Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Wakuu leo naomba kuleta Story yangu ya kweli ya jinsi nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu kule wala mtu wa kunipokea.

Ukweli kuna wakati ilifika nilichoka sana maisha ya hapa nyumbani, ilikuwa Mwaka 2014, nilikuwa napitia changamoto nyingi za maisha hasa katika familia. Ukweli akili ilikuwa imechoka sana ilisababishwa na kutokuwa na ajira muda mrefu.

Hata baadhi ya watu sikuwa napenda kukutana nao sana. Nikajiuliza kwani Maisha ni hapa tu nyumbani? kwani hakuna sehemu nyengine? Nikajisemea labda sikuandikiwa kutoboa hapa nyumbani ngoja nikajaribu bahati yangu sehemu nyengine.

Kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda South Africa, Kwanza niliwaza kujaribu bahati yangu Marekani, nina ndugu kama watatu huko. Nikamcheki ndugu yangu mmoja akanitumia Invitation Letter. Nikaanza kupambana pale Ubalozini. Nilifika kwenye Usahili lakini nilikosa VISA.

SWALI; Ulimuaga Paul Makonda???
 
Daaaah aisee halafu na South Africa na sikia kufa ni suala la kawaida sana japo popote una weza kufariki lakini kwa SA, nasikia una weza ukawahishwa muda wowote.
Mdau kama umezoea maisha ya amani Tanzania.Kwa Africa Kusini utaishi kwa uoga uoga,kwa matukio either utakayaona au kuyasikia kwenye vyombo vya habari.Kule usalama ni changamoto
 
Huyu kachanganya story ya KUMBU na KANYA. Sio bure
Kumbu mtoto wa kizulu mwenye umbo mpwito mpwito hizi stori za south africa nazipenda sana. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119]
 
Nani amekwambia hawakubaliki???....mfukoni wako vizuri

Wewe ambaye ukienda "unakubalika"..... Umefaidika nini??

Umasikini wa Naijeria na Huku kwetu wapi kuna nafuu???

Unajua ni hela kiasi gani zinaingia Nigeria kutoka kwa Diaspora?? Ambazo zinasaidia jamii yao??

Hayo mawazo ya kutaka " kukubalika" ndio utopolo tuliojazwa toka tunakua yani mpaka saivi vijana wanahangaika wazazi wanataka wote waajiriwe serikalini( SU-Soma Ule/Shirika la umma) matokeo yake vijana wamebaki kuwa na stress tu. Kasomesha mtoto na hana msaada mzazi kastaafu halafu mtoto anashindwa hata kumsaidia utaleta "kukubalika" kwenye kikao cha familia kumchangia mshua Aende Apollo India matibabu??

Kuna siku nilikua na demu mmoja wa Kiswana kutoka sauzi nikaanza kuongea huo utopolo wa Nyerere kaisaidia South Afrika nikitaka "nikubalike" wakati huyo dada hata Nyerere hamjui wala Tanzania haijui ananishangaa tu na "kukubalika" kwangu kwamba waafrika kusini ndugu zetu😂😂

Matatizo ya Ujamaa hayo......dunia hii ni yq ubepari fanya vyovyote kuwa na hela utakubalika tu. Unadhani tunawapenda sana Wazungu??? Madola wanayoyaleta ndo "tunawakubali"

Badilisheni mindsets hizo,kuweni na uthubutu
kweli kabisa, lazima tubadili mindset.
 
Bado nipo hai mkuu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji117] kaka nilipatwa na huzuni sana, pamoja na kuwa sikufahamu kumbe upo kaka. Habari za wapi mkuu maana ni kama vile ume fufuka sija wahi kukuona kwenye jukwaa lolote humu. Pia naomba umalizie story yako kaka, story ni ya kuvuti sana .

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom