Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Kuna mikasi humu kwenye stori yako mkuu???😂😂
Na matako ya kuning'inia??? Nataka kuweka kambi
 
Mkuu mimi nipo curious kujua hiyo hela ya kuweka akiba bank na nauli ulipataje kwakuwa umesema ulikuwa huna ajira na hali ya maisha ilikuwa ngumu kwako.

kila mtu ana benchmarks zake anaposema jambo. Like weweunaweza sema leo huna hela Same time una elfu 50 kwenye wallet. nahii inakua defined na uchumi wako.

Jamaa huenda ana uwezo wa kukusanya milionmoja but anahitaji milion100
 
kila mtu ana benchmarks zake anaposema jambo. Like weweunaweza sema leo huna hela Same time una elfu 50 kwenye wallet. nahii inakua defined na uchumi wako.

Jamaa huenda ana uwezo wa kukusanya milionmoja but anahitaji milion100
Sure Mzee kuna watu wakisema hawana pesa it doesn’t mean kwamba hana kabisa ila pesa alizonazo hamzitoshi kwa malengo yake aliyojipangia.
 
SEHEMU YA TATU

Nikafanya research kidogo nikaambiwa Benki inayopatikana kwa urahisi huko South afrika ni First National Bank (FNB), Kwa hapa Dar es Salaam hii Bank ilikuwa na Tawi lake Posta. Nikaenda mpaka Posta, Nikafungua Account, Nikaweka Akiba Kama ya Milioni Moja. Huyo Nikasepa zangu na ATM Card yangu. Niliona ni Salama zaidi kwenye hii Safari kutembea na ATM Card mfukoni kuliko kutembea na Million Moja Mfukoni ukizingatia safari yenyewe ni ndefu na niendako sipajui na wala simjui mtu.

Siku ya Safari ikawadia, Huyo mpaka Ubungo. Ukweli ile hofu ya kwenda mahali nisipopajua, na sina Rafiki wala ndugu ilinitawala sana, sema nilikuwa nimechoka sana kuishi Bongo mpaka nikasema liwalo na Liwe. Unajua katika maisha kuna wakati mtu unachoka kuishi sehemu moja, kupiga story zile zile kila siku na watu wale wale.

Hivyo safari ya kutoka Ubungo kuelekea South Africa ikaanza. Kwenye Bus Watanzania tulikuwa kama nusu ya Bus zima, Abiria waliobaki walikuwa Wakenya, Waburundi walikuwa wengi, wanawake kwa wanaume. Pia kulikuwa na Wazambia na Waangola waliokuwa wakirudi Makwao.

Ukweli kabla ya Safari hii, Sikujua kama pale Ubungo huwa kunapokea wageni wengi kiasi hichi. Sikujua kama Tanzania ni njia kubwa sana ya kuelekea kusini mwa Bara la Africa. Sikujua kama tunapokea Waburundi wengi hivi, Kila kitu kilikuwa kigeni kwangu.
Hizi stori za hv nazisomaga kwa Makin Sana Kama nipo chumba Cha mtihani.

Zinanivutiaga Sana.
.Nawew ndo utupe nzima nzima Sas sio nusu nusu
 
Back
Top Bottom