Nilivyo sasa baada ya kumfuma mwamba akilia mbele ya wazee na mkewe ili asiachwe!

Nilivyo sasa baada ya kumfuma mwamba akilia mbele ya wazee na mkewe ili asiachwe!

Binadamu tunatofautiana hisia. Nimrshashuhudia kwa jirani yangu aliachwa na mtoto mdogo mke kakimbia kwenye ngoma huko kwao jamaa akimtafuta mke hapokei simu na unaambiwa kwenye ngoma mkewe akinogewa anagawa uroda hadibkwa mpiga ngoma. Basi siku moja napita kwake nimjulie hali nikamkuta mwanae ni mdogo bado ila anaongea kumuuliza baba yuko wapi akaniambia baba alia ile kitoto toto sikuamini nikaita jirani mwamba kutoka macho yamejaa nikahoji vipi mwamba nae akafunguka niliumia roho pia ila nilichojifunza sio kila mtu anaweza kukaza asitoe chozi kutokana na mapito yake. Yaani kibaya dem akirudi wanaendelea kama kawa kwahyo ukijidai mshauri sana unaumbuka. Namuomba sana Mungu anipe huruma kwa familia yangu ila sio swala la kulilia mtu anaetaka kuondoka
Mke akirudi Wanapima ngoma Kwanza au wanaliendeleza hivyo hivyo?
 
Mke akirudi Wanapima ngoma Kwanza au wanaliendeleza hivyo hivyo?
Hilo sina uhakika nalo ila nijuavyo akirudi hakuna hata ugomvi unaotokea na wanaishi kama halikutokea jambo. Anaebaki kuumia ni mwanaume
 
Na hukumlilia hata mmoja!?
Acha kutupanga bwana, sema ukweli wako.
Wale wandere walinitenga na jamaa zangu....

Wale wandere wakanifanya weekend kutwa nishinde nao ndani...

Na mengine mengi ila sikufika kiwango cha kihobobo kuwalilia kwa kuwasotea magoti kama huyo mwamba [emoji1787]
 
Hakuna cha upendo wala nini, huyo jamaa yuko chini ya ulinzi wa malimbwata, hiyo iliwah kumtokea Rafiki yangu mmoja badae akaja kusaidiwa na Mjomba wake.

Ni kwamba, wanawake wanatuzidi sana wanaume katika mambo ya kiroho kwenye ndoa, na ndio maana wao huchelewa kufa, hv mtu kakulisha madawa ya kukufunga akili popote ulipo ni kumuwaza yeye anatembea nje unaletewa taarifa unapuuza (ndivyo malimbwata yalivyo), akikufanyia visa say amekunyima tendo miez hata 6, hiyo presha, msongo wa mawazo unakutokaje?

Huyo jamaa angefunguliwa hivyo vifungo asingemtazama huyo mwanamke mara 2, angetoa na talaka papo hapo.
Exquisite [emoji2956][emoji109]
 
Jamaa alikuwa safarini na mkewe wanatoka Arusha kuelekea Mbeya, muda mwingi mkewe yupo busy na simu anachat wakati mwanaume anaendesha gari yao ndogo wapo wawili tu.

Wamefika maeneo ya Mtera machakani, mke akamwambia mumewe simama nataka kuchimba dawa. Mume kasimamisha gari, mwanamke kashuka katokomea vichakani kwenda kuchimba dawa.

Unaambiwa mume alisubiri zaidi ya masaa, mkewe hatokei na akipiga simu yake mwanzo ilikuwa inaita haipokewi halafu baadaye ikawa haipatikani.

Ikamlazimu mume kwenda kuripoti kituo Cha polisi Mtera wakati huo anawasiliana na ndugu jamaa na marafiki. Baada ya muda jamaa zake walioko Iringa mjini wakampigia simu kumwambia mkewe ameonekana Iringa mjini akiwa na kijana mmoja shombe shombe wa kiarabu.

Hili lilimtokea baada ya kuwa kwenye ugomvi wa muda mrefu baina ya mume na mke, mke akidai talaka kwa kipindi kirefu bila mume kuridhia jambo hilo.

Kijana shombe shombe wa kiarabu alikuwa ni hawara wa yule mwanamke kwa zaidi ya miaka 2 ( kwa mujibu wa marafiki wa mwanaume ~mume wa yule mwanadada).

