Nilivyoingiza 17.6M ndani ya mwaka mmoja na nusu, kwa biashara ya Mgahawa kwa mtaji wa kawaida kabisa

Nilivyoingiza 17.6M ndani ya mwaka mmoja na nusu, kwa biashara ya Mgahawa kwa mtaji wa kawaida kabisa

Namlaani sana aliyenifundisha kubeti maana nimeshindwa kuacha na imekuwa sehemu ya maisha, kuna muda unasema umeacha ila baada ya miezi kadhaa narudi kulekule.
Bro ktk Madhambi makubwa dini yetu ya kiislamu basi KAMARI kumi bora hakosi any way nakupa pongezi na hongera kwa uthubutu wa kuamua kufanya biashara .Jambo lolote ukiamini kulifanya special la halali basi litakutoa tu kwa mfano kulikuwa na mshu shine moja mombosa miaka hiyo alikuwa akitamani amiliki bus la abiria naam alijipanga kila peni lake halitoki mfukoni na ilifika siku alimiliki bus na kazi yake hakuuacha ya shoe polish .Warusi wana joke yao moja hiyo maarufu urusi kulikuwa na bwana mmoja miaka ya nyuma akifanykazi 24/7 wakimwita Papa Kala ukimwambia mtu niko buzyy sana wanakwambia ww papa kala.
 
Habari zenu humu ndani?

si muandishi mzuri sana wa nyuzi humu jf ila leo nimejisikia kushare kitu kidogo na nyinyi juu ya biashara, nikiamini kwamba naweza kubadili fikira za baadhi ya vijana na wazee humu juu ya biashara.

Kwa taaluma mimi ni Civil Engineer na huwa napata vikazikazi ambavyo husukuma maisha yangu kwa kipato cha kawaida tu ila mwaka 2021 nilienda na jamaa yangu mmoja kama msindikizaji (kupoteza muda na kujifunza kitu kuhusu biashara ya dhahabu) sehemu moja inaitwa Dutwa ambako machimbo ya dhahabu yalizuka, kwa watu wa dhahabu watakuwa wanapajua vizuri. Sasa ile kufika kule nikakuta pilika za watu wengi balaa na huduma za jamii zinatolewa kwa bei ya juu kabisa, kwamfano watu walikuwa wanalala kwenye tugest tudogo twa mabati kwa 10K pre day so ukikuta mtu anavyumba 20 anakunja 200K yake kwa siku vizuri kabisa tena kwa kugombaniwa.

Nilivyorudi nyumbani Mwanza nikaa na kujiuliza sana mwisho wa siku nikaamua kuja na wazo la kwenda kuuza chakula kule, nilipojaribu kukusanya mawazo kutoka kwa watu nilikatishwa sana tamaa maana wengi walisema biashara kwenye migodi ya kulipuka huwa sio za kudumu kwana watu huhama mara kwa mara. Nilifikiria sana baadae nikaamua kujitoa mhanga, nikaandaa 2M kwaajili ya kujenga guesthouse za mabati na mgawaha na vyote nilivipa jina la CALFONIA HOLEL & CALFONIA GUEST (kwa wale waliowahi kufika dutwa namba moja watakuwa wanazijua), hazikuwa za kisasa sana ila kwa kiasi fulani niliset standards ukilinganisha na vimigahawa vingine vidogovidogo na guest za pale kihuduma.

MWANZO WA BIASHARA:
Nilinunua kila kitu kinachotakiwa kuanzisha mgahawa na ilinigharimu kama 1M nyingine, nilidhamiria kuuza kila kitu tofauti na wengine ambao walikariri chapati na chai, wali maharage nyama. Mimi nilitafuta mpishi mzuri kwaajili ya bites tu(chapati, Af cakes, na vitumbua na chai) ambae nilimlipa 10K siku, kisha nikatafuta pishi wa ugali na wengine wawili kwajili ya vitu vingine (Nyama, Samaki, wali, kuku, mbogamboga, maharage, maini...nk). Wahudumu nilitafuta wanne ambao niliwashonea sare kabisa.

