Nilivyomkomesha tapeli wa viwanja Kivule Dar es Salaam

Nilivyomkomesha tapeli wa viwanja Kivule Dar es Salaam

Hi
NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE

Habari zenu wadau wa JF!

Leo nami nimeonelea niwasimulie kisa changu jinsi nilivyomkomesha tapeli maarufu wa viwanja maeneo ya Kivule ajulikanaye kama Juma Kasangu,mnamo mwaka 2014 mwanzoni nikiwa katika harakati zangu za kutaka kujipatia eneo nikamshirikisha rafiki yangu mmoja ambaye yeye alishakuwa na eneo kule Kivule maarufu kama kwa mama Anna Mkapa

Huyu jamaa yangu alishaanza na ujenzi akawa ameshaweka msingi ila kutokana na changamoto za kiuchumi akawa ameliacha kwanza avute nguvu ndipo nami baada ya kumueleza tamanio langu naye akanipeleka nikapaone eneo analojenga nami baada ya kufika kiukweli nikapapenda sana kwanza pako tambarare, mazingira rafiki, mji ulikuwa umepangiliwa kwani Serikali ya mtaa ilichora njia kabisa na walikuwa wakali hadi kufikia kupita mara kwa mara kwenye maeneo ya ujenzi kuhakikisha hakuna anayejenga kiholela, mpangilio wa mitaa ulitiliwa mkazo sana, hizo ni mojawapo wa sifa kuu zilizopelekea kupapenda eneo lile.

Sasa kwakuwa huyu jamaa yangu alinunua eneo kutoka kwa huyu Juma Kasangu nami akaniunganishia kwake ili niweze kupata eneo maeneo karibu na eneo la kwake,(waweza kushangaa imekuwaje nimpe sifa ya utapeli wakati aliyenipeleka nae aliuziwa eneo na huyo huyo tapeli😂😂)

Kiukweli huyu Kasangu ni mbwa miongoni mwa mambwa koko wakubwa sana kiukweli sijui hatima yangu na namuomba sana Mungu anijaalie mwisho mwema ila huyu jamaa ana mzigo mzito sana kesho mbele ya muumba wake kama hajajirekebisha (sina uhakika kama bado yuko hai).

Huyu jamaa yangu nae wakati wa kimbembe changu ndipo akaja kupewa mkanda wake ponapona yake ilikuwaje hadi kutofikia kutapeliwa, kumbe kilichomuokoa ni kuwahi kuanza kujenga lile eneo kwani kumbe pale alipouziwa jamaa yangu mwenye eneo ni baba mkwe wake Kasangu (baba wa mkewe) na walipoona pameshaanzwa ujenzi ikabidi wakamalizane kiukwe na kutoyatoa hadharani (naamini hata huyo baba mkwe hakupewa chochote)

Turudi sasa katika sakata langu, siku hiyo mimi na jamaa yangu na ndugu yangu mwingine baada ya kumpanga bwana Kasangu, Jumamosi moja tukatoka makwetu wakati huo mimi nakaa Ilala Sharifu Shamba na wenzangu walikuwa wanatokea maeneo ya Ilala sokoni (kiuzawa mimi nimezaliwa maeneo ya Ilala sokoni) tukaelekea eneo la tukio kwa kupanda gari hadi Banana pale tukapanda hadi Kivule napo tukatembea mdogo mdogo kwenda huko kwa mama Mkapa (kulikuwa hakuna vigari wakati huo ni bodaboda tena hazikuwa kihivyo kuna mchanga sana ila nasikia siku hizi daladala zinafika)

Kasangu akaja na vijana wake wawili (Kasangu kikabila ni mnyamwezi)hao vijana walikuwa ni wakurya nao ni Marwa na mwingine sikuwa nimemtambua kwa jina vizuri maana ni siku hiyo tu sikumuona tena wakati wote wa sakata hili

Marwa nilimtambua kwakuwa uko mbele pia nilipata msaada wake, sasa tukafika eneo la tukio na akatuonesha viwanja vitatu ambavyo viko kama mita 120-150 kutoka eneo ambalo jamaa yangu ameuziwa, tukavikagua na mwishowe nikakichagua cha kukichagua na ikafika muda wa kufanya malipo na yule mtu aliyekuja nae pamoja na Marwa alinitambulisha kama mjumbe wa eneo lile kwani pia alikuwa na mihuri kabisa na mauzo yalikuwa ni 1,200,000/= (mauzo yote yalikuwa ni 1,500,000) nikampatia pesa na mashahidi wakaweka saini zao na nikamtaka lazima twende Serikali ya mtaa kukamilisha makubaliano ndio nimmalizie hiyo 300,000 yake

