Nilivyofyeka shamba la nyanya ekari moja la jamaa aliyekuwa akinichapia mpenzi wangu

Huu uzi unamhusu mwanamke msaliti ndio maana tunazungumzia upande huo.
Mkuu rejea comment yako ya kwanza ulisema mwanamke akikucheat ujue mwenye makosa ni mwanamke, sawa labda nikuulize vipi na mwanaume naye akicheat mwenye makosa anakuwa nani, labda nitaeleweka ninachotaka kusema
 
Utaacha wangapi mzee baba...! Unachekesha ujue
 
Vp sasa hivi anaekugongea unampango wa kufanya nn. Mwanaume usie na ujasiri haustahili kuishi
 
Imekaa mahala pake. Ukiona dem kakucheat basi hukua mwanaume wa kumtosha mwamba anakimbilia kuharibu mali zisizohusikaπŸ˜‚πŸ˜‚
 
.......ujinga ni pale ambapo tunaoa malaya then tunawaingiza hasara wanaume wenzetu.......
Mwanamke ni kiumbe dhaifu. Anaweza asiwe malaya lakini ukimkutanisha na watu wenye tamaa na mikwanja mirefu anaweza kukuona bonge moja la fala na kulegeza kamba kwa hao mabaharia. Ndio maana waarabu na wapemba wanawafungia ndani wanawake zao!
 
Wewe ndo mjinga. Mwanamke hatumii akili yake kufanya maamuzi bali hisia. Utakuta jamaa aliyemchapa alimdanganya tu ni yatima anaishi kwa tabu halafu manzi akamwonea huruma na kumpa tamu. Aliyekuchapia ndo wa kudili nae.
 
Weee jamaa ni mshamba sana demu alikuwa hakupendi unaleta swagga za kijijini. Alafu unaona ulifanya ujanja mwenyewe
 
Mwanamke ni kiumbe dhaifu. Anaweza asiwe malaya lakini ukimkutanisha na watu wenye tamaa na mikwanja mirefu anaweza kukuona bonge moja la fala na kulegeza kamba kwa hao mabaharia. Ndio maana waarabu na wapemba wanawafungia ndani wanawake zao!
.......uko sahihi kabisa mkuu, na hii ina maana mwenye jukumu la kulinda mahusiano au ndoa ni wewe mwenyewe mwenye ndoa, so huyu Jamaa yetu ilipaswa amlinde mkewe na kama alishindwa ilibidi akomae na mkewe kwa kufanya usaliti huo na sio kuleta tabu kwa wengine........
 
Mimi nilishawahi kuleta kisa humu. Nilimfungulia biashara mwanamke ili asikae doro, nikitoka mihangaiko tunakusanya na alichouza ili tupunguze makali ya maisha.

Aisee kumbe ndio nilikua nimewasogezea nyama wauza bucha aisee. Pisi ikawa inakutana na majibaba yenye pesa anapoenda kufatilia mizigo ya dukani kwenye maduka ya jumla. Wakamrubuni tukaishia kutemana. Biashara nikamuachia nikaendelea na mishe zangu! Kaishia kuifilisi na sasa hivi anajuta.

Ila nimepata funzo ina a very hard way!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…