Niliwahi kumwambia Hayati Dkt. Magufuli, nakwambia na wewe Rais Samia; Watanzania ni masikini sana!

Mwigulu juzi amesema yeye ndo atakuwa waziri wa fedha mpaka mwaka 2030...mtake msitake! Yaani hakuna kitu mnaweza fanya
 
Habari Watanzania wenzangu,

Kuna jambo ambalo naamini viongozi wetu huwa wanalipuuza wakifika kwenye viti hivyo.

Japo Tanzania ina utajiri mwingi sana, lakini Watanzania asilimia kubwa ni fukara sana.

Hii ni kuanzia kwa Mawaziri, Makatibu wakuu, viongozi wa Taasisi mbalimbali, Majaji, Bunge na Wabunge, Wawakilishi, Waziri Mkuu, Makamu na Rais; wote hawahisi kabisa magumu wanayopitia wananchi wengi waliopo ktk umaskini wa kutupwa.

Ukitaka kuthibitisha hili, angalia sera mbalimbali zinazotungwa na serikali. Haziakisi kabisa hali ya maisha ya Watanzania wengi!

SWALI: Shida ni nini?

Tuna sera za kijinga sana, tuna maamuzi mengi ya kipumbavu kweli kweli. Nchi imejaa mikorogano tu.
Ukiulizwa hii sera alitungiwa Mtanzania, hadi unahisi uchungu hadi moyo unataka kuchomoka.

Hawa akina Mwigulu, na Rais wetu Mh. Samia wana shida gani hasa?! Au shida ni vile ving'ora, au saluti wanazopigiwa, au misafara mikubwa mikubwa ile, Mbona hawaelewi kabisa uhalisia wa maisha ya WaTz wengi!

Niliwahi kusafiri hadi Bukombe, Geita huko. Nilimkuta Mwananchi mmoja, ameugua kweli, lakini kwa sababu alikuwa na Sh. 2000 tu. Hiyo hiyo anaitegemea kula, kuhudumia watoto, na kila kitu. Yule ndugu alichukua uamuzi wa kwenda kununua paracetamol (dawa za maumivu) za sh. 400/- ili ameze japo atulize maumivu ya mwili.

Watanzania wa aina hii wapo chungu mzima nchi hii. Mtu anaumwa, hana hela ya kumuona daktari, hana fedha ya vipimo, na wala uwezo wa kununua dawa. Anaamua kununua tu dawa za maumivu.
Si kwamba hapendi kutibiwa, la hasha, kipato kinakataa.

Nikuulize Mh. Rais Samia, huyu Mtanzania akitumiwa na ndugu yake sh 25,000/- aende hospital, mtumaji anakatwa tozo, na yeye akienda kutoa ana tozo. Rais wangu na wewe Dr. Mwigulu mnatengeneza Uchumi wa watu gani? Huu sio wa WaTz, labda mna watu wenu wengine mnaowawaza na kuwahudumia.

Ni wakati sasa Mh. Rais Samia ukate matumizi yote yasiyo ya lazima ndani ya serikali yako.

Haiwezekani Waziri, Naibu Waziri, Katibu mkuu, Wakuu wa Taasisi, Mamlaka mbalimbali, mkuu wa mkoa, n.k, atembelee gari ya thamani ya Tsh. 400 million, huku kuna Kijiji kizima hakina Zahanati, Kuna shule haina choo, kuna shule hawana madawati. Halafu unaweka Tozo kwenye sh. Elfu 10, unajiita Mzalendo, na tai ya rangi ya Tanzania unavaa. UNAFIKI!

KATA MATUMIZI YOTE YASIYO YA LAZIMA, KABLA HATUJAKWAMA KAMA TAIFA.

Watanzania ni fukara sana. Isipokuingia akilini hii, 2025 watakulazimisha upishe mwingine.
Kitendo Cha kumnyima pesa mfanyakaz wa serikali haya ndiyo maumivu yake
 
Mkuu nikisema upande mwingine hizi tozo tunazizingizia sana but ukweli kama tunataka kulikomboa taifa inabidi tuchek how we can save big money for our people na sio hizo petty monies
Katika hio transaction hapo tozo hazifiki buku but kama serikali ikiwekeza heavily kwenye kilimo na ufuguaji hao waTz wengi zaidi wataweza tengeneza pesa kubwa zaidi ya hio

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app

Kuna nchi serikali inasupport wananchi wake sana na zinaendelea sana tucheki hata Zambia na Rwanda wako mbali sana. Zambia ukubwa unakaribiana na TZ na bado ni locked country plus ina population ndogo sana. Why watushinde hakuna mwenye madini,mbuga za wanyama,bahari kama sisi ila sasa maisha yetu maigizo
 
Habari Watanzania wenzangu,

Kuna jambo ambalo naamini viongozi wetu huwa wanalipuuza wakifika kwenye viti hivyo.

Japo Tanzania ina utajiri mwingi sana, lakini Watanzania asilimia kubwa ni fukara sana.

Hii ni kuanzia kwa Mawaziri, Makatibu wakuu, viongozi wa Taasisi mbalimbali, Majaji, Bunge na Wabunge, Wawakilishi, Waziri Mkuu, Makamu na Rais; wote hawahisi kabisa magumu wanayopitia wananchi wengi waliopo ktk umaskini wa kutupwa.

