Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Umenena Vema! Lakini Kilio Chako Chaweza Kuwa Cha Samaki Machozi Kwenda Na Maji. Namaanisha Sidhani Kama Sauti Yako Inasikika Kwa Njia Hii. USHAURI: Pale Kijijini Kwenu Unapotoka Kapatengeneze Pawe Kama Ulaya Hata Kama Zipo Nyumba Mbili Kaboreshe Pakae Sawa Ili Usijekuaibika Utakapotembelewa Na Rafiki Zako Wa Huko Majuu Ili Ikaaibike Tz Wewe Ukawe Salama Maana Inakuuma Sana
 
Bus station za nini sasa kama hapo Mbezi. Stand tunapita tu. Ulaya wanafikiria mbali.
Hii nchi ina watu wajinga Sana kwenye madaraka yaani wanaona ni sawa kutumia mabilioni kujenga mastendi yasiyo na maana na kuacha kutumia hizo pesa kuleta huduma za msingi za watu ikiwamo kuwapimia watu viwanja waishe kwenye order

Si ajabu hakuna tofauti ya wasomi na wasio wasomi ndio maana Msukuma huwa anaponda Sana wanaojiita wasomi
 
Kwa ijumla miji ya Tanzania kimpangilio, ni ovyo sana.

DSM, sijui utailinganisha na mji gani!!

Achilia mbali miji ya Ulaya, hata ukilinganisha na miji ya Afrika tu, DSM si lolote, si chochote.

Hayo madaraja yanayoitwa flyovers, si chochote. Nilienda wakati fulani Bamako, Mali, nchi ambayo karibia robo tatu ni jangwa, ina mpangikio mzuri, mara 10 zaidi ya Dar. Flyovers wala siyo kitu cha kuongelea, ni kitu cha kawaida, na sijui zipo ngapi!!

Ukienda tu hapo Maputo, mji umejengeka na kupangwa hasa, japo pembeni kabisa huko, ni takataka. Lakini kati kati ya mji, ni mji hasa. Tunajisifu na daraja la Nyerere, letu ni fupi kuliko la Maputo.

Nenda Harare, Dar ni takataka.

Sisi tatizo letu, mafanikio kidogo, kelele ni nyingi sana.
Sasa mbona mataga huwa yanapagawa Sana na kupumbaza watu? Au ndio mentality za kimaskini kuanzia mwili hadi akili
 
Kuna wakati nilikuwa na jamaa waliotoka Ulaya. Tulikuwa kwenye chopa iliyokodiwa toka South Africa. Wale bwana ilikuwa mara ya kwanza kutembelea nchi ya Afrika, nje ya Afrika Kusini.

Tulitua eneo moja mkoani Tabora. Nikawaona wameduwaa. Nikawauliza kuna nini? Wakasema, hawa watu maisha haya wanaoyishi, nikisoma vitabu vya historia kule kwetu, inaonekana ni aheri maisha ya karne ya 18 Ulaya.

Ndiyo maana wenye akili wakimsikia mtu akisema kuwa Tanzania ni tajiri, tupo vizuri - hawawezi kuelewa kama huyo mtu ni mzima kabisa!!
[emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516] [emoji13][emoji13][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Jiwe
 
Havi kweli unafananisha majiji kama london, Berlin, tel Aviv, dotmund etc na mwanza na DSM!!!??
Majiji baadhi ya hayo yana miaka 50-200yrs, pia uchumi wa hayo majiji na yetu kweli lakini unafikia kufananisha london na dsm.
Nimelia sana niseme tu tz ndo kwenu na utarudi mfu au uzikwe huko kama mbwa. Kenge wewe
Vipi Jiji La Kigali na DSm?

Dar chafu vipi kigali. Najua utakimbilia kusema Kigali Ni ndogo ulivyo kilaza wa haja.
 
