Nilivyokuwa najiona mjanja, nikaishia kutapeliwa Milioni 42

Nilivyokuwa najiona mjanja, nikaishia kutapeliwa Milioni 42

Pesa inatengenezwa pale ambapo wengine hawawezi kudhani inawezekana.

Hivi unadhani kwa akili ya kawaida tu ile over invoice ya ATCL kwenye uhalisia wa kawaida unaweza kudhani mtu/watu anaweza/wanaweza kuyafanya yale??

Nimeona hoja yako hapo juu labda nisaidie kumjibia mleta uzi.

2. Hiyo miaka ya 2010 alivyokuwa anauza Ipad kama wali ulikuwa 1,000 tena chuoni, unashindwaje kuamini miaka 7 au 8 nyuma wali kuwa 200 kwenye canteen za shule za sekondari??

4. Mimi nimesoma Private School, tena hapahapa Dar yenye kila aina ya usimamizi na nidhamu. Lakini nilifanya biashara ya kuuza pipi (Ivory) na vyakula kama Sambusa na Chipsi kwa miaka mitatu kuanzia Form Two mpaka Form Four bila hata kushtukiwa. Ile shule ilikuwa ukiruka tu ukuta uingie mtaani wale wa mtaani iwe raia au hata walinzi wa shule wakikukamata na wakakupeleka shuleni wanalipwa laki moja cash (kwa kulisema hili nadhani waliosoma ile shule kama wapo hapa watakuwa wameijua) ila kwa mazingira hayohayo magumu mimi na biashara yangu ilisurvive kwa miaka mitatu na ilikuwa lazima hii mizigo ifuatwe nje na ije kuuzwa shuleni. Kuna mbinu nyingi sana nilikuwa natumia, nilinunua viongozi wa dormitories pamoja na maprefects ikiwemo Head Boy, nilijenga urafiki na Patrons ingawa hawakujua ninachofanya. Nilifanya hivyo makusudi ili wale spies directly wasiweze kuwa threat kwangu sababu walijua wakienda either kwa maprefects au Patrons kunichongea lazima habari zitanifikia. So kwa upande wa jamaa tena shule za serikali ambazo walimu wapo busy na mambo yao sidhani kama inashindikana jamaa alichokifanya.

Kitu kinachotenganisha utajiri na umaskini ni UTHUBUTU tu. Maskini wamekariri njia rahisi na salama kupata pesa ila matajiri ni tofauti. Maskini ni muoga, anaogopa kupoteza alichonacho, tajiri yeye plan yake anaangalia atachopata kwanza sio alichonacho mkononi.​
Hii comment nimetamami kulipa like tano.. umetisha Sana
 
Umesema kipindi hicho ilikuwa sahani ya wali unanunua 200, so 5k ya kipindi hicho ni kama 50k ya sasa

Halafu unamkopesha mtu elfu 5 (50k ya sasa) wakawa wanakulipa 15k (150k ya sasa) na biashara ikawa kubwa?

Yaani hapa ndipo nilipoishia kusoma hii story, hii ni chai ambayo haina sukari,.😂😂😂 Hiyo biashara ungefilisika baada ya muhula mmoja tu
Naongea haya kwa sababu nina experience na biashara ya kukopesha pia

Ukikoesha watu hela tena kwa riba kubwa bila kuwa na dhamana inayoweza kuuzwa kirahisi hapo jiandikishie kufilisika


Haya mnaoamini hii ni kweli nitoleeni povu
😂😂, hii bei ya Wali sh 200 ni miaka ya 90,labda kukopesha kaanza akiwa chuo kikuu, miaka ya 2000
 
JF kuna wajuaji sana si kila kitu lazima uelewe au ukipinge wanaosema ni chai sijui uji waambie watuelezee hustlin zao wengine wapo hapa JF hawajawahi hata kurisk laki moja wala hawajui biashara ni nini me nlishawahi poteza mill 24 kwenye kangomba na nilipoteza kizembe sana, kwahiyo naelewa achana nao hawa wakatisha tamaa.
KANGOMBA[emoji16]UMENIKUMBUSHA MBALI SANA
 
Mkuu sijui kama umemsoma vizuri huyo jamaa.. Amesema kabisa alikuwa anaangalia wa kuwakopesha na kiasi nadhani pia alikuwa anazingatia. Amesema kabisa wale mbavu mbavu alikuwa hawapi hata wafanyaje, wale familia duni pia alikuwa hawapi. Nadhani alikuwa anaangalia sehemu ya kupeleka hela yake ambayo alikuwa na hakika itarudi. The guy was smart na hicho ndicho kinachofanya wengine wawe matajiri na wengine maskini, UTHUBUTU WA KUFANYA YALE WENGINE WANAHISI HAWAYEZEKANI AU MAGUMU.
Nilichogundua watu wengi humu.

1;Wanauwezo wa kusoma ,ila hawana uwezo wa kufikiria.


2;Watu wengi humu hawana uwezo wa kuchanganua mambo.


3;Watu wengi humu hawana uwezo wa kuweka kumbukumbu kutoka Aya Moja kwenda Aya nyingine.