Nilivyoanza sikutaka kucheka na nyani kwakua vitu vilikuwa standard nilikuja na bei ambazo hazikuwako kabisa. Kwamfano:-

Chapati 500Tsh (wao 300)
Andazi 500Tsh (wao 200)
Kitumbua 250Tsh (wao 200)
Wali nyama 3500Tsh (wao 2000)
Wali roast 4000Tsh (wao 3000)
Supu 2000Tsh (wao 1000)
Kipande kimoja cha nyama ya kuku ilikuwa ni 6000.
Samaki mzima nilikuwa nauza 10K hadi 12 wakati mimi nilikuwa nawachukulia 5k hadi 7K pale Ramadi, yani ni kwamba nilinunua vitu kwa bei ndogo na kuuza mara mbili yake. Nilizingatia usafi wa eneo langu na wahudumu wangu muda wote.

Siku ya kwanza hadi ya nne mauzo hayakuwa mazuri sana ila yalienda yanaongezeka,nadhani walikuwa wanapeana habari. Wiki ya pili nilianza kuuza hadi nilishangaa maana watu wa kule wakikaa kula hakuna kujibana, kwenye mgahawa wangu watu walipishana wengi sana ambao kwa mjini ili uwapate unahitaji uwe na mtaji mkubwa sana, nilipata tenda hadi kwenye ofisi za shamba ambako walikaa wale makota wa dhahabu. Mauzo ya chai na supu(7Kg) yalifika hadi 120K-140K kutokana na siku, mchana hadi usiku kwa pamoja nilikuwa nakusanya mauzo si chini ya 350K-400K (watu mtashangaa ila uhalisia ulinishangaza hata mimi)

Baada ya hesabu na kuwalipa wafanyakazi kukunja 60k-70k kama faida ilikuwa ni swala la kawaida kabisa. Nikikaa pale kama cashier kwa wiki tatu kisha baada nikaleta ndugu asimamie ili nirudi mwanza kuendelea na issue nyiingine ila akaanza kuniletea habari za faida 20K wakati mimi nishapiga hesabu za mbali kabisa, nilimtoa nirudi mwenyewe mzigoni(sikutaka kumpeleka wife kule mgodini) na mambo yakaendelea kuwa mzuri na mpaka mwisho wa mwezi ule nilikunja kama 1.2M benki. Biashara ya Guest Ilianza kuzorota maana ilifikia hatua chumba ikaw ni 3k baada ya guest kuwa nyingi.

CHANGAMOTO KUBWA:

Baada ya kama miezi miwili mambo yalianza kwenda kombo yani nikawa nauza msosi kwa raia wengi ila usiku wakati wa mahesabu hakuna hela hadi naanza kubembelezana na wafanyakazi kuwalipa hela, nikaanza kuchukua hela nje ya biashara ili kuinusuru, niliwaza labda naibiwa na wafanyazi ila kwakua mimi ndo nilikuwa mshika hela sikufikiria hivyo sana. Mimi huwa ni si muumini wa wa mambo ya tiba asilia na nilikuwa na msimamo sana ila baada ya kuona vyakula vinaisha ila hela haionekani jioni nikaamua kuomba ushauri, kila mtu akawa anadai bariadi wachawi sana na kwamba sitatoka na kitu nikizubaa. Nikaamua kumshirikisha mjomba wangu mmoja aliyekuwa anafanya kazi GGML ambaye alikuwa ni tajiri sana kutokana na biashara zake nyingi( RIP), alinisisitiza sana swala la kwenda kwa mganga nilikataa sana ila baadae niliingia kwenye line kisha akaniunganisha na mzee fulani hivi (sitaki maswali PM) nikaenda kuaguliwa japo kishingo upande, niliambiwa kuwa kulikuwa na chuma ulete kwenye biashara yangu na kwamba hela zikikuwa hazikai.