Tukatoka eneo la tukio salama na jamaa yangu akanisisitiza kuanza ujenzi japo msingi wa vyumba viwili kwani jambo la moto unalifanya na moto wake nisipoe tena nami baada ya kama miezi minne nakumbuka nikaanza kujipanga na kuanza ujenzi (pesa yake iliyobaki nikawa nampa kidogo kidogo mara 50 mara 20)

Itaendelea...
#&++$ wewe
 
NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE

Habari zenu wadau wa JF!

Leo nami nimeonelea niwasimulie kisa changu jinsi nilivyomkomesha tapeli maarufu wa viwanja maeneo ya Kivule ajulikanaye kama Juma Kasangu,mnamo mwaka 2014 mwanzoni nikiwa katika harakati zangu za kutaka kujipatia eneo nikamshirikisha rafiki yangu mmoja ambaye yeye alishakuwa na eneo kule Kivule maarufu kama kwa mama Anna Mkapa

Huyu jamaa yangu alishaanza na ujenzi akawa ameshaweka msingi ila kutokana na changamoto za kiuchumi akawa ameliacha kwanza avute nguvu ndipo nami baada ya kumueleza tamanio langu naye akanipeleka nikapaone eneo analojenga nami baada ya kufika kiukweli nikapapenda sana kwanza pako tambarare, mazingira rafiki, mji ulikuwa umepangiliwa kwani Serikali ya mtaa ilichora njia kabisa na walikuwa wakali hadi kufikia kupita mara kwa mara kwenye maeneo ya ujenzi kuhakikisha hakuna anayejenga kiholela, mpangilio wa mitaa ulitiliwa mkazo sana, hizo ni mojawapo wa sifa kuu zilizopelekea kupapenda eneo lile.

Sasa kwakuwa huyu jamaa yangu alinunua eneo kutoka kwa huyu Juma Kasangu nami akaniunganishia kwake ili niweze kupata eneo maeneo karibu na eneo la kwake,(waweza kushangaa imekuwaje nimpe sifa ya utapeli wakati aliyenipeleka nae aliuziwa eneo na huyo huyo tapeli[emoji23][emoji23])

Kiukweli huyu Kasangu ni mbwa miongoni mwa mambwa koko wakubwa sana kiukweli sijui hatima yangu na namuomba sana Mungu anijaalie mwisho mwema ila huyu jamaa ana mzigo mzito sana kesho mbele ya muumba wake kama hajajirekebisha (sina uhakika kama bado yuko hai).

Huyu jamaa yangu nae wakati wa kimbembe changu ndipo akaja kupewa mkanda wake ponapona yake ilikuwaje hadi kutofikia kutapeliwa, kumbe kilichomuokoa ni kuwahi kuanza kujenga lile eneo kwani kumbe pale alipouziwa jamaa yangu mwenye eneo ni baba mkwe wake Kasangu (baba wa mkewe) na walipoona pameshaanzwa ujenzi ikabidi wakamalizane kiukwe na kutoyatoa hadharani (naamini hata huyo baba mkwe hakupewa chochote)

Turudi sasa katika sakata langu, siku hiyo mimi na jamaa yangu na ndugu yangu mwingine baada ya kumpanga bwana Kasangu, Jumamosi moja tukatoka makwetu wakati huo mimi nakaa Ilala Sharifu Shamba na wenzangu walikuwa wanatokea maeneo ya Ilala sokoni (kiuzawa mimi nimezaliwa maeneo ya Ilala sokoni) tukaelekea eneo la tukio kwa kupanda gari hadi Banana pale tukapanda hadi Kivule napo tukatembea mdogo mdogo kwenda huko kwa mama Mkapa (kulikuwa hakuna vigari wakati huo ni bodaboda tena hazikuwa kihivyo kuna mchanga sana ila nasikia siku hizi daladala zinafika)

Kasangu akaja na vijana wake wawili (Kasangu kikabila ni mnyamwezi)hao vijana walikuwa ni wakurya nao ni Marwa na mwingine sikuwa nimemtambua kwa jina vizuri maana ni siku hiyo tu sikumuona tena wakati wote wa sakata hili

