Niliwaambia wazazi wasubiri niweke mambo yakae sawa wakanigomea, sasa naona yakitimia

Jamaa hajalazimishwa bali yeye kalazimisha kuishi na mtoto wa watu mpaka kumpa mimba. Ukute huko watawahi ili ajifungulie ndoani na Binti kaishi na jamaa anaufahamu uchumi wake hivyo katoa ramani nzima kwa ndugu zake,na majigambo ya hapa na pale ile kujitapa wakaona kibopa wamepata. Cha msingi mleta mada aongee na wazazi wake na washenga wao watamuelewa
Jamaa anasema hana kitu, hayupo tayari kwenda. Sasa kwanini wanamlazimisha.
Jamaa akiwapa room ya kumlazimisha saa hizi, watamfanya hivyo hivyo hata akishaoa.
Kumbuka, 'you teach people how to treat you'.
 
Ya bomani na ya kidini zote sawa kasoro tu ya dini haina talaka(japo mahakama inaweza kutoa)ya bomani inayo ila mgawo pasu kwa pasu upo pale pale. Sherwhe za kukomoana zinatokea kwenye familia ila ukiwa na msimamo harusi haitakufilisi utaenda vile unavyopanga
Hesabu zangu zipo calculated sana hasa na hawa viumbe jinsia KE.

Na sio mtu ninayeogopa kubadilisha geer angani na ndio maana hata ndoa nili opt ya bomani na sio ya kidini.
 
Mi nadhani wanataka Binti yao apate mtoto akiwa kashaolewa/kufunga ndoa inayotambulika .
Faida yake ipo wapi kama nikishindwa kufuata utaratibu wanaoutaka kisha akapata mtoto kabla hajaolewa??
 
🤣 uchumi ni hohaheha ndio maana najaribu kuupambania sana uchumi wangu nisije kuaibika hapo mwezi wa sita.

Shida ninayoiona hapa ni kuendekeza baadhi ya mila ambazo mwisho wa siku zina komoq kwa upande wa muoaji na muoaji akiingia mitini hasara inakua kwao.
 
Budget waliyopanga kwaajili ya hiyo tafrija nikitoa hela alafu wakaenda watu wawili watazidi kuona kama familia yangu imefanya madharau.
Ebwana ndiyo naelewa.

Ila mbona najua kwamba upande wa Kike kama watataka kitu kama hicho gharama inakua juu yao? Au makabila tunatofautiana
 
Faida yake ipo wapi kama nikishindwa kufuata utaratibu wanaoutaka kisha akapata mtoto kabla hajaolewa??

Wazazi wake hawataki kuruhusu Hali hiyo kuzaa mtoto nje ya NDOA.

Wanataka mtoto apatikane akiwa katika Ndoa Halali
 
Sijaelewa yaani ulimgomea binti kurudi kwao hata mahari hujamtolea,na ukapanga sikukuu ale kwenu na sio kwao. Na bado una nguvu ya kuja kulalamika humu daah
Rudia tena kusoma
 
Ebwana ndiyo naelewa.

Ila mbona najua kwamba upande wa Kike kama watataka kitu kama hicho gharama inakua juu yao? Au makabila tunatofautiana
Upande wetu ni tofauti Mkuu
 
Wazazi wake hawataki kuruhusu Hali hiyo kuzaa mtoto nje ya NDOA.

Wanataka mtoto apatikane akiwa katika Ndoa Halali
Ndio wapange tarehe za kunikomoa?? What if nikashindwa kisha binti yao akazalia kwao??
 
Ndio wapange tarehe za kunikomoa?? What if nikashindwa kisha binti yao akazalia kwao??

Unakuaje mwanaume usiwe na msimamo wewe ndiye unaeamua Lini utakuwa tayari kufunga Ndoa kama haupo tayari wao wanalazimisha basi wakae na Binti yao Hadi pale utakapokuwa tayari .. unashindwa kuwajibu hivyo.

Kuwa na msimamo.
 
Niende siku washenga walipotumwa??

Sidhani kama ni appropriate kwa tamaduni za kitz.
 
Haya mambo anayaweza Patric
Haya Mambo ya Pochi nene mwachieni patrickk wa G ndio hamnaga chenga nazo,,
 
T-Bagwell Ndugu yangu, wewe ni mtu mzima, kuendeshwa na wazazi labda utake wewe
Usipokua na msimamo watakupangia mpaka kuzaa

Mimi kama mm mtu hanipelekeshi hasa mambo ya ndoa mimi nagawa dozi ya Muting mpaka akili zinawakaa sawa

Mzazi ukinizingua siji nyumbani wala siongei na wewe

Heshima ifuate mkondo wake
 
Humfai huyo binti utamtesa tu una roho mbaya
 
Huyu hafai kuwa mume wa Uyo binti kitendo cha kusema haamini Dini hafai kuwa Na familia
 
Reactions: Tsh
Kumuogopa Mungu kuna uhusiano gani na niliyoyaandika hapo, wazazi wangu wenyewe wameshangaa kwanini imekua ghafla hivyo na sasa wapo upande wangu.

Je nikimiuacha akaendelea kukaa kwao huoni kama ndio nitaonekana nina madharau??
Madharau unayo
 

Unasema ulishawaonya wazazi wako?

Mtoto kumuonya mzazi ndio mara ya kwanz kusikia Jambo hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…