4;Kwa kifupi jamaa ameandika vizuri sana,ila humu kumejaa mambumbu.Tukatae tukibali humu watu wamejaliwa kusoma na kuandika ila uwezo wao wa fikra ni mdogo.
 
Umesema kipindi hicho ilikuwa sahani ya wali unanunua 200, so 5k ya kipindi hicho ni kama 50k ya sasa

Halafu unamkopesha mtu elfu 5 (50k ya sasa) wakawa wanakulipa 15k (150k ya sasa) na biashara ikawa kubwa?

Yaani hapa ndipo nilipoishia kusoma hii story, hii ni chai ambayo haina sukari,.[emoji23][emoji23][emoji23] Hiyo biashara ungefilisika baada ya muhula mmoja tu
Naongea haya kwa sababu nina experience na biashara ya kukopesha pia

Ukikoesha watu hela tena kwa riba kubwa bila kuwa na dhamana inayoweza kuuzwa kirahisi hapo jiandikishie kufilisika


Haya mnaoamini hii ni kweli nitoleeni povu
Hapana kishule shule mbona hio riba yake ni ndogo. Watoto wa mama wakiishiwa tulifaidi sana hela zao kwa riba kubwa kabsa. Enzi hizo unasema home umepasua bubsen burner inauzwa 90'000. Mshua anakupa kiroho safi. Enzi hizo tunaandaa barua za kuongeza ada au michango isio na kichwa wala miguu; ilimradi tuonekane ma Don
 
Kwa mamlaka niliyojipa ninautangazia umma kuwa huu uzi ni chai... tuusome kwa kujifurahisha tu hakuna uhalisia wowote hapa.

1. Form one alienda akiwa hajui kama shule haina wanafunzi wa kike. Wasichana kutokuwa admitted ni badiliko kubwa sana ambalo huwa sio la siri. Chai no. 1
2. Chakula Tsh 200 canteen. Kama alisoma wakati wa iPad zinatoka ni kwamba sio miaka mingi iliyopita. Kukadiria ni kama 2010 kuendelea. Vyuoni misosi ilikua Tsh 1000 na zaidi. Hakukuwa na uwezekano upate kwa Tsh 200 wali maharage hata kwa shule za sekondari. Au ilikuwa ni Ihefu sec school? Chai no.2
3. Biashara ya mkopo kwenda smoothly bila mgogoro wowote ni Chai no.3 kwenye biashara ya mikopo lazima watokee wasumbufu. Labda kama wateja ni malaika.
4. Kumiliki simu 4 maalum kwa kutazama porn shuleni ni Chai no.4 hii isingeweza kuwa siri kwa vyovyote vile lazima lingemfikia mwalimu wa nidhamu. Katika wanafunzi kuna wenye maadili wasingelifumbia macho. Kuna wenye wivu na pesa unazopiga wasingekaa kimya. Kimsingi hustles za ndugu mwandishi wakati wa secondary zimetawaliwa na chai.

Kwa hustles za Chuo sina tatizo nazo maana angalau zinawezekana.
Mbona mimi nilikuwa nauza viroba na kupima konyagi shuleni na hadi namaliza hakuna mwalimu yoyote aliefahamu. Na simu tulizimiliki sana. Wanafunzi kwenye jambo lenye maslahi ya wengi watakulinda kama roho ili huduma/faraja yao isipotee. Ndio maana akasema alipotishia kusitisha biashara ya kukodisha simu kwa ajili ya porn; wanafunzi wenyewe walianza upelelezi uliopelekea mpaka kupatikana kwa simu bila ya mhusika kutumia mabavu yoyote yale. Nro hujasoma boarding nini ukaona vituko?
 
Mkuu ilikuwa hatari!!jamaa alichonifanyia kipindi kile sukari ya kutumia nusu mwezi mtu unamuwekea kwenye kopo moja tu,na bado anakwambia nasikia kwa mbali!!ule ulikuwa ni UGAIDI!!!
Shule ina kuwa kama kambi ya watalibani!!na ole wako ukashitaki jamaa atakuwa suspended lakini haliendi kwao linabakia kijijini hapo usiku linakuja linakuvunja mguu,au kiuno,ndio linaenda kwao!!!mzee mmoja alimleta mtoto wake akawa amefika jioni sana hivyo ikabidi apewe sehemu alale na mwanaye hadi kesho ndipo zoezi la kupokelewa lifanyike!!bnana usiku mtoto ,baba walitembezewa kichapo!!kesho mzee akaairisha kimuachq mtoto wake akaondoka naye akasema hii sio shule!!!eti Mungu anamakusudi yeke hili kutokea,kumbe "mwanangu alikuwa anaenda kufa"
Kipindi kile mtu akipewa suspension alikuwa haendi kwao,anaishia kukaa maporini na usiku anarudi dom kulala na notice anaandika kama kawa,ikiisha anamnunua mwana nzengo wanaenda nae shule ana act ndio mzazi wake,

Ilikuwa ukianzisha ubaya na jamaa kama huyo shule utaiona chungu,bording school za zamani ilikuwa ni balaa,ukitoka huko wewe ni mwanaume tosha kabisa
 
Back
Top Bottom