Niliporudi ofisini mambo yalichachamaa kaisi kwamba ikanilazimu kuongeza wahudumu kutoka wanne hadi 9 ili kuendana na kasi ya wateja, watu walitoka mbali (namba 2 na 7 kuja kula Calfonia ambayo ipo namba 1), kikuweli niliuza sana kisha baadae niliongeza biashara ya chips na nyama choma ambayo nayo ilinipa faida sana, swala la kuweka 90K- 120K kama faida likawa la kawaida sana au la lazima kabisa na kila mwisho wa mwezi benki ilibaki 900K- 1.4M (haikuwa constant kwasababu ya matumizi ya kijinga ikiwemo betting)

Hili swala la betting nilishashindwa kabisa kuliacha, na hata humu Jf mimi ni member mzuri tu wa jukwaa la mikeka😄.

Maisha yalikuwa mazuri sikuwa na hitaji kufanya kingine kabisa tofauti na mgahawa wangu, Mwanza nikawa naingia weekend (ijumaa- jpili) na nikifika na kula bata na marafiki na jamaa na kila aliyeuliza mishe yangu mpya nilimwambia nipo mgodini😄.

Baada ya mwaka mmoja mgodi ulienda unapunguza idadi ya watu walihamia Kakola na sikuwa na mpango wa kukimbizana nao hasa nikiangalia faida niliyoipata ndani ya muda huo, taratibu mauzo yalipungua mpaka ilipofikia mwezi wa tatu nikaamua kuibomoa nili nirudi kutulia nyumbani.

Mpaka nafunga biashara benki nilikuwa na 17.6M achilia mbali zile ambazo nilikuwa na kula au zile ambazo nilikuwa naliwa kwenyr betting.

NILICHOJIFUNZA

👉🏽Biashara ni location, huo mgahawa ukiuleta Mwanza mjini ungeonekana local kabisa na pengine nisingepata haya mauzo kabisa.

👉🏽Kwenye biashara utajikuta tu unaingia kwenye ushirikina kutokana na nature ya wateja ambao utawapokea (wapo wasio na nia nzuri ) unless uwe mcha Mungu thabiti kitu ambacho wengi hatuwezi.

👉🏽Ningekuja kuomba ushauri humu jf kwa mtaji ambao nilianza nao pale basi ningekata tamaa, maana humu nilishawahi kuona jamaa anasema hata mtaji wa 12M hauwezi kukupa faida ya 2M daaah😄.

👉🏽Kuna mishe zinaonekana za kijishusha viwango sana ila kiuhalisia ni zinalipa sana kama utaamua kuweka aibu pembeni.

NB; Sijaeleza yote, mengine nitakuwa naeleza huko chini kutokana na maswali ya wadau.
Mbwembwe nyingi kumbe unampgia promo Karumanzila
 
Bro ktk Madhambi makubwa dini yetu ya kiislamu basi KAMARI kumi bora hakosi any way nakupa pongezi na hongera kwa uthubutu wa kuamua kufanya biashara .Jambo lolote ukiamini kulifanya special la halali basi litakutoa tu kwa mfano kulikuwa na mshu shine moja mombosa miaka hiyo alikuwa akitamani amiliki bus la abiria naam alijipanga kila peni lake halitoki mfukoni na ilifika siku alimiliki bus na kazi yake hakuuacha ya shoe polish .Warusi wana joke yao moja hiyo maarufu urusi kulikuwa na bwana mmoja miaka ya nyuma akifanykazi 24/7 wakimwita Papa Kala ukimwambia mtu niko buzyy sana wanakwambia ww papa kala.
Unadhani sijui kuwa mi dhambi mkuu? Naelewa ila ndiohivyo nimenaswa, naweza kusema nimeacha then baada ya mwezi unajikuta kulekule.

