Jamaa alikuwa safarini na mkewe wanatoka Arusha kuelekea Mbeya, muda mwingi mkewe yupo busy na simu anachat wakati mwanaume anaendesha gari yao ndogo wapo wawili tu.
Wamefika maeneo ya Mtera machakani, mke akamwambia mumewe simama nataka kuchimba dawa. Mume kasimamisha gari, mwanamke kashuka katokomea vichakani kwenda kuchimba dawa.
Unaambiwa mume alisubiri zaidi ya masaa, mkewe hatokei na akipiga simu yake mwanzo ilikuwa inaita haipokewi halafu baadaye ikawa haipatikani.
Ikamlazimu mume kwenda kuripoti kituo Cha polisi Mtera wakati huo anawasiliana na ndugu jamaa na marafiki. Baada ya muda jamaa zake walioko Iringa mjini wakampigia simu kumwambia mkewe ameonekana Iringa mjini akiwa na kijana mmoja shombe shombe wa kiarabu.
Hili lilimtokea baada ya kuwa kwenye ugomvi wa muda mrefu baina ya mume na mke, mke akidai talaka kwa kipindi kirefu bila mume kuridhia jambo hilo.
Kijana shombe shombe wa kiarabu alikuwa ni hawara wa yule mwanamke kwa zaidi ya miaka 2 ( kwa mujibu wa marafiki wa mwanaume ~mume wa yule mwanadada).
Jamaa hakuamini kilichomtokea na ndoa yao ya miaka kadhaa na watoto 3 iliishia hapo.
Sent using
Jamii Forums mobile app