Ukitaka kuthibitisha hili, angalia sera mbalimbali zinazotungwa na serikali. Haziakisi kabisa hali ya maisha ya Watanzania wengi!

SWALI: Shida ni nini?

Tuna sera za kijinga sana, tuna maamuzi mengi ya kipumbavu kweli kweli. Nchi imejaa mikorogano tu.
Ukiulizwa hii sera alitungiwa Mtanzania, hadi unahisi uchungu hadi moyo unataka kuchomoka.

Hawa akina Mwigulu, na Rais wetu Mh. Samia wana shida gani hasa?! Au shida ni vile ving'ora, au saluti wanazopigiwa, au misafara mikubwa mikubwa ile, Mbona hawaelewi kabisa uhalisia wa maisha ya WaTz wengi!

Niliwahi kusafiri hadi Bukombe, Geita huko. Nilimkuta Mwananchi mmoja, ameugua kweli, lakini kwa sababu alikuwa na Sh. 2000 tu. Hiyo hiyo anaitegemea kula, kuhudumia watoto, na kila kitu. Yule ndugu alichukua uamuzi wa kwenda kununua paracetamol (dawa za maumivu) za sh. 400/- ili ameze japo atulize maumivu ya mwili.

Watanzania wa aina hii wapo chungu mzima nchi hii. Mtu anaumwa, hana hela ya kumuona daktari, hana fedha ya vipimo, na wala uwezo wa kununua dawa. Anaamua kununua tu dawa za maumivu.
Si kwamba hapendi kutibiwa, la hasha, kipato kinakataa.

Nikuulize Mh. Rais Samia, huyu Mtanzania akitumiwa na ndugu yake sh 25,000/- aende hospital, mtumaji anakatwa tozo, na yeye akienda kutoa ana tozo. Rais wangu na wewe Dr. Mwigulu mnatengeneza Uchumi wa watu gani? Huu sio wa WaTz, labda mna watu wenu wengine mnaowawaza na kuwahudumia.

Ni wakati sasa Mh. Rais Samia ukate matumizi yote yasiyo ya lazima ndani ya serikali yako.

Haiwezekani Waziri, Naibu Waziri, Katibu mkuu, Wakuu wa Taasisi, Mamlaka mbalimbali, mkuu wa mkoa, n.k, atembelee gari ya thamani ya Tsh. 400 million, huku kuna Kijiji kizima hakina Zahanati, Kuna shule haina choo, kuna shule hawana madawati. Halafu unaweka Tozo kwenye sh. Elfu 10, unajiita Mzalendo, na tai ya rangi ya Tanzania unavaa. UNAFIKI!

KATA MATUMIZI YOTE YASIYO YA LAZIMA, KABLA HATUJAKWAMA KAMA TAIFA.

Watanzania ni fukara sana. Isipokuingia akilini hii, 2025 watakulazimisha upishe mwingine.
Umezungumza kwa hisia. Kuhusu hoja ya umasikini vijijini; tunakubaliana kimsingi ni tatizo kubwa. Rural poverty ni tatizo kubwa si tu Tanzania bali ktk devoloping countries, hasa za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Chanzo kikubwa; ni kutokufanya mapinduzi ya kilimo. Kwa sababu rural economy ktk hizo nchi inategemea kilimo, lakini poor teknoloji, black market na ukosefu wa mitaji na utaalamu umefanya kilimo cha kujikimu, hivyo mnyororo wa umasikini tena wa kurithi (generational poverty) kuzidi kukua. Umasikini wa kurithi yaani masikini anazaa masikini hadi vijukuu. Kwa msingi huo, issue siyo tozo bali kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo. NDICHO ANACHOKIFANYA MHE. RAIS SAMIA. Nampongeza sana Mhe. Rais.

Rais anafanya mapinduzi ya kilimo. Tusaidie mawazo kufanikisha mapinduzi ya kilimo maana ni mfumo endelevu wa uchumi na wa kukata mnyororo wa umasikini vijijini, kuhakikisha food security, kujenga taifa la watoto wenye lishe bora hivyo kuondoa udumavu wa akili na mwili. Tumsaidie Mhe. Rais SSH.🙏🙏🙏
 
Kuna nchi serikali inasupport wananchi wake sana na zinaendelea sana tucheki hata Zambia na Rwanda wako mbali sana. Zambia ukubwa unakaribiana na TZ na bado ni locked country plus ina population ndogo sana. Why watushinde hakuna mwenye madini,mbuga za wanyama,bahari kama sisi ila sasa maisha yetu maigizo
Kweli kbs. Lkn ktk serikali ukiwa na mamwinglu, msukma na yule mhindi, hakna ubunifu, wakisoma walichosema wengne, hata bila kupigia mahesabu wanakileta kwetu. Wamekosa ubunifu, wamelewa pesa
 
Viongozi Wana umasikini wa akili wananchi Wana umasikini wa kipato
 
Msipofanywa kuwa masikini watawaongozaje sasa?
 
Si ajabu kukuta hata timu zao za mpira zinasapotiwa kwa kodi zetu
 
Back
Top Bottom