Marwa nilimtambua kwakuwa uko mbele pia nilipata msaada wake, sasa tukafika eneo la tukio na akatuonesha viwanja vitatu ambavyo viko kama mita 120-150 kutoka eneo ambalo jamaa yangu ameuziwa, tukavikagua na mwishowe nikakichagua cha kukichagua na ikafika muda wa kufanya malipo na yule mtu aliyekuja nae pamoja na Marwa alinitambulisha kama mjumbe wa eneo lile kwani pia alikuwa na mihuri kabisa na mauzo yalikuwa ni 1,200,000/= (mauzo yote yalikuwa ni 1,500,000) nikampatia pesa na mashahidi wakaweka saini zao na nikamtaka lazima twende Serikali ya mtaa kukamilisha makubaliano ndio nimmalizie hiyo 300,000 yake

Tukatoka eneo la tukio salama na jamaa yangu akanisisitiza kuanza ujenzi japo msingi wa vyumba viwili kwani jambo la moto unalifanya na moto wake nisipoe tena nami baada ya kama miezi minne nakumbuka nikaanza kujipanga na kuanza ujenzi (pesa yake iliyobaki nikawa nampa kidogo kidogo mara 50 mara 20)

Itaendelea...
Mmmh nawew unaleta story yaani umekah ukaona uje story unadhani utaweza kuwa sawa na kina molel na umughaka

Embu fupisha uongo wako ,na Wala sijasoma upuuuz wako .nilivyoona tu itaendeleee nikajuwa hi ndegelezz vip