Nimepokea pongezi zako mkuu, asante.
 
𝐂𝐇𝐀𝐊𝐔𝐋𝐀!! 🍍🍉𝐂𝐇𝐀𝐊𝐔𝐋𝐀!!🍗 𝐂𝐇𝐀𝐊𝐔𝐋𝐀!! 🥥𝐂𝐇𝐀𝐊𝐔𝐋𝐀!!🍔 𝐂𝐇𝐀𝐊𝐔𝐋𝐀!!!
꧁༒☬*𝓤𝓼𝓪𝓯𝓲 𝓝𝓪 𝓒𝓱𝓪𝓴𝓾𝓵𝓪 𝓒𝓱𝓮𝓷𝔂𝓮 𝓛𝓪𝓭𝓱𝓪 𝓝𝓭𝓲𝓸 𝓜𝓼𝓲𝓷𝓰𝓲 𝓜𝓴𝓾𝓾 𝓦𝓪 𝓚𝓪𝔃𝓲 𝓨𝓮𝓽𝓾☬༒꧂

𝐊𝐰𝐚 𝐌𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐲𝐚 #𝐌𝐏𝐈𝐒𝐇𝐈𝐈 𝐖𝐚 𝐤𝐮𝐩𝐢𝐤𝐚 𝐊𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐒𝐡𝐮𝐠𝐡𝐮𝐥𝐢 𝐲𝐚𝐤𝐨 Au Mgahawa 𝐘𝐮𝐩𝐨 𝐇𝐚𝐩𝐚.😊
𝐏𝐨𝐩𝐨𝐭𝐞 𝐩𝐚𝐥𝐞 𝐭𝐮𝐧𝐚𝐤𝐮𝐣𝐚 𝐤𝐮𝐟𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐤𝐚𝐳𝐢.

