SEHEMU YA TISA : MUME WA MTU MTAMU
PART 2
Baada ya wao kusafiri, mimi akili yangu ikiwa imetulia kiasi huku nasubiri warudi na waendelea na maisha yao ya wana ndoa.
Niliamua kubadilika kabisa, mawasiliano yangu na mzee Zuberi yalikuwa ya nadra sana na kwa siri sana, hatukutaka kufumaniwa tena na tulionana mara chache chache sana na kwa vile nilikuwa nataka tu pesa ya kujenga nyumba nilikuwa nikiwasiliana naye ili asisahau ahadi yangu, na siku zote aliniambia anakumbuka, na saa nilimpatia bank accaount number yangu na ilikuwa ni rahisi yeye kuniwekea pesa mara anapoenda bank, na aliniambia kwamba niwe naangalia salio kujua kwamba ananipenda na hatonisahau.
Lakini kwangu na mume wangu, nilirudisha mapenzi, na tukawa tunaishia kwa upendo wa hali ya juu kama hakuna kitu kilichowahi kutokea. Jones alifurahia sana namna nilivyokuwa namjali na kumpenda na kumtunza, alijifunia mimi.
Niliendelea kunawiri na kupendeza sana. Na siku moja nilipoelekea bank nilishangaa sana kukuta account yangu imeingiziwa milioni 11, hii ilikuwa ni maajabu kwangu, Haraka sana nilijua tu ni Mzee Zuberi, nilifurahi sana na kweli alikuwa ni yeye, nilifurahi sana na nisingeweza kuacha kumshukuru, niliamua kumpigia simu. Nilimpigia simu na iliiita sana haikupokelewa, iliiita mda mrefu sana, na haikupokelewa kabisa. Badae niliacha. Kwani sikupenda kuandika msg.
Na sikuandika kabisa msg. Badae sana mzee Zuberi alinipigia simu kwa namba ingine na kuniambia mkewe ameshkilia simu, hivyo nisipige wal akuandika msg, nilimwambia samahani nilitaka kukushukuru tu kuhusu pesa niliyokuta kwenye account yangu,, aliniambia haina neno mwanangu usijali.. mhh, nilishangaa kaniita mwanawe… nilishangaa sana.
Nilimuaga na kkubaliana sasa tuwe tunawasiliana kwa simu za ofcn tu na sio za mikononi. Nilimuelewa, na alinipenda kwani kila alichoniagiza nilikifanya sawa sawa na alivyosema.
Shaloo naomba uwe makini ili niweze kukusaidia, sitaki kukutafutia matatizo, ndoa yako bado changa. sawa mama,,, ndio nilijibu.. na alinipenda sana kwa utii wangu.
Nilirudi nyumbani nikiwa na furaha ya milioni kumi na moja. Na kiwanja hiki sikutaka k umshirikia mume wangu hata kidogo, sikutaka kabisa.
Ni kiwanja kizuri, kikubwa na kilichopo maeneo ambayo ni hot cake, ni kiwanja ambacho nikikigawa mara mbili na kuamua kuuza pc moja ni zaidi ya mamilioni ya pesa, pc moja tu ya mita 35 x 20 ni kama milioni 40 hivyo ni pesa nzuri sana. Na nilishaanza kuwazakuuza pc moja ili moja nijenge.
Na wateja walikuwa kila mara wakiulizia hicho kiwanja ni cha nani na je anauza? Hizi ni taarifa nilizokwua nazipata kutoka kwa majirani ambao wanaishi kwenye eneo hilo, na majirani wote wamejenga mijumba ya haja, ni mtaa ambao husifika kwamba ni mtaa wa wenye nazo. Kwani majuumbo yote ya mtaani hapo ni ya kifahari. Na mimi nilikuwa nataka niweke kitu chenye adabu pia.
********************************************************************************************
Maisha yalisonga sana, Majid na Husna walirudi kutoka Dubei, waliishi maisha yao mazuri sana, walikuwa wamepangisha nyumba nzuri tu ya kifahari, Husna alikuwa na gari yake nzuri ya kutembelea, na mara nyingi alikuwa akipendelea kukaa tu nyumbani, hakuwa ni msichana wa kupenda kujishughulisha, zaidi ya kukaa nyumbani. Na alikuwa ni mke wa kwanza kwa Majidi, na majidi naye alikuwa ni mume mkewe wa kwanza.
Walikuwa na ndoa nzuri. Miezi sita ilikuwa imeshapita, Husna alipendeza sana, alikuwa ni mke ambaye bila shaka aliipenda na kuimudu ndoa yake, alikuwa ni mke wa kujitanda sana na kuvalia vyema, hakuwa mke mang’aa, alimpenda sana mumewe.