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE

Sehemu ya 4

USIKU WA DENI ULIPOFIKA

Ilipofika mida ya saa 10 yule bwana Chacha akiwa ameshatangulia kule Kivule na maskani yao hasa ilikuwa pale Kivule njia panda ya shule kuna kipub yule Kasangu alikuwa amekifungua na mara nyingi amekuwa akipatikana hapo ndipo bwana Chacha alipopapanga kama eneo la kufanyia tukio na sisi huku tukawa tunajipanga na nikamfata ndugu yangu flani ambaye alikuwa anafanya shughuli ya ufundi wa magari anaitwa Meddy ambaye alitutaka kuweka mafuta kwenye gari na tungekwenda sote yaani mimi,Kindamba na Meddy kuelekea Kivule,ilipofika muda wa saa 11.30 tukatoka kuelekea uko na katika majadiliano ikaonelewa mimi nishukie eneo linaloitwa Bambucha na wao wangekwenda wenyewe kupitia mwongozo wa Chacha ambaye alishakuwa tayari ameshafika kule Kivule na walipofika pale wakiwa wanawasiliana na hatimaye kukutana naKasangu wakamtaka awapeleke kwenda kutizama maeneo na kuyakagua na ikiwapendeza ndio wakae chini kujadili bei na namna gani ya kufanya malipo sasa yule Kasangu wakati wa kutakiwa hivyo akawa anataka kuwapa vijana wake ndio wawapeleke wale jamaa zangu na akawa anataka kupanda pikipiki ambayo ilikuwa imepaki pale kwenye pub yake ndipo yule Kindamba akamfata na kama aliyepatwa na machale Kasangu akashuka na kuanza kutoka mbio nasikia wakaanza kumkimbiza na akaenda kujikwaa kwenye kisiki na mguu wake mmoja ukawa umejeruhiwa na damu ikawa zinamtoka sasa yule Kindamba akawa anaact kama yeye ni askari akamwambia kimbia nikumwage ubongo na akawa anaomba msamaha na akawa anagugumia na kuka chini,wakambeba msobemsobe na wale kina Chacha wakawa wanawauliza kina Kindamba imekuwaje tena?😂 wakawaambia kuwa huyu ni tapeli na tunaondoka nae na mtaenda kujulia uko Staki shari,sasa yule Kasangu hadi anakamatwa pale hakuwa anajua amekamatwa kwa kosa alilomtendea nani kwakuwa ni mtu wa matukio sana na akawa anaumiza kichwa hawa ni wa nani niliyemtapeli? Wakamtia garini na kuelekea nae Staki shari na wakanipitia pale Bambucha sasa wakati wanasimama na mimi kupanda dah jamaa alichoka sana akajisemea moyoni kweli huu mziki niliouingia safari hii HAPATOSHI!
Nikapanda garini na akawa ananiomba sana awapigie ndugu zake kujua namna gani tunalimaliza lile shauri nje ya polisi,nikamwambia sina njia yoyote zaidi ya kutaka pesa yangu na kama anaendelea kuzingua polisi itamuhusu tena nikamwambia nataka hao matapeli wenzake salama yake walete M3 kamili ndio nimdamp sasa toka saa 1 usiku hadi saa 3.30 tumepaki gari pale ukivuka reli ya njia panda ya Segerea,ilipofika 3.30 wakiwa wenzake wawili wamekuja mmoja akijitambulisha kama mjomba wake😂 kumbe tapeli mwenzake anajifanya kutoa viapo hapo wee nikawa najiambia wewe apa miungu yako yote huyu atafika eneo la tukio kama hamtatoa pesa yangu,baada ya kuona sound zimekuwa nyingi nikamtuta yule bwana hadi Staki shari na kufika kaunta askari anaanza kunifokea mbona umemuumiza bila ya kuhoji imekuwaje (alikuwa anajuana nae akataka kunitingisha) nikamwambia muulize mwenyewe imekuwaje na Juma akamwambia alikuwa anakimbia akajikwaa ndio akaniuliza tatizo nami nikamueleza akanitaka nimpe RB# nikatoa kitochi changu cha Nokia upande wa meseji kwenye draft uwa nasave baadhi ya vitu vyangu muhimu na namba hizi nilizisave huku,nikampatia atamzungusha na kumuweka selo akanitaka nifike kesho yake asubuhi,nami nikatoka pale na nikamjuza kwa simu yule mzee Juma kuwa mtuhumiwa yupo pale na ninaondoka zangu
Asubuhi na mapema nikafika Staki shari nikamkuta yule mzee amenuna hata sikujua kwanini akawa ananambia nenda Madafu uko ukamalizane na jamaa yako (Madafu ni mahakama ya mwanzo Ukonga inayohudumia maeneo yale yote)mi nikatoka zangu nikaelekea kule mahakamani muda kama wa saa 2 hivi gari la kubeba watuhumiwa likawa limefika na nikawa nimekaa pale niko mwenyewe tu,watu wakawa wanaitwa na wenye kuachiwa kwa dhamana wanaachiwa,wenye kushinda wanaondoka na wenye kufungwa wanafungwa hadi mida ya saa 8.30 ndio tunaitwa kumbe pale utaratibu wao flesh case zote wanaziweka mwisho,njaa inaniuma ila hata kwenda kujiibia kwenda kula naogopa isije akaitwa nami sipo eneo la tukio,wakati naelekea mahakamani asubuhi kutoka Staki shari kuna mshkaji wangu mmoja yeye ni hakimu uko eneo flani mkoa wa Singida (naomba nisitaje eneo kumuhifadhi) huyu ni mshkaji wangu sana tumefanya mambo mengi ujanani ya hatari na mazuri sasa nikamvutia uzi kumpa habari kuhusiana na hii ishu akanambia bob we nenda pale hakimu mfawidhi wa pale mwanae sana wamesoma wote intake moja uko Lushoto mambo ya uhakimu nikamwambia poa Imeisha hiyooo!!
Tumekaa pale mara tukaitwa ndani katika kichumba alikuwepo hakimu na wazee wawili wakike na wa kiume ambao ni wazee wa baraza (walaaniwe wale wazee) na mdada aliyekuwa akichukua maelezo tuliyokuwa tunayatoa pale na mheshimiwa akaletewa faili na yule mdada na akatuita majina kuhakiki kama ndio kesi husika na waliopo mbele ndio wahusika wenyewe na alipojiridhisha akamsomea shtaka yule Kasangu na akakana pale na mheshimiwa akaaghilisha kesi kwa muda wa wiki 2 toka siku ile na wakati anaaghilisha palepale nikamuuliza jina lake akanitajia,kumbe ni yule yule mwanae mwanangu nikajua MBUZI KAFIA KWA MUUZA SUPU! nilijidanganya!😂

Itaendelea!
 
Mmmh nawew unaleta story yaani umekah ukaona uje story unadhani utaweza kuwa sawa na kina molel na umughaka

Embu fupisha uongo wako ,na Wala sijasoma upuuuz wako .nilivyoona tu itaendeleee nikajuwa hi ndegelezz vip

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kaa kwa kupoa wewe nakujua ni wa upinde
 
Back
Top Bottom