Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Ulivopakazania hapo pakusema Allah sio Mungu sasa,
Mi mnyakyusa yesu namwita Kyala.......!!! napo utakataa utasema huyo Yesu na kyala ni watu wawili tofauti.


Yani wakristo na waislamu imefika point nawaonaga wapuuzi tu,.....wana haribu image ya Mungu, wameharibu na kuvuruga ovyo maandiko ya Mungu kwenye vitabu vyake, mfano wew mleta mada hapa......umejawa chuki uliolishwa na wachungaji zako....
Atakuja muislamu nae atashusha chuki juu ya ukristo aliolishwa na mashekhe wake na maustadh.

Kwa kifupi kuna wakati nawaona nyie wote mafala tu.

Mmejitoa kabisa katika ibada na misingi sahihi ya Mungu.

Utafiti uliofanyika mwaka 2013 unaonesha utofauti wa dini na mafundisho yake unachangia 30% ya chuki baina ya binadamu na binadamu duniani.

Ndo zinafata tofauti kama "Rangi za ngozi, Mali, Ukabila, etc
Hajasema Allah sio Mungu bali Allah sio Yehovah.
 
Hapa ndipo vijana wengi tunapokwama.

Unajua fika wewe ni dini tofauti na mpenzi wako. Unajua fika ukifosi kuna sehem pande zote mbili kwa wazazi na ndugu mtatengwa. Tena hata mkifosi mkaoana kuna uwezekano watoto wakakosa direction na kujua wafate mafundisho ya dini gani maana wazazi mpo dini tofauti. Mmoja anasali msikitini mwngne kanisani. Wapo mtakaosema ikitokea tumezaa mtoto akikua ataamua afate dini ipi! Jamani mafunzo mazuri ya dini siku zote huanzia utotoni, hapo ndipo mtoto anapopata good narration to see the right and wrong.

Hali hii itazidi kuwatafuna kadri vizazi vyenu vitakavyoendelea na hakutakua na amani ndani. Trust me hakutakua na amani. Najua wapo watakaonipinga na kusema mapenzi hayaangalii dini. Ni kweli mapenzi hayaangalii dini, lakini kuishi na mtu kama mke na mume dini lazima ipewe kipaumbele chake. Tena ni kigezo muhimu sana hiko wala tusidanganyane.

Tusitake kuishi kizungu wakati bado tamaduni zetu hazijafika huko. Na sidhani kama tutafika huko maana kila dini ina mafundisho yake na tunarithishana vizazi na vizazi. Kuepuka usumbufu wowote ule na mpasuko ktk familia ni bora uwe na mahusiano na mtu wa dini yako. Itakuweka huru sana.

Ifike hatua tusiishi kwa kuendeshwa na hisia bali akili. I REST MY CASE.
MI dini kwangu sio kipaumbele watoto wenyewe walikua watachagua wenyewe .
 
Ibrahimu hakuwa na dini.

Alimwamini Mungu tu.

Dini zilikuja baadae sana.

Kwani uislamu si umeletwa na Muhammed? Sasa Ibrahim alikuja kuishi baadae?
Unawezaje kumuamini Mungu bila yeye kukupa muongozo ? Alikuwa anamuamini vipi Mungu ?

Siyo tu Ibrahimu bali mpaka nabii Nuhu ambaye alikuwa kabla yake alikuwa Muislamu. Anasema Allah mtukufu :

71. Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.

72. Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu. (Yunus : 71-72)

Akasema tena kuhusu Ibrahiim ;

130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.

131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.

132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. (al-Baqarah : 130-132)

Kwa ufupi hakuna nabii wala mtume ambaye hakuwa Muislamu.

Uislamu aliokuja nao mtume Muhammad umetofautiana na walio mtangulia katika sheria ila imani na itikadi zao ni sawa.
 
KWA HAPA TANZANIA TENA HAINA NGUVU KAMA HUKO MASHARIKI YA KATI, WAKATI MWINGINE KAMA MMEPENDANA INATAKIWA MCHUKUANE HIVYO HIVYO WAZAZI WATAWAELEWA TU!
 
Ukitaka kuharibu jamii basi ruhusu mahusiano ya kimapenzi baina ya imani mbili tofauti.

Ukiona mtu ana uhusiano wa kimapenzi na mtu wa imani nyingine huyo hajitambui au anajiendekeza. Huu ukweli mchungu.
Ukweli upi mkuu?
 
Dah! Upo kama me nina binti wa kislamu me ni mkristo huyu mwanamke ni mzuri ile mbaya ananipa mahaba haswa ukirudi home anivua shati, viatu sometimes nalishwa sema sasa hiv kasafiri kikazi nimemmiss ila alinipa tahadhari kuwa Wazazi wake hawapendi yeye aje aolewe na mkristo ingawa bado sijajitambulisha kwao kujulikana.Mzee baba niliwahi kuleta mada hapa "Wanawake wa waislamu wengi Wana mahaba ukilinganisha na wakristo wakristo wanakwama wapi"? kuna baadhi wakanipinga especially wanawake wa kikristo lakini uhalisia tunauona sisi Wanaume kiukweli wanawake wakislamu wanajua mahaba na wajua kumtreat mwanaume vizuri kwenye Hili lazima tuwape sifa yao na mademu wakikristo wasione wivu kuna jambo la kujifunza kwao

Na sie wanawake wa Kikristo tuna mahaba mno na wanaume wa Kiislam sasa sijui tufanyaje???
 
Back
Top Bottom