Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Majaji wangapi wameikimbia unaposema kila jaji? Jaji wa kwanza mlimkataa, mkaletewa huyu wa Sasa, huyu wa Sasa kapanda Cheo hivyo majukumu yameongezeka, naye nafsi yake imemsuta ameona Kwa majukumu aliyonayo Sasa atachelewesha kesi, Bora aachane nayo! Au mlikuwa mnataka jaji aendelee na kesi na awe anapiga kalenda kila siku kesi iende miaka 2? Haya si ndiyo tumekuwa tunayapinga kila siku, full exaggeration
Kama jaji akikataliwa anajitoa, yule hakimu wa kesi ya Sugu angejitoa. Kwani hata sasa hiyo kesi inaendeshwa kwa kasi mpaka useme awe anapiga kalenda? Kuna majukumu yapi makubwa anaenda kuyafanyia kazi, maana mahakama ni sehemu inayofanya kazi itakavyo, kinyume kabisa na matakwa ya umma. Hakuna sehemu kuna malimbikizo ya kesi kama huko mahakamani, na sababu za ucheleweshaji huo ni za kipuuzi kabisa.Mahakama yetu ni moja ya taasisi za mfano kabisa za utendaji kazi wa kigoigoi na chini ya weledi. Huu ni ukweli ambao sina shaka nao.