Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Hii story inazidi ya khumbu kwa sababu hii story ya kiume yaani kwenda nchi ya watu bila saport yeyote pesa yake ndio ndg yake,konda msafi alikua na sapoti kubwa jamaa zake wauza ngada walimpa mpka matumizi na nyumba Sasa huyu mwamba ni jeshi la mtu mmoja
 
Hii story inazidi ya khumbu kwa sababu hii story ya kiume yaani kwenda nchi ya watu bila saport yeyote pesa yake ndio ndg yake,konda msafi alikua na sapoti kubwa jamaa zake wauza ngada walimpa mpka matumizi na nyumba Sasa huyu mwamba ni jeshi la mtu mmoja
Kazi ya Konda Msafi ikawa ni kupaka tu vumbi la kongo na kuosha mbupu huku akimsubiria mtoto Khumbu aibuke ajigegedee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole, najifunza sana habari hii. Japo nilisafiri majuu bila misukosuko kama hii yako lkn naona kweli bongo maisha ni kupambana. Ulaya ni mteremko sana. Nilikwenda mwenyewe kwa ramani tu.

Wakuu naanza kusoma michango dada yenu. Story tamu jamaa nitag, ukitaka nihagi..lkn usiniduuu
 
Story teller chungu cha sita kimeenda wima nini hebu tiririka basi
 
SEHEMU YA SABA

Tulifika pale CHIRUNDU nikiwa makini sana yasije yale ya Tunduma yakajirudia. Nilikuwa naogopa sana kutumia pesa nyingi kwa sababu nilikua sijui niendapo.

Kuna swali kuna mdau ameniuliza naomba nilitolee ufafanuzi, ameniuliza kama Bongo nilikuwa sina ajira nilipata wapi hiyo pesa Milioni Moja ya kuweka Akiba Banki. Ni hivi hapo Kabla kuna Ofisi nilikuwa nafanyia Kazi, kuna wafanyakazi tulipunguzwa ndipo nikaanza kufatilia mafao yangu pale GEPF. Mafao yangu hayakuwa makubwa sana ndo nilitumia kwenye hii Safari.

Sasa tuendelee, Pale Chirundu nilipanga foleni hadi kwa Afisa Uhamiaji, Swali langu kichwani likiwa moja tu, Je niweke hela kidogo katikati ya Passport kama nilivyofanya Tunduma? Uzuri hapa hapakuwa na Vishoka wengi kama Tunduma. Yule Dada Matilda ambae ni Abiria mwenzangu tulishaanza kuzoeana kidogo, kumbuka yeye alikuwa ni mzoefu wa hii njia, alinifuata akaniambia mdogo angu sio kila sehemu unakimbilia kuweka hela, soma kwanza upepo. Ukiwa na mazoea ya kuweka hela kila boda utaishiwa utafika South bila hela. Nikamwambia basi Dada tangulia, Mimi nitapanga foleni nyuma yako. Akasema sawa.

Tulifanikiwa kugongewa Mihuri bila kutoa pesa Ila kwa tabu sana maana maswali yalikuwa mengi, Mara kuna karatasi walinipa nijaze, niandike taarifa zangu, Kama Passport Namba, Mahali ninapokwenda, Namba za Bus nililopanda na maelezo mengine. Utaratibu huu wa kupewa karatasi tulipewa wengi. Lakini mwisho wa siku tulikomaa hatukutoa hela.

Tulifanikiwa kuingia nchi ya Zimbabwe mpaka Harare.Tulifika Harare kwenye kama saa kumi na moja jioni. Pale Harare ilikuwa ni stand ndogo, sio kubwa kama Ubungo lakini ilikuwa na Mabus mazuri sana. Tulikuta kuna wapiga debe kibao wa Mabus hayo ambao ni Wabongo, kwa hiyo tulivyoshuka tu kwenye Bus walitukimbilia na kutupa Msaada wa kupata Bus la South.

Pale tulitawanyika kwenye mabasi mbalimbali, kwenye bus nililopanda Mimi tulikuwa wabongo 4 tu, Nilikuwa Mimi , Ahamad, Matlida na Jamaa mwengine. Ndani ya Bus wengi walikuwa ni abiria wa pale Zimbabwe na Zambia. Ndani ya Bus Kiswahili ndo kilipotea kabisa. Hata Matangazo ya ndani ya Bus yalitolewa kwa lugha zao za pale Zimbabwe.

Nakumbuka tukiwa tumeanza safari, tunatoka pale Stand, niliwaona wale madogo wakiingia mtaani utafikiri ni wenyeji vile. Ukweli nilijifunza kitu kutoka kwa wale madogo, walikuwa majasiri mno.

Hatimae usiku wa saa Tisa, tulifika Boda ya Mwisho ya BeitBridge, Nadhan ndio Boda kubwa ukanda wetu wa chini mwa jangwa la Sahara. Palikuwa busy balaa, watu kibao.

Nilivyoona watu wengi vile, kitu cha kwanza nilichojisemea moyoni ni kwamba "Muda huu Mimi huwa nimelala kumbe kuna sehemu nyengine hapa duniani muda huu watu wapo busy hivi"

Kulikuwa na watu mataifa mbalimbal, Weupe na Weusi. Sasa wabongo tukawa kama ndugu tayari. Ukweli moyoni nilikuwa siwaamini sana hawa jamaa maana nilishawai kusikia South Afrika, Wabongo kwa wabongo ndo hatari kuliko hata wageni. Lakini nikasema No sweti maji nishayavulia nguo. Kama wakitaka kuniibia au kunifanya jambo baya poa tu. Hata Matlida mara nyingi alikuwa ananihimiza dogo usiwaamini sana wabongo watakuliza. Basi muda wote nilikuwa makini.

Tulipanga foleni kwenye Ofisi za Uhamiaji, yule jamaa mwengine alisema tukitaka South Africa tupewe siku nyingi za kuishi humo, hapo ni Lazima katikati ya Passport tuweke hela.

Alisema tusipoweka hela basi tutapewa siku chache sana. Huyo jamaa, Ahamad na Matlida wakawa wanabishana pale, Matlida anasema tusiweke, yule jamaa anasema lazima tuweke la sivyo tutapewa siku chache mno.

Matlida anasema hata tukipewa siku chache sio mbaya maana lengo tufike kwanza, tukishafika hayo mengine tutajua huko ndani namna ya kuongezewa muda.

Mwisho wa mabishano tukakubaliana tuweke pesa, ila kwenye foleni yule jamaa ndo asimame mbele yetu, yaani awe wa kwanza. Mimi nilisimama nyuma yake. Matlida akasimama nyuma yangu, Ahamad akasimama nyuma ya Matlida. Foleni yetu ilivyofika Kaunta. Mara nikashangaa yule Askari wa Uhamiaji wa pale Kaunta anamuita Askari mwenzie aje kumkamata yule jamaa etu kwa kosa la kutoa rushwa. Ukweli nilitetemeka kishenzi, fasta sana nilitoa pesa niliyoiweka katikati ya Passport yangu kisha nikasogea pale Kaunta. Yule Mzungu Mkaburu akawa ananiangalia tu.
 
Back
Top Bottom