𝐓𝐮𝐧𝐚𝐩𝐢𝐤𝐚 𝐁𝐈𝐑𝐈𝐀𝐍𝐈, 𝐏𝐈𝐋𝐀𝐔 𝐊𝐔𝐊𝐔/ 𝐍𝐘𝐀𝐌𝐀, 𝐍𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐂𝐇𝐎𝐌𝐀, 𝐒𝐀𝐌𝐀𝐊𝐈 𝐖𝐀𝐋𝐈 𝐌𝐖𝐄𝐔𝐏𝐄/𝐌𝐀𝐔𝐀, 𝐍𝐃𝐈𝐙𝐈 𝐍𝐘𝐀𝐌𝐀/𝐔𝐓𝐔𝐌𝐁𝐎, 𝐌𝐀𝐍𝐃𝐈, 𝐒𝐀𝐌𝐁𝐔𝐒𝐀, 𝐊𝐔𝐊𝐔 𝐂𝐇𝐎𝐌𝐀, 𝐊𝐀𝐓𝐑𝐄𝐒𝐈 𝐧.𝐤😋
𝐏𝐢𝐚 𝐓𝐮𝐧𝐚𝐤𝐮𝐩𝐢𝐤𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐊𝐮𝐤𝐮𝐥𝐞𝐭𝐞𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐖𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢 𝐔𝐧𝐚𝐨𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐭𝐞𝐧𝐚 𝐊𝐢𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐛𝐚𝐝𝐨 𝐜𝐡𝐚 𝐌𝐨𝐭𝐨𝐨𝐨𝐨🔥🔥🔥🔥🔥🔥
𝐊𝐚𝐦𝐚 𝐔𝐭𝐚𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐁𝐔𝐅𝐅𝐄𝐓 𝐏𝐢𝐚 𝐈𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐞𝐤𝐚𝐧𝐚 𝐍𝐢 𝐰𝐞𝐰𝐞 𝐍𝐚 𝐕𝐢𝐥𝐞 𝐮𝐧𝐚𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐓𝐮𝐧𝐚𝐤𝐮𝐩𝐚 𝐇𝐮𝐝𝐮𝐦𝐚 𝐁𝐨𝐫𝐚 𝐊𝐚𝐛𝐢𝐬𝐚𝐚.
𝐊𝐰𝐚 𝐖𝐚𝐭𝐞𝐣𝐚 𝐖𝐚𝐩𝐲𝐚 𝐖𝐨𝐭𝐞 𝐓𝐮𝐧𝐚𝐩𝐢𝐤𝐚 𝐊𝐰𝐚 𝐁𝐞𝐢 𝐘𝐚 𝐏𝐔𝐍𝐆𝐔𝐙𝐎 * *𝟒𝟎% 𝐍𝐚 𝐤𝐮𝐡𝐚𝐤𝐢𝐤𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐀𝐦𝐞𝐥𝐢𝐝𝐡𝐢𝐚 𝐇𝐮𝐝𝐮𝐦𝐚 𝐘𝐞𝐭𝐮 𝐊𝐰𝐚 𝐀𝐣𝐢𝐥𝐢 𝐘𝐚 𝐊𝐮𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐚 𝐊𝐮𝐟𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐍𝐚𝐞 𝐤𝐚𝐳𝐢 𝐧𝐲𝐢𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐳𝐚𝐢𝐝𝐢.
𝐊𝐰𝐚 𝐌𝐚𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐨☎️📞
𝐏𝐢𝐠𝐚/𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐚𝐩𝐩: 𝟎𝟔𝟓𝟕 𝟑𝟑 𝟐𝟖𝟏𝟒
𝐈𝐧𝐬𝐭𝐚𝐠𝐫𝐚𝐦: @𝐦𝐩𝐢𝐬𝐡𝐢𝐢_
𝐄𝐦𝐚𝐢𝐥:📧𝐦𝐩𝐢𝐬𝐡𝐢𝐦𝐚𝐬𝐡𝐮𝐡𝐮𝐫𝐢𝐧𝐢@𝐠𝐦𝐚𝐢𝐥.𝐜𝐨𝐦
𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐔𝐍𝐆𝐔 𝐀𝐖𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈𝐊𝐈
 

Attachments

  • mpishii .jpg
    mpishii .jpg
    63.3 KB · Views: 39
  • Ndizi.jpg
    Ndizi.jpg
    62.3 KB · Views: 42
  • BIRIANI .jpg
    BIRIANI .jpg
    98.4 KB · Views: 46
  • Mpishii 0657 33 2814 .jpg
    Mpishii 0657 33 2814 .jpg
    67.1 KB · Views: 46
  • NDIZI 2.jpg
    NDIZI 2.jpg
    64.3 KB · Views: 45
Unadhani sijui kuwa mi dhambi mkuu? Naelewa ila ndiohivyo nimenaswa, naweza kusema nimeacha then baada ya mwezi unajikuta kulekule.

Nimepokea pongezi zako mkuu, asante.
Mkuu chaka gani kwa sasa naweza kwenda kuwekeza kwenye mgahawa?
 
Mkuu chaka gani kwa sasa naweza kwenda kuwekeza kwenye mgahawa?
Ukienda sehemu moja panaitwa KAKOLA kijiji cha Nyamishega huku utauza sana tu, maana kuna machimbo yameibuka hivyo watu wa dutwa wamekimbilia huko
 
Ukienda sehemu moja panaitwa KAKOLA kijiji cha Nyamishega huku utauza sana tu, maana kuna machimbo yameibuka hivyo watu wa dutwa wamekimbilia huko
Asante sana ila napenda kufahamu yana mda gani tangu yaibuke,naanisha naweza kwenda too late pengine,Asante!
 
Asante sana ila napenda kufahamu yana mda gani tangu yaibuke,naanisha naweza kwenda too late pengine,Asante!
Yes kuna machimbo huibuka na kuisha lakini si ndani ya muda mfupi hivyo kama wengi wanavyofikiri, huwa yanakaa hata for two years kwahiyo ukiwa mjanja unatengeneza pesa nzuri tu.

