Darlin
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 4,796
- 10,646
Hapa ndipo vijana wengi tunapokwama.
Unajua fika wewe ni dini tofauti na mpenzi wako. Unajua fika ukifosi kuna sehem pande zote mbili kwa wazazi na ndugu mtatengwa. Tena hata mkifosi mkaoana kuna uwezekano watoto wakakosa direction na kujua wafate mafundisho ya dini gani maana wazazi mpo dini tofauti. Mmoja anasali msikitini mwngne kanisani. Wapo mtakaosema ikitokea tumezaa mtoto akikua ataamua afate dini ipi! Jamani mafunzo mazuri ya dini siku zote huanzia utotoni, hapo ndipo mtoto anapopata good narration to see the right and wrong.
Hali hii itazidi kuwatafuna kadri vizazi vyenu vitakavyoendelea na hakutakua na amani ndani. Trust me hakutakua na amani. Najua wapo watakaonipinga na kusema mapenzi hayaangalii dini. Ni kweli mapenzi hayaangalii dini, lakini kuishi na mtu kama mke na mume dini lazima ipewe kipaumbele chake. Tena ni kigezo muhimu sana hiko wala tusidanganyane.
Tusitake kuishi kizungu wakati bado tamaduni zetu hazijafika huko. Na sidhani kama tutafika huko maana kila dini ina mafundisho yake na tunarithishana vizazi na vizazi. Kuepuka usumbufu wowote ule na mpasuko ktk familia ni bora uwe na mahusiano na mtu wa dini yako. Itakuweka huru sana.
Ifike hatua tusiishi kwa kuendeshwa na hisia bali akili. I REST MY CASE.
Wewe ni muislam au mkristo maana ulizaliwa ukawakuta wazazi wako wana dini hiyo ndio maana ukawa na dini hiyo.
Hivyo sioni ubaya mtu wa mtu mzima alie na miaka 18 kubadilisha dini kwa hiari yake mwenyewe kisa mapenzi.