Muda wote Majid aliponitafuta nilimueleza tafadhali naomba kaa na mkeo kwanza, afurahie ndoa yako. Mimi nipo tu wala kisikusumbue. Mimi wakati huo nilikuwa ni mtu wa kupanga taratibu zangu, sikutak Husna asiumie, nilitaka aumie kama nilivyoumia, Na nilipogundua Husna ana mimba nilifurahia sana, nilifurahia sana, nikasema sasa huyu ndiye mke haswa, na kama nikilipiza kisasi kipindi hiki ndipo kitanoga.
Bado sikuwa na haraka. Deal la flat screen nilishalikancell kwa Majid na nilimueleza tumepata ambaye atatupatia flat screen hizo. Hivyo bado aliamini ninaweza kumpatia biashara.
Na nilimueleza tu kwamba na mimi nahitaji kufanya biashara za kutoka na kwenda china, na je ni shilingi ngapi kama nikitaka kufanya biashara? Aliniuliza ni biashara gani nataka kufanya? Nilimueleza yoyote ambayo ingelipa, na aliniambia atanisaidia ila niandae kama milioni 50 hivi atanisaidia na kuniambia nifanye biashara gani.
Haraka nilikumbuka kiwanja, na nilikiweka sokoni. Na baada ya hapo nilikumbuka nina cach yangu kama milioni 15 hivi.
Kiwanja niliuza pc moja tu na nikapata milini 48, nilifurahia sana, na kisha nilimueleza Majid nina pesa ya kutosha kabisa.
Alinishangaa nawezaje kuwa na pesa nyingi hivyo? Nilimueleza huwa napokea tenda za watu wengi na wakinituma vitu huwa Napata na faida. Hivyo hizo pia ni kazi zangu.
Aliamini, kwani aliijua tabia yangu vyema, na sikuwa mwanamke was kendo mtaani, ila asijue ndo natengeneza skendo nay eye.
Aliniambia akitaka kusafiri atanijulisha, na atashughulikia kila kitu change, kuanzia ticket na visa na kil a kitu, na safari ya kwanza ilikuwa ni tunaenda Hongkong. Nilikuwa nimeshajipanga.
Niliongea na mume wangu na kumueleza nataka kufanya biashara hivyo anitafutie mtaji. Jones alinipenda sana, na hakuwa akiniwazia mabaya, aliniambia ni biashara gani nataka kufanya? Nilimwambia nataka kufanya biashara ya nguo na chochote ambacho nitaona kinafaa, ila taget yangu ni nguo.
Alifurahi kwa namna ambavyo nachanganya akili, na aliniambia yeye hana pesa ila kuna mikopo hutokea kazini, anaweza kunikopea kama milioni 20 ila nijue kwamba atakuwa hana pesa kwa yeye kukatwa marejesho ya kila mwezi.
Nilimhakikishia kwamba mimi ninapokea mshahara mzuri tu, na nitampatia card yangu ya bank ili awe nayo yeye kila mshahara ukiingia basi tusaidiane kubajet, tulimaliza makubaliano yetu vyema.
Sasa ikawa imebaki muda ufike ili nisafiri.
Ni kama miezi mitatu mpaka kusafiri, Na tayari nikawa natafuta frem.
Na jones naye akinisaidia kutafuta frem.
Husna ujauzito uliendelea kukua, nafikiri sasa ni mimba ya miezi 7 ama 8.
Safari ya China iliwadia. Nilikuwa nimekamilisha kila kitu change, kuanzia pesa, passport na visa. Hakuna ambacho sikuwa nacho.
Kazini niliomba ruhusa yangu ya mwaka mzma. Siku 28. Na pia sikujali sana kazi wkani sasa nilikuwa nataka kuwa mfanya biashara na kujikita kwenye biashara, niliona inavyolipa na mtu pia kupata muda wa kupumzika na kujipangia mambo mwenyewe. Niliamini ili uwe tajiri ama matajiri wengi ni wale ambao wametoka kwenye kuajiriwa, kujiajiri kisha Kuajiri, hawa ndio niliamini ni matajiri. Nilitamani kujiajiri kisha niajiri na mimi watu siku moja.
Nilishaanza kuona ukubwa wa duka langu la nguo, pochi na viatu, nilitaka kuwa famours in town ndizo ndoto zangu.
Saa kumi na mbili jioni tayari safari ya kuelekea airport ilianza. Mume wangu alinisindikiza mpaka airport.
Nilifika na tukawa tumekaa kwenye restaurant huku tukiwa tunapata kahawa tukisubiri muda usogee kidogo kwani tuliwahi sana kuogopa jam za mji.
