Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaendelea au ndo imeisha mzee wangu???
Mmeanza aandike ndefu unadhani ana kazi ya kukuandikia wewe tu hana kazi nyingine nyie ndio wale tuma na ya kutoleaMkuu jaribu kuandika ndefu kidogo
Kama Kuna mtu anauza popcorn humu naomba za 2mil.
Maana hii habari itakua🔥View attachment 1755780
Karibu huku Bulwa tulime iliki.Ngoja nipaki nguo kwenye begi, nami nitafute pa kwenda.....
Unatuandikia stori kama vile unamtumia demu text vile..fupi fupi..
Mkuu fanya kuandika aisee..page hata moja bado ila stori tayari ina episodes tano.
Sent using Jamii Forums mobile app
andika story ndefu basi....hivi vipisi vinaboa mkuuSEHEMU YA SITA
Ile Asubuhi kabla ya Safari kuanza, Kuna wadogo zetu kama 4 wa umri kama wa Miaka 16/17/18 walipanda ndani ya Bus. Waliomba kwa Konda kuongea na Abiria. Walituambia kuwa na wao wanaelekea South Afrika ila nauli zao ziliishia pale Tunduma. Waliomba tuwachangie Nauli.
Wametokea Dar ila wamekaa pale Tunduma kwa muda wa wiki nzima wakitafuta nauli ya kuendelea na safari. Kwa hiyo walikuwa wanaomba tuwachangie nauli ili waweze kuendelea na safari. Tulianza kuwachangia, Mmoja wao alikuwa na simu akaiuza mle ndani ya Bus. Madogo walikuwa wamechangamka sana. Mpaka wanakwenda South kwa nauli za kuunga unga. Wenyewe kutumia Mwezi mzima njiani ni kawaida tu.
Akiba waliyokuwa nayo, pamoja na Michango yetu waliweza kupata nauli ya kuwafikisha mpaka Harare. Walisema wakifika Harare watakaa tena wiki nzima wakitafuta nauli ya kuendelea na safari. Hivyo tuliendelea nao na safari kwenye bus letu. Kwa kifupi mbele ya safari katika kupiga piga nao story tulikuja kujua kwamba kati ya wale madogo, mmoja wao ndio kiongozi wao, yeye alishawai kuishi sana South Afrika. Ilionekana kila akirudi kwao Manzese Tanzania, wakati wa kuondoka huwa anachukua Vijana wengine anaenda nao South. Yani kwa zile story za Madogo nilijiona kumbe ni mim tu ndo sijafika South Africa, Kwa maelezo yao ni kama vile Vijana wengi wapo huko tayari.
Ni kweli kwa pilikapilika za Vijana niliowaona pale Tunduma niliona ni kama Vijana wengi sana wanaikimbia hii nchi, kila mmoja akilalamika kuwa Bongo Maisha magumu.
Staili ya hawa madogo kusafiri ni ya kuunga unga nauli, hawa madogo walivyofika Tunduma walikaa hapo, sidhani kama Kuna namna nyengine walifanya ili kupata nauli zaidi ya wizi. Na wapo madogo wengine wengi wa staili hii.
Pia pale Tunduma sio Waburundi wote walifanikiwa kupita, kuna baadhi walikosa pesa ya kulipia Visa ya kuingia Zambia. Sisi watanzania tunaingia Zambia bila kulipia Visa. Hivyo waburundi ndani ya Bus walipungua
Kila tulivyokuwa tukiendelea na Safari ndivyo Lugha yetu pendwa ya Kiswahili ilivyokuwa ikipotea. Tulifika Lusaka Mji Mkuu wa Zambia saa tatu usiku. Tulilala hapo. Wengine tulishuka kwenda kupata Huduma za Chooni, Wengine ndo ilikuwa mwisho wa safari yao. Asubuhi kulivyokucha tuliendelea na safari yetu ya kuelekea boda ya Zambia na Zimbabwe inaitwa CHIRUNDU
Khumbu ilikuwa kali kisa kulikuwa na kunjunjana mwanzo mwisho.Story itakuwa hot kama ya khumbu na konda msafi...ishajionyesha mkuu usikatikie tu hewani hewala hewala mkuu...
We nenda hapo darfur Sudan[emoji1787]Ngoja nipaki nguo kwenye begi, nami nitafute pa kwenda.....