SEHEMU YA SABA: "JICHO KWA JICHO” NA “JINO KWA JINO”
PART 1
Ilikuwa siku ya ijumaa, nilikuwa nimejikali nyumbani tu, siku hiyo nilikuwa nimeomba ruhusa ya kumpeleka mtoto shule kwa ajili ya sports day, na ilikuwa ni lazima kuhuwepo, hivyo niliongea na muajiri wangu na akanipatia likizo ya siku sita kama nilivyoomba. Kwani nisingeweza kupewa ruhusa ya siku moja kutokana na taratibu za kazi, akanishauri ni bora nichukue likizo ya siku saba kama kuna ambalo nataka kulifanya nilifanye kabisa.
Zaidi ya kuwepo shuleni kwa siku moja hiyo kwa sports day sikuwa na jambo lingine la kufanya. Sijui ni furaha ya kulipiza kisasi ama ni nini, Nilipendeza sana na kunawiri mno, uzito uliongezeka, lakini kutokana na umbo langu bado nilionekana nimependeza sana na kunawiri, kila aliyeniona alinisifia sana na kuniambia nimependeza mno. Hii ilinifanya niendeleee kupata moyo, wasijue yanayonisibu.
Ninazo siku 6 za kukaa tu nyumbani, hapana haiwezekani, nitasafari na Majid, kwani si kanihitaji mwenyewe, nitasafiri.
Je nitaombaje ruhusa? Lazima nitafute ugomvi, Jones nikimuomba ruhusa hivi hivi hataniruhusu, hawezi, hawezi, ananilinda sana sasa hivi, lazima nitafute ugomvi.
Ahaa, naweza kutafuta ugomvi, naweza hili halinishindi, naweza.
Niliporudi kutoka shuleni, Jones alikuja na kunikuta nimekaa chumbani, alikuwa na furaha sana. Ama Kweli ashukuriwe Mungu ambaye mwanadamu huwezi kuona moyo wa mtu anavyokuwazia, tungechinjana sana.
Aliingia ndani na kunikuta nimejibwaga kitandani, alikuwa na furaha sana,
Aliniuliza habari za mtoto shule, na nilimueleza ni njema sana,
Akaingia bafuni kuoga na akatoka, bado nilikuwa nimejilaza kitandani, kila nilipokuwa kimya nilikuwa nikitunga sheria, Kimya change siku zote kilikuwa sio cha kutulia tu hivi hivi la hasha, ni kimya cha kutunga shiria nitalipizaje kisasi ili wahusika waumie haswa.
Jones alitoka na alipotoka ikawa kama alijua namtaka uchokozi. Cha kwanza aliniuliza mbona kama umechoka? Ama umekunywa pombe zako tena Charlote?
Heeeee, alijuta,, nasema ungekuta nalumbana naye ungemhurumia.
Nilikaa, nilikuwa nimefunga khanga ya kifuani tu na kwani nilihitaji kupigwa na upepo. Kwa umbo langu lilivyo kubwa nilisimama na kila kiungo cha mwili wangu kilitetemeka kwa namna nilivyokuwa naongea, sio makali, mapaja , wala mikono na matiti,, nilisimama na kushika kiuno.
Nilimtazama na kumwambia,,, Jones, naona umenichoka,,hivi kwa nini huniamini? Nakuuliza hivi kwa nini huniamini? Kwa nini unapenda kuniambia sana kuhusu pombe? Si tumekubaliana ni ache na leo ni karibu wiki ya pili sinywi? Hivi mbona unapenda maneno wewe mwanaume? Khaaaa,,, nilikuwa nimeshika chupa ya perfume nikaipigiza chini, tena ile perfume aliyoninunulia.
Jones alishikwa na butwaaaa. Akanishika mikono na kusema, Charlote,, sipaswi kukuliza mama? Sipaswi mke wangu kukuuliza lolote? Ni makosa? Aliongea kwa upole sana,, niliitoa mikono yake kwangu kwa kuirusha ili iiachane,,
Kisha nikamtazama na kumuuliza,, hivi nikikuuliza Bado tu hujaachana na Husna utajiskiaje?
Jones, alisema basi mama, basi mke wangu yaishe,, yaishe…
Nilianza kulia na kulalamika ndoa gani hii ambayo haina furaha wala amani, ndoa gani hii jamani? Nililia sana na huwa nina machozi ya karibu sana.
Lakini nilikumbuka kwamba kinachoniliza ni uchungu wa Jones kuwa na mahusiano na Husna, yani jambo hili liliumiza sana moyo wangu na kuwa na Donda kuu lisilopona. Ndicho kiliniliza, nilimpenda sana jones, sikutaka kusikia habari hizi kabisa, na kusamehe nilishindwa, isipokuwa ahueni nilikuwa naipata kwa mimi kulipiza kisasi, na ni ahueni ya kuniliwaza kwa muda tu, lakini sio ya kuniliwaza kwa moja kwa moja.
Jones alinifuata na kuniambia mke wangu samahani, samahani Charlote mke wangu am sorry mami,, sikujua nimekuumiza samahani, yaishe.
Nilikuwa nalia sana, kweli hakukuwa na pombe kabisa ndani kwani nilishaacha kabisa kunywa, kwa sababu niliona najiumiza maini yangu. Kwa namna nilivyokuwa nakunywa nyingi bila kipimo. Nikaogopa kuwa abused na alcohol.
Ilifika saa mbili usiku bado tunalumbana, Jones aliniomba sana msamaha, nikawa siongei tena ila nalia tu.
Jamani,, ni kukuuliza tu ama kuna jengine charlotte? Mbona un hasira hivi? Huwezi kusamehe na kuachilia mke wangu?
Nilimtazama na kumwambia sio kirahisi hivi, Je wewe ukigundua nina mahusiano nje ya ndoa utajisikiaje? Nijibu nakuuliza utanisamehe?
Jones alisema ndio nitakusamehe. , nitakusamehe charlotte.
Nikamwambia, basi subiri siku niwe naye alafu nikuombe msamaha unisamehe.. mfyuuuu nikafyonza na kuondoka kuelekea chumba cha watoto ambacho hakitumini ila hutumika kwa waageni tu na kujifungia humo.
Nilifyonza kwani ninajua waname wengi ambao hawawezi na hawakuwasamehe wake zao mara baada ya kusikia, kuhisi ama kuiona wana mahusiano na wanaume wengine, hivyo nilijua kusamehe kwa mwanaume ni ngumu sana.
Nilikaa chumbani huko mpaka nikalala, nikiwa nimejifungia mlango. Jones alikuwa anajuta kwa nini alifanya mahusiano na Husna, ndoa yake sasa alianza kuiona achungu. Asijue mkewe nina agenda ya kulipiza kisasi na karibu sana mission yangu itatimia.
Aligonga sana, badae mida ya saa saba usiku nilifungua na kuelekea chumbani, nilimkuta amekaa anasoma kitabu, ni mpenzi wa kusoma, hakuwa na usingizi.
Aliniambia Charlote unanitesa sana, naumia sana juu yako.
Nilimwambia … Jones, maumivu unayoyapata ni moja ya nane na yamumivu niliyo nayo mimi kuhusu wewe na Husna, na sijui hili donda litaponaje, kila nikijaribu kuliponya inakataa.
Jones alinitazama na kuniambia,, kwa hivyo unataka kuniambia hukunisamehe?
Kwa sauti kabisa nilijibu, NDIO NIMESHINDWA KUKUSAMEHE, NIMESHINDWA.