Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
- Thread starter
- #221
Kaka , Ahsante kwa kunishambulia ila hoja yangu ipo very clear sitetei na sitawahi kutetea uhalifu, hata ukisoma nilichokiandika .Nchi yetu Ina katiba ,sheria za mienendo ya Makosa ya jinai ,PGO,Kanuni za Jumla za Adhabu sheria zote hizi zimeweka utaratibu wa kushughulikia makosa ya uhalifu .We nae kumbe huna akili, unawatetea hao majambazi, inafaa nawewe ukamatwe upewe stahiki yako,
Yaani ungejua hao vijana jinsi walivyo jeruhi watu kule maeneo ya tegeta na kunduchi, kawe wameua kabisa, na kwingineko pia,Tena polisi wameua wachache Sana hao majambazi
Hakuna sehemu Polisi amepewa mamlaka ya kuuwa mtu kama njia ya kupambana na uhalifu , Polisi wamepewa wajibu wa kuchunguza na kupeleleza sio kuhukumu kwa kupiga mtu Risasi ni Mahakama tuu ndiyo yenye jukumu la kutoa adhabu iwe ni adhabu ya kifo ,kifungo Cha maisha au miaka yeyote hayo hufanywa na Mahakama. Mimi unanishambulia Nina taka Sheria tulizojiwekea tuzifuate na kuziheshimu ,kama hatuzitaki zimepitwa na wakati ktk kupambana na uhalifu tuzibadili, kwanini tuzivunje ???
Ndio maana tuna sheria,katiba , kanuni na taratibu zimeweka utaratibu wa namna ya kupambana na uhalifu .
Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi , ndio maana kuna Mahakama ,ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa.
Hata hao Panya Road wanaofanya uhalifu sheria zipo wakikutwa na hatia wanaadhibiwa sawa na sheria inavyosema kuna kifungo adhabu ya kifo , kifungu cha maisha ,miaka 30 na adhabu zingine . Kwanini wasishtakiwe kwa mujibu wa sheria wajibu wa Polisi ni kufanya upelelezi na uchunguzi kuisaidia Mahakama kufanya maamuzi sio kuuwa watuhumiwa.
Kama tunaona hakuna haja ya kuchunguza na kushtaki Polisi washinikize sheria zibadilishwe ili iwe rahisi wao kufanya wanachokifanya , hakuna mtu anatetea wahalifu ,ninachotaka utaratibu ufuatwe ktk kupambana na uhalifu na kama sheria zetu ni Butu basi tuzibadili na sio Polisi kuchukua hatua ya kuuwa Watuhumiwa bila kuwapeleka mahakamani.