Ndugu yangu wazungu au jamaa zako wakishangaa sijui tunaishije nawe washangae wanaweza kuishije kwenye apartment ambazo ukipiga hatua huko chooni, hatua upo sitting, hatua nyingine chumba cha kulala. Nyumba utazani ni sero

Kuna siku Mzungu mmoja ni msomi ana PhD, aliwahi ishi Tanzania tulikutana nchi moja Ulaya. Akaanza kuleta dharau ati alienda Arusha watanzania tunapanda katika gari na mbuzi. Eti kwanini mbuzi mnyama na watu wanapanda gari moja.

Nilimtazama, nikamwambia mbona nanyi huku Ulaya tunawashangaa mnapanda na mbwa katika gari la abiria, mbwa ni mnyama. Na mnalala nae kitandani. Ni kamuuliza kuna utofauti ipi na Tanzania? Tanzania uliona Mbuzi kwenye gari huku mbwa kwenye gari na wote ni wanyama.

Mzungu alinitazama akanambia, "umenifundisha kitu. Na umenipa challange"! Toka siku hiyo ananiheshimu sana. Tukawa marafiki wakubwa hadi leo. Na baadae alifall in love. Watanzania tusipende jidharau.
Ko mkuu huwa unapanda na mbuzi kwenye gari [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Vipi Jiji La Kigali na DSm?

Dar chafu vipi kigali. Najua utakimbilia kusema Kigali Ni ndogo ulivyo kilaza wa haja.
Kwa akili ya kawaida tu huwezi fananisha jiji lenye watu 4M na 100k kwenye development na maintanance labda uwe juha.
Kilaza wewe
 
Nawaangalia Halafu Nasema Hii Bhaghosha
😄😃
 
Tanzania Ni Pazuri
Tanzania Ni Tajiri!!
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Limbukeni akioneshwa mwezi hujidai yeye ndiye mwanzilishi wa kuona mwanga;
Wanaokutumia kwa kukulipa pesa ambazo hujui zimetokana na nini ndio waliokujaza kiburi ambacho kabla hujarejea ukimbizini utarejea kwenye jukwaa hili kuomba msamaha.
Kwa nini watu wengi hatupendi kusikia ukweli....na kwa nini tunapenda kusifiwa sifiwa tu...kwani kuna lipi la uongo alilosema mtoa mada....au ni kosa yeye kujaribu kusema na kuamsha hisia kuwa bado tunayo safari ndefu kujilinganisha na ulaya...!!, Tukubali tukatae....kufikia hata robo yao bado ....na ili tufike lazima tukubali pia pale tulipokosea..... Tubadilike.
 
Steve wa HD hatumii lugha za kuudhi bali uhoji kwa staha ingawa wakati mwingine u-provock muhojiwa kwa maswali tatanishi. Na mwisho wa kipindi kama mahojiano yameenda vyema utoa furusa kwa muhojiwa kutoa ushauri kwa jambo husika!
Unataka wote tuwe akina Stive ? Hilo hakuwezekani ndio maana Jiwe hataki ushindani na JK aliweza
 
Swali la kitoto, kama hutaweza kutuambia inahitaji miaka mingapi kufikia hatua yao!! Kuna nchi kama Malaysia, Singapore na Vietnam. Miaka ya 1970s zilikuwa kama sisi. Je leo ziko sawa na sisi???

Kazi yetu sisi kupiga mdomo tu!
Achana na hayo mataga hayana akili,yanatumia mabilioni ya fedha za walipa kodi kujenga eti stand ambazo technically ni useless kwa umma na wanaacha kutoa huduma za jamii na mipango miji.

Hao ni viazi unfortunately ndio wameshika madaraka
 
Kwa tanzania unaweza ilaumu serikali
Lakini #1 ya matatizo hayo ni sisi wenyewe
Ustarabu ni 000000

Ova
Ustaarabu kwani mtu anazaliwa nao? Ustaarabu unatengenezwa na jamii na kwenye umaskini hakuna ustaarabu
 
Wewe huna tofauti na mtu aliyepata senti kidogo anaanza Ku Google madhara ya kula ugali.
 
