Hilo la kupotea kwa cash nimelisikia kwa wafanyabiashara wengine pia baada ya kuuliza, pengine wapo humu pia labda.
Ni sawa mkuu, mimi nimejaribu kuelezea uzoefu wangu juu ya huo mradi bila kuficha kitu na hakuna sehemu ambayo nimejaribu kushawishi watu kupita njia zangu. Hata mimi sikuwahi kufikiria katika biashara nyingine zote nilizowahi kufanya, pengine labda mazingira ya unapofanya nayo yana athari zake. Huenda Bariadi ikawa ni tofauti na huko uliko.
Mwisho wa siku tunaangalia namna ya kufika point fulani, njia zinaweza kutofautiana.