Baada ya nusu saa nilimuona Husna na mumewe, niliweza kumgundua Husna baada ya kumuona Majdi, Nilitaka Husna anione na ajue ninasafiri. Hivyo nilimwambia mume wangu kwamba sasa nataka kucheck in kabla foleni haijawa kubwa.
Mume wangu alinikumbatia na tukaagana na akaondoka.
Kisha nilienda kukaa kwenye vitu nikisubiri kucheki in.
Baada ya kuhakiki Jones kashaondoka, nikiwa nimevalia Skin tight nyeuzi ambayo imeshika umbo langu sawia nd dress top nzuri ambayo ilinikaa vyema,, nilichukua cheni zangu mbili za miguuni kwenye pochi na nikazivaa, zilikaa vyema mguuni kwani Mungu kanijali mguu wa chupa ya bia,, na sendoz nilizovaa zilikamilisha umaridadi wa muonekano wangu wa miguuni. Kila mwanaume alinitazama kwa kunitamani.
Baada ya sekunde kadhaa nilitazama huku na huku, kisha nikaona Majdi na Husna wakiwa wanaagana… Nilipata kicheko moyoni,, huku nikishangilia sana .
Majid alikuwa na uhakika kabisa kwamba mke wake hanifahamu, hivyo hakuwa na wasi wasi.
Nilipita mbele yao,, Husna nilimuona kama ameshangaa Fulani hivi… Kisha nikapiga simu kumuaga rafiki yangu na kumueleza naenda china na nitarudi baada ya siku kadhaa.
Nilimuaga na Husna akasikia, lengo langu ilikuwa ni Husna atambue kwamba ninasafiri na mumewe.
Kisha nilisogea na kurudi kukaa kwenye kiti nikisubiri muda wa kucheki in ufike.
Muda ulifika na nailicheki in. Nilijua tu Husna ana mawazo, kwani kila nilipogeuka nilikuta akinitizama. Asiweze kuniambia lolote, na mumewe alipocheki in nilimsogelea na kumsalimia kwa mmkono, huku tukiwa tunaongea mawili matatu, Na husna alituona tukiongea,, maskini tayari nilishamuwekea alama ya ulizo. Na ndilo lilikuwa lengo langu, ajue maumivu ya mume na utamu wa mume. Hili ndilo nilikusudia miaka miwili iliyopita ya seke seke zima, na kuhakikisha KISASI CHANGU KINAFANIKIWA.
Tulisafiri, na Majid alizima simu yake.
Nilishangaa kupigiwa simu na mtu ambaye nina takribani miezi kama tisa hatuwasiliani,, akili ikaniambia huyu lazima ametumwa na Husna, kwani ni mtu ambaye pia alimfahamu husana na kisanga kizima.
Nilisema sasa ni muda wa kumueleza kila kitu kuhusu safari yangu. Nilimueleza nasafiri kwenda china, hongkong nitakaa huko siku kama 14 hivi, nimeenda kuvuta raha tu na kutuliza akili.
Aliniambie niko na nani? Nilimjibu si juu yako kufahamu, ila take care, nikirudi nitakuletea zawadi. Akaniambia basi usiache kunitumia mapicha yaw hats app, nikamwambia poa hizo umezipata,, na kwa kuanza tu nilimtumia picha kama mbili hivi ambazo mimi niko mbele form y amble na Majdi yuko form ya nyuma yangu tukisubiri ku board, nilifanya makusudi nikijua na kuhisi katumwa.
Husna roho yake ilikuwa ikidunda sana, bila shaka. Kwani huyu aliyekuwa akiwasiliana na mimi ni kama aliyekuwa akisukumwa kufanya hivyo na nilijua tu ametumwa. Baada ya dakika chache nilimuaga na kumueleza ninazima simu tutaongea nikifika, nikakata simu, na hao tulikuwa tunaelekea kwenye ndege.
Safari yetu ilikuwa nzuri sana nay a utulivu wa hali ya juu.
Tulifika na kupokelewa na mwenyeji wa Majid, Majid aliniambia huwa hapendelei kufikia hotelini na huwa anafikia kwa mwenyeji wake huyo, na tulienda pamoja .
Kweli nilikuwa nashangaa sana kwani ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kutoka nje ya nchi na kwenda kwenye nchi kama hiyo, nilikuwa nashangaa kila kitu, majengo bara bara na kila kitu.
Wiki ya kwanza ilikuwa ni wiki ya kutembea na kuujua mji, kisha nikaingiwa uchizi, nikaona kuliko kufanya biashara ya nguo ni bora nifanye biashara ya stationery,, niliona inavyolipa, basi nilkaa na kupiga mahesabu na kuona endapo nitamua kufanya biashara ya stationery nitapata pesa nyingi sana na kufanikiwa sana kuliko biashara ya nguo, na tayari niliamua kuwasilian na Jones na kumueleza. Hivyo akaniambia ni sawa tu, kikubwa nihakikishe kwamba nakwua makini kweye biashara na sio mchezo mchezo.