Shalom,

Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.

Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya ujerumani. Pia ili kukidhi haja ya moyo wangu nimetembelea karibu miji yote mikubwa na midogo ya nchi ninayoishi. Pia nilibahatika kutembelea tel aviv na jerusalem nchini israel. Kwa ujumla matembezi yangu yameniwezesha kujionea landmarks muhimu karibu yote kwenye nchi nilizotembelea. Pia kwa kuwa, mbali na safari ya London, Oslo na nchini Israel ambapo nilipanda ndege miji yote iliyobaki nilisafiri kwa bus ambapo nilipata furasa ya kuiona ulaya kwa undani zaidi hasa highways. Kwa ufupi ulaya imeunganishwa na barabara nzuri sana na zenye ubora wa hali ya juu kabisa. Kuna raha yake kusafiri nchi za Ulaya kwa kutumia barabara.

Baada ya utangulizi sasa naeleza nilivyoiona tanzania baada ya kutua Dar es Salaam.

1. Kwa kuwa tulitua usiku, haikuwa ajabu sana kuiona Dar es Salaam.mfano wa nyota za angani ambazo huwa hazina mpangilio maalum maana naijua vema na hata kabla sijaondoka kwenda ng'ambo nilitua na kupaa mara kadhaa kwa safari za ndani, nilijua Dar es Salaam. ina mipango miji mibovu inayofanya nyumba kujengwa bila mpangilio na hivyo usiku kuonesha taa zilizozagaa kama nyota angani. Tofauti kabisa na unavyoshuka usiku kwenye miji mingine duniani ambapo utaona namna barabara za mitaa na highways zilivyopangwa, na hata taa za mji kuwa kwenye mpangilio maalum. Tofauti na nilivyouacha uwanja wa ndege. Walau mara hii terminal 3 kwa mbali sana nilikiri inaondoa aibu tuliyokuwa nayo, lakini hata hivyo niliona kama bado ni ndogo sana.

2. Baada ya kutua na kuvuka security control nilitoka nje na kukutana na dereva wa "hotel' niliyofanya booking kwa njia ya simu baada ya kuiona kwenye booking.Com, haiko mbali sana na airport, nikili wazi njia nzima kuelekea hotelini, nikiwa na picha ya miji ya ulaya kichwani, niliona mji kuwa ni masikini na mchafu kupindukia. Hotel yenyewe niliyolipia laki moja ambayo kiukweli ni hela ndogo sana kwa euro niliikuta ni ya hovyo, chumbani nilikuta kuna neti ya mbu hiki nacho kilinistua maana Ulaya sikuwahi kulala na neti, pia nilikuta chumba kimepuliziwa dawa ya mbu. Palinishinda ilibidi nitafute sehemu nyingine ya kulala.

3. Kesho yake asubuhi nilisafiri kuelekea Mwanza. Baada ya kutua nilendelea kuona umasikini kama niliouona Dar es Salaam, nyumba za kimasikini zisizopangiliwa vema. Airport mtu anakubebea mzigo kwa vile vigari mpaka kwenye taxi, lakini baadaye anakuomba hela wakati haukukubaliana naye. Sintoongelea sana Mwanza.

4. Siku zangu zilivyokaribia za kurejea Ulaya, nilirudi Dar es Salaam. siku 2 kabla, lengo likiwa ni kuona mechi ya timu ya taifa. Nakumbuka kulipokucha na baada ya breakfast nilimwambia dereva taxi anizungushe dsm niione kwa ukaribu, hasa miundombinu inayoongelewa sana kwamba imeifanya Dar es Salaam kuwa kama Ulaya. Lengo lilikuwa baada ya kuzunguka mimi na dereva taxi tukaone mechi. Nilikubali kumlipa kwa ujumla. Nilimtaka anipeleke tff maana kulikuwa na dada mmoja nilitaka kukutana naye ili aniuzie jezi za timu ya taifa, Daraja la Mfugale, daraja Ubungo, kisha twende Mlimani City kwa ajili ya chakula, kisha daraja la Selandar, baadaye twende Kigamboni kupitia Daraja la Nyerere.

