Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Baati ulinunua shilling ngapi?
Bati nimenunua Sh. 4,800,000 zote na hakuna baki hata moja. Hizo ni Bati pamoja na kofia na valley. Bati nilinunua elfu 31 kwa bati moja sawa na 10333 kwa Mita moja ya bati la geji 30. Hiyo ni bei ya Septemba au Oktoba 2021
 
Tiles za robo nusu chumba zinaweza kutegua mguuπŸ˜…. All in all kila mtu na mtizamo wake maana hata ukifanya wiring lazima uweke ceiling unless uwe umeshahamia au una mlinzi. Muhimu kama unadunduliza uwe na target
 
Labda kama huna pakuweka lakini kama unapo unajikongoja tu. Mwingine anaweka msingi anakimbia. Kila hatua dua
 
tia kashata madirishani mengine unafanya ukiwa humo ndani
Grill Mlango wa mbele na nyuma,kwa wakati husika Mlango utakua maPazia

kuna boya mmoja napga nalo story kila siku lishamaliza kupaua,lishatia grill madrisha yote

ila linalalamika kila siku halina hela linatafuta hela ndio lihamie kwake, mi imefika wakati namwambia

mwanangu usiniletee mastory yako ya huna hela,shida unazitaka mwenyewe,lipo tunaendelea nalo umia

kwenye ma kodi yale unampa mwenye nyumba hela huku roho inakuuma,una nena kwa lugha zote kimoyo moyo,ila halikomi wala halijifunzi.
 
hiyo kodi ya miezi sita tayari umeshapiga bonge la hatua. alafu bwana uzuri wa ujenzi kadri unavyomaliza chumba kimoja ndio unapata stimu na una pambana zaidi ili na vyumba vingine vipendeze. dawa ni kuhamia tuu alafu mengine humo humo
 
wakukujua watakufanyaje mbona watanzania tunaishi kama digidigi...
Tumeshakaririshwa kuwa JF hautakiwi kujulikana,nahisi watu wanatambaa na hiyo imani

Ajabu et hadi wachungaji na masheikh wa humu eti nao wanaogopa kutaja wanahubiri wapiπŸ˜‚
 
hutajenga kamwe kwa hesab hizo.chchot kidg peleka site uone maajabu
 
Binafsi naamini finishing kwangu itakuwa rahisi sana kwasababu naweza kufanya kidogo kidogo kwa kila kitu
uwe na moyo wa uvumiliv.kwa maana kuweza kutoudhika kwa zile vumb vumb mchanga ila finishnig ukiw ndan easy kila basd ya mda unasogez kitu fulan
 
Nani kasema finishing kwa miaka 3? Nimekwambia kujenga BOMA na kuezeka inawezekana kwa miaka 3@2*5m=7.5m.

Sio kila nyumba ya vyumba 3 basi ni kubwa,,kuna nyumba za vyumba 3 hazizidi 90sqm so inategemea na ramani na upatikanaji wa materials za ujenzi.
 
Mdanganye aingie na 7.5m sasahivi aone, labda kama anajenga ilmradi, hebu pigia Nondo tu za mm12 zitakazohitajika kwenye beam ya lenta kwa bei ya sasahivi, ukitoka hapo njoo kwenye bei ya cement (mifuko itakayotimika katika ratio ambayo ni standard), akianza msingi tu kwanza ni lazima ajikune kichwa.

Hatoboi kwa 7M hiyo nyumba unayosema ndani ya miaka mitatu, labda mitano na hapo itategemeana kama vifaa vya ujenzi havitaendelea kupaa.
 
Pole Sana naweza kumpa ramani ya vyumba 3 na kama yuko mkoani ambako atatumia tofari za kuchoma na udongo wa mfinyanzi kujenga atatoboa vizuri tuu..

Mbao bei itategemea mkoa uliko na aina ya mbao unazotaka kutumia,mikoani kuna options nyingi sio lazima za Njombe/Mafinga.

Kuhusu nondo usikariri hujengi ghorofa unatumia 8mm unafunga 3 Kwa ringi hapo haizidi 50,000 badala ya kununua 12 mm mbili kwa 52,000..Mwisho unaweka beam ukuta wa nje hakuna haja ya Kuta za ndani hazibebi mzigo ..

Kama uko mkoani nipe 7.5m nikujengee hadi kupaua.
 
Uko sahihi kabisa, kwa Mkoani hiyo hela unaweza maliza boma ambalo halijaezekwa, hasa kwa Mkoa na Iringa Ujenzi rahisi sana. Msingi unatumia mawe, unaweza weka beam au usiweke wala haina shida, na binafsi huwa sioni watu wa Iringa wakiweka beam.

Ila hiyo hela kwa eneo kama Chalinze, inaishia kwenye msingi tu na inaweza isitoshe, maana pale mahali sijui pana udongo gani, nyumba zinapasuka vibaya sana.
 
vipi wenye kipato cha 4000 kwa siku tunaruhusiwa kukoment au tuendelee kuzimaliziaa kwa wamama watembeza karanga
 
Hapo sasa nadhani tutakuwa tumeelewana, ni kwamba kwa hiyo 7.5M atatakiwa kuminimize cost kwa kuchagua option ya chini kabisa katika kila stage ya ujengaji wake.
 
Unaezaka,BOMA gani unajenga kwa mil.7.5 😁😁😁
 
Unaezaka,BOMA gani unajenga kwa mil.7.5 😁😁😁
Mmmh we jamaa umezidi sasa, nyumba ya vyumba vitatu uijenge hadi kupaua kwa 7.5 M??πŸ˜…

Sio nyumba ni kajumba , nimavyojua mimi, msingi tu wa maana utachukua zaidi ya 2.5M endapo akijenga kwa kujibana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…