Mara zote Husna alipokuwa akizungumza na Majid ni kama walikuwa wangombana, Nilimuuliza Majid ni nini tatizo?
Aliniambia yani mke wangu sijui kaambiwa umbea gani, kaambiwa nimesafiri na mwanamke ila hataki kumtaja,, na ninajua hakuna mtu anajua issue yangu mimi na wewe. Nilimwambia ni kweli, ila wanawake tuna wivu tu, wewe ongea naye vizuri na muulize anataka ufanye nini ili asikie raha?
Majid alicheka na kusema dah kuoa kazi kweli kweli. Tulicheka wote, kisha tukaenda kupumzika na kukubaliana siku inayofuata ni kukusana mizigo baada ya kutembea maduka mengi kujua tunataka vitu gani.
Kweli siku iliyofuata ilikuwa ni siku ambayo tuko busy sana, tulitiembea sana na kuchoka sana, kisha tukapata mizigo yote na kuikusanya, Na majidi akaniambia kwamba ataaweka mzigo wangu kwenye contena lake hivyo nisijali kwani haoni sababu ya kuniombea mizigo yangu kwa baadhi ya watu anaowafahamu, hii ni ili kulinda usalama wa mahusiano yetu.
Nilifurahia sana na kweli siku mbili zilizofuata ikawa ni kufunga mizigo kwenye contena kisha kuanza hatua za kukabidhi mzigo ili usafirishwe. TUlimaliza process zote hizo salama na sasa kujipongeza, na siku sita zilizobaki kabla ya kurudi Tanzania, tuliazimia kujirusha na kutembea baadhi ya miji ya jirani kuvuta raha tu.
Tulivuta raka kama tulivyokubaliana. Na baada ya kupongezana tulijiandaa kurudi Tanzania. Kiusalama zaidi, Nilitangulia mimi na siku iliyofuata Alikuja Majid.
Jones alifurahia kuwa na mwanamke kichwa ambaye anawezakubuni biashara nzuri kwa haraka. Nilifika na kumueleza kila kitu kuhusu safari yangu, na miji ya china ilivyo, alitamani sana kusafiri nay eye. Nilimwambia tuombe Mungu biashara iwe nzuri kisha tutasafiri tu.
Aliniambia ameshapata frem, na tulianza kuifuatilia na kuiandaa kwa ajili ya kuweka biashara yetu.
Baada ya muda kidogo tu, mizigo iliwasili na kufngua stationery. Ilikuwa kubwa, nzuri ,nilikwua na mashine za photocoyy. Scarner na kila kitu, kila mteja aliyekuja pale alipata huduma zote alizohitji pamoja na kuuza bidhaa zote za muhimu ambazo zinahitajika kwenye stationery. Nilianza kuktafuta wateja kila mahali, Na mzee Zuberi alinisifia sana kwa kazi nzuri niifanyayo na alinitafutia wateja kwa hali na mali. Sasa nilikuwa naingiza pesa bara bara.
Maisha yalianza kuwa matamu, na niliandika barua ya kuacha kazi. Na niliacha kazi. Wala sikujuta, stationery yetu tuliiweka karibu na maeneo ambayo watu walihitji huduma hiyo.
Siku moja nikiwa ofcn, Majid aliamua kunitembelea, Alikuja na hakuamini kunikuta kwenye stationery ambayo imejaa, imependeza sana, na kwa vile kazi hiyo niliisomea nilitafuta pia wasichana wawili wambao ni liwakagua vyema na kujua wanaijua kazi hiyo vyema na kuwaajiri. Biashara ilikuwa nzuri sana, Majid alinisifia sana na alinipenda sana.
Sasa kupatikana kwangu kukawa shida, kwanza kumbuka Sikumpenda Majidi kimapenzi ila kulipiza kisasi.
Kisha sasa nina biashara yangu naifanya na sitaki kuharibu biashara yangu, hivyo kunipata kwangu ikawa taabu sana, na hakuweza kuvumilia, ikawa anapiga simu kila mara hajali tena, na mkewe akawa yuko kwa mama yake akila uzazi, alijaliwa mtoto wa kike.
Maisha yangu yalikuwa mazuri mno, ni kama nilikuwa natamani sasa nisilipize kisasi, lakini hapana nitaachejee kulipiza kisasi ili hali Husna hajaonja joto ya jiwe?
Hili ndilo lilikuwa likinikera, ni lazima kimuume kama kilivyoniuma mimi.
*********************************************************************************