  • Daraja la Mfugale - sina mengi ila niliona ni kama kituta fulani tu kilichojaa umasikini - hakuna la maana la kupiga kelele nyingi
  • TFF - licha ya hela zote wazipatazo nilisikitika kuikuta kama nilivyoiacha, inatia aibu
  • Daraja la kijazi - hakuna kitu, kampala tu mbali na kuihusisha nairobi tunatia aibu kwa kelele tuzipigazo, maana wenzetu wa east africa wako mbali sana kwenye mambo ya flyovers
  • Mlimani City-licha ya kuwa napafahamu sana, niliona kuna ulazima wa kujenga malls kubwa zaidi kama ilivyo kwa nairobi na miji ya south africa
  • Daraja la baharini Selandar
  • Niliona kama tunajipiga wenyewe, kiukweli sikuona umuhimu wa lile daraja, maana kijiographia niliona kama limelazimishwa, nadhani linalenda kuwarahisishia mabalozi na watu wakubwa wakaao maeneo ya Mbezi Beach, Oysetrbay na kwingineko kufikia ofisi zao kiurahisi.
  • Maeneo yote ya Upanga na hata ikulu niliona ni pa hovyo sana, uchafu ni mwingi mno, pengine nimeathiriwa na kuishi miji ambayo eneo lote la mji limewekewa tiles.
  • Barabara ya Ali Hassan Mwinyi niliona kuna majengo yamechomoka kidogo yaliupendezesha mji, maana kiukweli Watanzania tuko obsessed obssessed sana na maghorofa pengine kuliko miundombinu muhimu ikiwamo maji taka na maji safi na umeme, hivyo kiurefu wa majengo tu, dsm inayazidi majiji yote niliyotembelea, labda kwa uimara yanaweza kuwa chini ya kiwango ila si haba.
  • Hatukubahatika kuliona daraja la nyerere maana muda wa mechi ulikuwa umefika.

Mwisho - siyo kwamba napachukia nyumbani lengo la uzi huu ni kutaka tubadilike na ikiwa tunataka maendeleo ya kweli ya miji yetu ni lazima tukubali kujifunza na kuona wenzetu wanafanyaje. Ili dsm yetu iwe na hadhi ya kidunia ni lazima (ukweli mchungu) kubomolewa upya, labda kuacha maeneo machache sana, na kujengwa upya (ni hasara lakini baada ya kujengwa upya faida yake ni kubwa sana)

Nawaomba viongozi wetu watembee, wajifunze jinsi miji inavyojengwa kuna faida kubwa sana kwa kufanya hivyo
1.Kipofu kaona mwezi.
2.Maskini akipata,matako hulia mbwata.
 
Kwetu Mwanza. Nitapaongelea siku ingine. Lengo siyo kujionesha, ama kwamba napachukia nyumbani. TANZANIA NI KWETU. LENGO LANGU NI KWAMBA TUNATAKIWA KUJITATHMINI. KUDHANI TUMEFIKA KUNATUPOTOSHA.

Tuna viongozi wenye upeo mdogo sana! Na wengi wao , kama sio wote, hawajui kuwa hawajui.

madhara yake ni, mfano unapokuja kwenye Mipango, iwe mipango miji au mingineyo ya maendeleo - tuko hoi sana!
  • sio endelevu,
  • ni yakisiasa /kichama inayotegemea sana hulka ya raisi/mwenyekiti wa chama,
  • kama walivyo wapangaji wake, imekosa upeo na mwelekeo mpana,
  • etc.
 
Back
Top Bottom