbu.
 
Sawa kabisa. Lakini siyo kwa haraka hivyo iharibu mpango mingine ya maendeleo.
 
Ni kweli laweza kuwa tatizo 2025.
Hata hivyo, wapiga kura wengi hawajui maana au umuhimu wa kura yao, hufuata mkumbo kama nyumbu.
Inategemea unaishi wapi, ila nikueleze tu kwasasa Dola ndiyo inaisaidia CCM kushinda siku wananchi wakichoka itakuwa balaa wananchi wanajitambua sana uelewa wao umekuwa mkubwa haswa miaka ya karibuni
 
Una maana gani unaposema hauwagusi watanzania wengi? Kwani reli ya kati au mabasi yanawagusa watanzania wengi? Mbona wengine wanaruka na ndege tu?
Umefikiria kibinafsi sana. Ukianza kufikiria kama umefungiwa kwenye box, hakuna kitu kitafanyika. SGR ni muhimu mno tuache ujuaji kwenye mambo tusiyoyajua
 
Sema ni wewe haujaufurahia!! Watanzania walio wengi tunaufurahia sana mradi wa SGR. Mabeberu ndio hawaupendi! Kama kuna kitu Rais Samia anatukuna watanzania ni kuendeleza miradi aliyoianza Magufuli. Akifanya hivyo tunajikuta tunamsamehe bure hata mapungufu mengine tunayoyaona kwake!
 
Inategemea unaishi wapi, ila nikueleze tu kwasasa Dola ndiyo inaisaidia CCM kushinda siku wananchi wakichoka itakuwa balaa wananchi wanajitambua sana uelewa wao umekuwa mkubwa haswa miaka ya karibuni
mkuu watu wanaojielewa wako JF wengine wako bize na mambo yao!
 
Unajisemea mwenyewe mkuu, halafu unawaunganisha waTanzania wengi wawe ni kupitia kwa mawazo yako.
Haya ni maajabu makubwa.
Kama huelewi maana ya reli hiyo, ungejaribu kuchukua muda kidogo ukajielimisha juu yake kwanza badala ya kuleta hapa jambo ambalo huna ufahamu juu yake kabisa.

Sipingi mawazo yako, lakini usifanye mawazo yako ndiyo ya waTanzania walio wengi kama ulivyofanya hapa.
 
Tatizo ni umasikini wetu,bajeti ndogo na mapato ya serikali madogo.

Barabara ulizozitaja ni muhimu kiuchumi,ni barabara ambazo zingejegwa vizuri zingeweza kuinua hali ya uchumi za maeneo husika.
SGR pia ni muhimu kwa sababu:
1.Itapunguza uharibifu wa barabara.
2.Itapunguza foleni barabarani.
3.Itapunguza ajali zinazosababishwa na malori.
4.Bidhaa zitakazotoka Dar watu wa kanda ya ziwa watanunua kwa bei nafuu na bidhaa kutoka kanda ya ziwa watu wa Dar,Moro nk watanunua kwa bei nafuu mfano dagaa au ng'ombe kutoka Mwanza au Shinyanga akisafirishwa na SGR bei yake itakuwa nafuu kuliko yule atakayesafirishwa na Lori.Nazi zitakazotoka Pwani na kusafirishwa na SGR watu wa Mwanza watazinunua kwa bei nafuu kuliko zile zitakazosafirishwa na Lori.
5.Tutaliteka soko la kutumia bandari yetu kwa nchi za DRC,Burundi na Rwanda.

Kinachotakiwa viongozi wa serikali na wataalam wabuni vyanzo vipya vya mapato ili SGR na barabara za vijijini zijengwe.Vyanzo vya mapato vipo vingi kuna madini hata kuchimbwa hayajachimbwa,chuma cha liganga kipo ila tunaagiza chuma kutoka nje,ardhi ya Tanzania ni kubwa kuliko Indonesia na Malaysia lakini nchi hizo zinaongoza kuuza mafuta ya mawese Duniani.Tuna ardhi kubwa kuliko Ukraine lakini ngano tunaagiza nje. Tuna vitu vingi sana vya kutuingizia mapato ambayo yangeweza kuleta fedha za kujenga hizo barabara lakini tumelala usingizi wa pono.
 
mkuu watu wanaojielewa wako JF wengine wako bize na mambo yao!
Natembea sana Vijijini Hali siyo kama unavyozani kadri maisha yanavyokuwa magumu na utandawazi unavyoongezeka ndivyo mabalidiko yapo huko usiichukulie rahisi kihivyo
 
Kwa hiyo mkuu unataka mradi wa sgr usimame?. Fedha nyingi ilishaenda kwenye sgr. Mtu mmoja alianzisha miradi mikubwa ambayo kwa uchumi wetu hauhimili. Bwawa la umeme na sgr ni miradi haikutakiwa kufanywa muda mmoja.
 
Kwanza ni hivi maisha ya mtanzania kwa sehemu kubwa tunaumia sana kwa gharama za usafirishaji mfano unatoa semi yenye nondo moja kutoka dar mpaka karagwe na wakati mzigo huo ungeweza kubebwa kweye train kwa mabehewa ya kutosha na mzigo ukashushwa Bandari kavi ya Isaka unapunguza sana gharama ya usafurishaji na kugusa sehemu kubwa ya awananchi

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
mkuu hujui SGR yetu ni wazo likitoka Kenya waliposhindwa kuimaliza SGR yao kwa ufisadi uliotukuka wa mawaziri wawili. Iliishia Naivasha na kushindwa kutimiza lengo la kuunganisha bandari ya Mombasa na nchi jirani kwa usafiri wa uhakika na wa haraka!!
mf unakopa pesa benki unaanzisha jengo uweke maduka kabla hujamaliza mwanao anaiba na kutokomea South unabaki kukabwa koo na benki na jengo halina duka hata moja!

SGR yetu ikiisha Dar Mwanza to Kigoma Kenya watakuwa wakikuona wanasonya! Mkuu huu ni mradi wa akili kubwa ya mbele not for us! Bandari ya Mombasa itadorora kuliko unavyofikiria.

Kumbuka SGR is not for the benefits of Tanzanian ADULTS!

SGR ikiisha yote Mwanza na Kigoma watoto wa Kibongo watakuwa na sifa na kutetema Africa nzima na watasema Wazee wa kibongo wako smart sana upstairs!! watatuenzi!

Hebu nenda kasome kuhusu Kenya, Wana uchumi mkubwa kuliko sisi na SGR yao sio ndefu kuliko yetu, deni wameshindwa kulipa, imebidi wakope IMF kulipa deni la Wachina
Yaani unakabwa hadi unakopa huku iliukalipe kule
 
Inategemea unaishi wapi, ila nikueleze tu kwasasa Dola ndiyo inaisaidia CCM kushinda siku wananchi wakichoka itakuwa balaa wananchi wanajitambua sana uelewa wao umekuwa mkubwa haswa miaka ya karibuni
Uelewa bado, ni sehemu chache sana zinazoweza kuwa uwezekano sawa wa ushindi kati ya chama tawala na upinzani.
Mikoa chini ya kumi kwa Tanzania Bara na Zanzibar ni yote.
Kwa kutaja bila mpangilio maalum ni Zanzibar, Kilimanjaro, Dare salaam, Mbeya, Kigoma, Kagera, Arusha, Mwanza na Mara.
Bado kazi kubwa inahitajika kuamsha fikra za wananchi kuhusu demokrasia.
 
Kile kitendo cha kung'ang'ania SGR badala ya kuilekeza nchi jirani nilimshangaa sana yule jamaa. Nilijiuliza anatumia kanuni gani za uchumi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…