Jamaa hakuamini kilichomtokea na ndoa yao ya miaka kadhaa na watoto 3 iliishia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
.....na ndio maana bila ya mwanaume kutokuwa na moyo mkuu na wa subira matokeo ni KUJIPOTEZA wewe na malengo yako...

Sasa wanaume wengi tuna ufahamu huo...unaanzaje kulia na kumpigia magoti mwanamke...mbususu tu ?!! Mhhh hapo kuna namna [emoji1787]
 
Nimefadhaika, nimehuzunika, nimekasirika, nimeshangaa, nimechoka na nimekata tamaa kabisa!!

Yaani jamaa analia 'live' mbele ya wazee waliokuja kusuluhisha mgogoro wao na mkewe ambaye anadai talaka aondoke.........analia huku amempigia magoti mkewe (huku wazee wakishuhudia) akimsihi asiondoke. Dah!!!!
Wakati nipo mdogo niliwahi kushuhudia kwa kumchungulia chumbani jamaa akimlilia demu wake kuwa anamtesa!!!, yani kilio kabisa mixer kwikwi na demu anamkalisha kwa maneno ya karaha kabisa , mwishowe demu akamuamuru jamaa afute machozi ili amsamehe, na kweli yakaisha ! Mwamba alikuwa mbabe haswa na kijiji kizima tulikuwa tunamuogopa !!!

Never underestimate power of papuchi !! That's all i can say.
 
Binadamu tunatofautiana hisia. Nimrshashuhudia kwa jirani yangu aliachwa na mtoto mdogo mke kakimbia kwenye ngoma huko kwao jamaa akimtafuta mke hapokei simu na unaambiwa kwenye ngoma mkewe akinogewa anagawa uroda hadibkwa mpiga ngoma. Basi siku moja napita kwake nimjulie hali nikamkuta mwanae ni mdogo bado ila anaongea kumuuliza baba yuko wapi akaniambia baba alia ile kitoto toto sikuamini nikaita jirani mwamba kutoka macho yamejaa nikahoji vipi mwamba nae akafunguka niliumia roho pia ila nilichojifunza sio kila mtu anaweza kukaza asitoe chozi kutokana na mapito yake. Yaani kibaya dem akirudi wanaendelea kama kawa kwahyo ukijidai mshauri sana unaumbuka. Namuomba sana Mungu anipe huruma kwa familia yangu ila sio swala la kulilia mtu anaetaka kuondoka
Daaah maskini
 
Umewaza uchawi lakini mapenzi ni zaidi ya uchawi na nyumba hizi zinaficha mengi,

Kabla hujafa, omba ukutane na mtu akupe mapenzi na mahaba.
Asee uko sahihi kabisa , halafu sidhani kama ni kupewa mahaba , kuna mtu unakutana naye halafu mna click tu .
Binafsi wala sitaki tena kukutana na mpenzi wa aina hiyo , maana niliwahi kuteseka sana kwa dada fulani, siku aliyosema tuachane ni kama aliondoka na moyo wangu , sijawahi kupata breakdown ambayo iliniumiza kama hiyo, halafu sasa wala hakuwa beauty qween .na wala siamini kama nililogwa .
 
.....na ndio maana bila ya mwanaume kutokuwa na moyo mkuu na wa subira matokeo ni KUJIPOTEZA wewe na malengo yako...

Sasa wanaume wengi tuna ufahamu huo...unaanzaje kulia na kumpigia magoti mwanamke...mbususu tu ?!! Mhhh hapo kuna namna [emoji1787]
Huyo jamaa ilibidi wataalamu wa saikolojia wafanye kazi ya ziada ili kumuamisha kwamba mkewe hayupo naye tena maana kumtoa tu pale Mtera ilichukua takribani siku nzima akiamini mkewe atatoka machakani alikoenda kuchimba dawa arejee kwenye gari safari yao kuelekea Mbeya iendelee. Alitamani kujiua, alijifungia ndani kwa zaidi ya miezi 2 hafanyi chochote.....mapenzi ni kitu mbaya sana yakikukalia vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asipolia unadhania nani atakayempa hivyo vitu anavyopewa, Muache alie tu anajua akatayoyakosa😂😂😂
 
Back
Top Bottom