Nilivyotapeliwa Tsh 500,000 na wanaoagiza bidhaa kutoka China

maishakujipanga

Senior Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
115
Reaction score
119
Katika harakati zangu za kutafuta maisha.

Kuna jamaa flani akanipa mchongo wa kuagiza mzigo China akaniambia ila niwe na uvumilivu.

Kijana nikajikusanya kila kitu nikafuatilia nikaunganishwa na tapeli mmoja mwanamke alikuwa na ofisi feki Kigamboni.

Alikuwa na acount Instagram Login • Instagram anapost vitu anavyoagiza na alikuwa na group la WhatsApp nikaunganishwa nikatoa oda yangu.

Nikathibitisha muamala nikasubiri mzigo ufike sasa.

Mwezi 1 ukapita, wa 2 wa sita nikashtuka kwenye group niko peke yangu.

Instagram kashafuta picha zote akabadilisha biashara.

Namba yake ni +255 689 652 136, Jina Pendo Minja

Na wasaidizi wake ni 0699 696 598 Salma 0764 643560 Chomba

Sasa hawa mchezo wao ni kutengeneza groups za kuagiza mizigo China, then wanakusanya hela za watu halafu wanavunja group.

Bahati mbaya niko mkoani sikuweza kufatilia zaidi.

Ila nimeona magroup yao sehemu nyingine wanachangisha watu huku wakiwadanganya na picha za bidhaa.

Huu umeshakuwa mchezo wao kuweni makini na hao watu.

Nb. nina ushahidi wa kila kitu

Screenshot_20220223-143536.jpg
Screenshot_20220223-145950.jpg
 
Katika harakati zangu za kutafuta maisha.

Kuna jamaa flani akanipa mchongo wa kuagiza mzigo China akaniambia ila niwe na uvumilivu.

Kijana nikajikusanya kila kitu nikafuatilia nikaunganishwa na tapeli mmoja mwanamke alikuwa na ofisi feki Kigamboni.
Physical adress ni muhimu sana, unatumaje Hela online kwa Mtu usiemfahamu? Kama unataka Kuagiza mzigo china wapo Mawakala kibao wa loose container, Fika ofisini fuata utaratibu.
 
Duh group mlikuwa kama wangapi ? Mnaeza mkajiorganize waliopo Dsm wakaenda police
 
Physical adress ni muhimu sana, unatumaje Hela online kwa Mtu usiemfahamu? Kama unataka Kuagiza mzigo china wapo Mawakala kibao wa loose container, Fika ofisini fuata utaratibu.
Ukiwa mkoani ni ngumu kufika dar, af alikuwa anatangaza ofisi yake kumbe ni feki
 
Physical adress ni muhimu sana, unatumaje Hela online kwa Mtu usiemfahamu? Kama unataka Kuagiza mzigo china wapo Mawakala kibao wa loose container, Fika ofisini fuata utaratibu.
Hawa huwa wanaagiza kwa mfumo wa "crowd funding" ili kupata kwa Bei nafuu.

Kwahiyo huyu hajatapeliwa na Wauzaji. Katapeliwa na mkusanya pesa, maana wengi Ni watu wa mitandaoni wqnaounganishwa tu kupitia WhatsApp group
 
Yah mkusanya pesa, au agent.
Anakusanya pesa anaagiza mzigo mkubwa
 
Back
Top Bottom