Sasa yale yamevuma sana mwezi wa 4 na dhahabu ni nyingi, kwahiyo hujachelewa mkuu. Kule watu ni wengi kuliko unavyofikiri na kuuza ni lazima kwasababu mnakuwa mbali na mji hivyo huduma nyingi watu lazima wazipate hapohapo.
 
Yes kuna machimbo huibuka na kuisha lakini si ndani ya muda mfupi hivyo kama wengi wanavyofikiri, huwa yanakaa hata for two years kwahiyo ukiwa mjanja unatengeneza pesa nzuri tu.

Sasa yale yamevuma sana mwezi wa 4 na dhahabu ni nyingi, kwahiyo hujachelewa mkuu. Kule watu ni wengi kuliko unavyofikiri na kuuza ni lazima kwasababu mnakuwa mbali na mji hivyo huduma nyingi watu lazima wazipate hapohapo.
Asante sana mkuu...ndani ya week hii nitafika huko,nitakupa mrejesho.
 
Daah mkuu mwenyw nataman kuanzisha biashar hii ya mgahaw kweny chuo flan hv maan kusoma bila kujishughurisha uongoo lakn kalee ka moyo ka kuanzaa ndoo changamot
 
Hongera sana mkuu, but sorry hiyo tiba ya mganga kwa namna yoyote ilihusisha kuwawekea wateja kitu/dawa yoyote kwenye chakula ili wazidi kuongezeka labda? Ama alikutibu vipi?. Unahisi kweli baada ya tiba mganga ndiyo ukaanza kupata pesa zaidi? Siyo kwamba kuna kitu ulijirekebisha ulipokua ukikosea mwanzo mfano, proper records management, both cash in and out? Ili kujua ulikua unaspend zaidi ya kinachoingia au pia uliboresha huduma zaidi ikapelekea wateja kumiminika?🤔

Hongera sana.
Nyie endeleeni kuongea kisomi!! in reality ni lazima uwacheki sangoma ili kuepusha vikwazo na kusonga front
 
Mimi sijawahi kwenda kwa mganga na biashara zinaenda vizuri na kuna wakati nilizidiwa na wateja kwa kuwa walikuwa wengi kama nyuki

Hilo la kutopokea hela keshi au mkononi nitalifuatilia kuona kama lina ukweli.

Ila kuhusu kufanikiwa nilishafanikiwa siku nyingi na sikutumia mganga mpaka leo sina wazo la mganga

Biashara ni matangazo na ubunifu, hayo ya mganga bado sana kwangu

Pia tangu nizaliwe sijawahi kubet au kushiriki mchezo wowote wa bahati nasibu
Comment za hivi zinanipaga moyo sana.
 
Namlaani sana aliyenifundisha kubeti maana nimeshindwa kuacha na imekuwa sehemu ya maisha, kuna muda unasema umeacha ila baada ya miezi kadhaa narudi kulekule.
Siku moja moja sio mbaya, ni kwa hamu tu.
 
Natamani nikueleze kwa upana ila sijui niazlnzie wapi, kiufupi pamoja na uzoefu wangu katika biashara, elimu na umakini wangu ilifikia hatua nikataka kukata tamaa.

Kwenye biashara kuna mambo mengi mkuu, hivyo ni vyema kuchagua upande mmoja kati ya mbili kisha ushikamane nao haswa. Muombe Mungu bila unafiki ikiwa mengine huwezi kuliko kuishi bila kujua unasimamia wapi, vinginevyo utakuwa msindikizaji siku zote.

Kwanini hukuchagua upande wa Mungu ukasimama nao sawasawa ila ukaona huwezi kutoboa mpaka sangoma ahusike, ningependa kufahamu tafadhali
 
Back
Top Bottom