Nilivyonusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali miaka 15 iliyopita. Tanzania kufariki ni dakika 0 tu!

Niliwahi koswa koswa kupondwa na mawe mtaroni kisa mlevi mmoja tabata.

Nilikua nimepaki gari kipindi hiko bar inaitwa BL karibu na bar ya camp mtaa wa st. Marry. Sasa ikafika muda nikataka kusepa. Ile nataka kuondoka nikaona mtu kapaki boda nikashuka nikaenda kumwambia nataka kutoka.

Hapa na pale akatokea mwenzake kalewa. Akaanza nyie wenye magari mna dharau blaah blaah kibao. Ghafla watu wakaanza kukusanyika. Wakati nashangaa mara teke mara nipo mtaroni mtu anaita mwizi mara naona mtu kabeba bonge la jiwe anataka kulishusha kichwani. Sijui nani alimzuia yule mtu.

Baada ya hapa na pale nikaweza kuondoka ila nikamkariri yule jamaa.

Nilimripoti pahala jamaa yangu akampata. Alishughulikiwa vilivyo ila jamaa hakutaka kunionyesha anaishi wapi.

Mpaka leo imepita miaka zaidi ya 10 niliapa yule jamaa siku nikikutana naye lazima nitalipa kisasi tu.

Kila nikikumbuka hili tukio huwa natetemeka sana...

Ningekufa kibwege sana.
 
Wananchi wengi hatupo tayari kufuata sheria ila ndo tuko mstari wa mbele kulalamikia watekaji na viongozi wasiofuata sheria. Tanzania watembea kwa miguu wengi huvunja sheria za barabara ila hawawajibishwi. Tukiamka na kuanza kuheshimu sheria itapunguza uhalifu hasa mauaji.
 
Mazali kama haya ya kusingiziwa na kuitwaa mwizi natamani yanitokee yani huo mkono ntakavyoutembeza maamaee.
 
Watanzania wana uwezo mdigo wa akili Sana .

Kipindi nipo Bukoba waliua jamaa mmoja ambaye alikuwa sio mwizi yaani hawafikirii kwa kina waswahili.

Pia nakumbuka kipindi kile Bukoba kuna yale mauaji ya Koromeo around 2014/2015.

Nakumbuka siku moja usiku natoka zangu nyumbani naenda Saloon alikuepo Kijana Fundi umeme anaitwa Baraka alikamatwa na kuanza kupewa kipigo kikali eti anaua watu .

Kumpekua walimkuta na kisu , bisibisi prize Ilawalivyoona hivyo kipigo kikazidi kumbe zilikuwa zana za Kazi yake ya umeme.

Hii kitu ilinifanya nifikirie Sana japo huyo jamaa aliokolewa na police dk kama ya 70%

Ukisikia kelele za mwizi usikurupuke kuua ni hatari Sana.
 
kuna Mwaka mmoja uliwahi kucomment kwenye uzi mmoja hivi ile comment iliweza kumaliza wiki yangu yote kazini comment ilikuwa inasomeka hivi

mleta mada we ni muongo Acha kukaa kwa shemeji acha kupiga nyeto🤣🤣
 
Pole sana ndugu yangu
 
Inaendelea au mwisho.
 
Coincidence gani ya kuzama kwenye nyumba halafu bahati ikawa nyumba ya mjumbe?
Hii ilikuwa ni kama bahati Tu iliyosababishwa na MUNGU..nimekutana na matukio mengi sana kwenye maisha yangu miaka ya nyuma sana niliwahi kupewa kesi ya unyang'anyi wa kuitumia siraha ( armed robbery), wakati nikisubili Vyeti vyangu niliamua kazi ya ulinzi kwenye kampuni moja ya kichina huko jijini. Siku moja Mimi nikiwa nipo mapumzikoni ( sikuingia shift) usiku majambazi walivamia eneo lile . Walinzi wawili walikuwa lindo usiku Huo walifungwa mikono na miguu na kutishiwa kuuawa endapo Tu wangepiga kelele. Wale majambazi walifanikiwa kulizingira eneo lile na baadhi ya wachina waliokuwa wanaishi eneo lile walijeruhiwa kwa mapanga na baadhi ya vitu kama pesa taslimu , simu na kompyuta viliibiwa. Kesho yake ya tukio ilikuwa ni ziara ya waziri mkuu , Katika hotuba yake katika ziara hiyo alisititiza zaidi walinzi wanaolinda eneo hilo ndio kundi linalotakiwa kukamatwa na kutoa maelezo zaidi huenda tukio lile tunalifahamu au sisi ndio tulitengeneza njama ya kuvamiwa wachina hao. Itaendelea............
 
Kinachoniuma Kwa askari wetu hawana maswali yaani unabebwa.na hela unatoa huku kosa huna.

Hata chembe ya aibu hawana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…